NYUMBA YA WALIMU YAJENGWA KWA VIWANGO SHULE YA MTEMI CHILOLOMA
Na.
Dennis Gondwe, DODOMA
KAMATI
ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na viwango vya ujenzi wa nyumba ya
walimu ‘two in one’ katika Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma na kusema kuwa
utakuwa imejengwa kwa viwango bora.
![]() |
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga akiongea na umma baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya walimu (two in one) |
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga
alipoongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua utekelezaji
wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Mbaga
alisema kuwa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na ujenzi wa nyumba ya
walimu shuleni hapo. “Mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu ni nzuri na umejengwa
na kusimamiwa vizuri. Huko zamani wahandisi walikuwa nyuma katika kusimamia
miradi ya ujenzi, lakini siku hizi wapo mstari wa mbele na wanafika katika
kusimamia miradi ya ujenzi. Jukumu letu ni kuwaambia wananchi kazi nzuri
inayofanywa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hapa tumeambiwa zilitolewa
shilingi 95,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu ‘two in one’ na
sasa zimeletwa shilingi 216,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato
cha tano na sita” alisema Mbaga.
Akisoma
taarifa ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa
Dodoma, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma, Mwl. Livinus Tangayika alisema
kuwa serikali kupitia mradi wa kuboresha shule za sekondari (SEQUIP) ilitoa
jumla ya shilingi 95,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu ambapo
lilikuwa ni hitaji kubwa kwa sababu eneo la shule liko mbali na eneo la makazi
ya watu. Fedha za ujenzi ziliingizwa katika akaunti ya shule tarehe 20/6/2023
na kuvuka mwaka na kuanza kutumika katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Akiongelea
utekelezaji wa mradi huo alisema kuwa ulianza tarehe 9 Septemba, 2023 baada ya
taratibu za manunuzi kukamilika na ujenzi unatekelezwa kupitia ‘force account’.
“Mradi huu unahusisha
ujenzi wa nyumba moja ya walimu (two in one) yenye vyumba vitatu, sebule, jiko
na stoo kwa kila nyumba. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 99 ikiwa
bado milango michache ambayo ipo kwa fundi katika hatua ya umaliziaji pamoja na
ufungaji wa vyoo viwili vya kukaa. Mradi unategemea kukamilika kabla au ifikapo
tarehe 25 Novemba, 2023 tayari kwa matumizi” alisema Mwl. Tnganyika.
Kuhusu faida za mradi ukikamilika, alizitaja kuwa
ni walimu kukaa kwenye mazingira ya shule na hivyo kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi. Nyingine ni kuwezesha mazingira mazuri ya kuishi kwa walimu,
aliongeza.
![]() |
Nyumba ya Walimu Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma |
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa Shule ya Shule ya
Sekondari Mtemi Chiloloma umetumia kiasi cha shilingi 94,823,000 hadi wakati Kamati
ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma inaitembelea.
MWISHO
Comments
Post a Comment