Wananchi wa Kata ya Mtumba wanufaika na Mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri
Na. Leah Mabalwe, MTUMBA
Kata
ya Mtumba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma yapatiwa jumla ya shilingi 83,000,000
kwaajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na
watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mtumba, Huruma Mwigune
Hayo
yalielezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mtumba, Huruma Mwigune wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo
katika kata hiyo.
Alisema
kuwa wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri imewawezesha
kuendesha maisha na kukuza kipato. “Katika wanufaika wa mikopo ya asilimia 10,
Kata ya Mtumba ni miongoni mwa kata ambayo imenufaika na mkopo wa jumla ya
shilingi 83,000,000 kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Mkopo ulitolewa kwa baadhi ya
vikundi vilivyokidhi vigezo na kikundi kimojawapo ni kikundi cha wanawake Ngalawa
kinachojishughulisha na ushonaji. Kwa kweli mkopo huu unatunufaisha kwa kiasi
kikubwa tumejikita kufanya shughuli mbalimbali tofauti na hapo awali” alisema
Mwigune.
Nae mjumbe wa kikundi cha Ngalawa, Monica Petro aliishukuru serikali kwa kuwainua kupitia mikopo ya asilimia 10 inayowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha. “Mikopo hii kwa kweli imetuinua kwa kiasi kikubwa kwa kuendesha shughuli mbalimbali hususan katika familia zetu kwa kujipatia kipato, kipindi cha mwanzo tulikuwa na vishughuli vyetu vidogo vidogo ambavyo tulikuwa tunajichanga changa sisi wenyewe” alishukuru Petro.
MWISHO
Comments
Post a Comment