Agenda ya Lishe yaongeza Ari ya usomaji S/M Dodoma Makulu
Na. Abdul Iddi, DODOMA MAKULU Shule ya Msingi Dodoma Makulu imeshukuru agenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya lishe shuleni kwa sababu inawaongezea ari ya kusoma na kupata matokeo yanayokusudiwa. Shukrani hiyo ilitolewa na Mwalimu wa Lishe, Rehema Kalinga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari waliotembelea shule ya msingi Dodoma makulu kujionea hali ya lishe kwa wanafunzi shuleni hapo. Alisema kuwa shule yake inazingatia ajenda ya Lishe kwa kuwapa wanafunzi wote kuanzi awali mpaka darasa la Saba uji. Darasa la Nne na la Saba kupata chakula cha mchana. “Toka ajenda hii kuanza kutekelezwa, tumeanza kuona matokeo Chanya. Kwanza kwakupunguza utoro, pia watoto darasani wanafundishika” alisema Mwl. Kalinga. Aidha, alitoa pongezi kwa wazazi kwa kusikiliza ajenda ya Lishe na kuitekeleza bila kusuasua kwasababu waliweza kutoa mchango kwa kiasi walicho kubaliana na kamati ya wazazi wa shule hiyo. “Muitikio ni mkubwa kwasababu watoto wote katika Shule ya Dodoma Makulu wanapata uji ...
Comments
Post a Comment