Na. Halima Majidi, DODOMA Wananchi wa Kata ya Makutupora, jijini Dodoma, wameeleza kilio chao juu ya changamoto kubwa zinazowakabili, zikiwemo ukosefu wa maji safi, matatizo ya umeme, pamoja na shule kuwa mbali, hali inayowakwamisha katika shughuli za kila siku. Wakizungumza katika mkutano wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika Kata ya Makutupora, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema wamekuwa wakikumbana na shida ya maji kwa muda mrefu, huku wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu. Akitoa kero hiyo, mkazi wa Mtaa wa Sekondari, Pasisi James, alisema kuwa, tangu kuhamia katika mtaa huo ni miaka mingi hivyo ameiomba serikali kuwasogezea huduma ya maji kwa sababu imekuwa ni changamoto kubwa na hivyo kushindwa kuendelea na kazi zao za kila siku. “Maji ni tatizo hapa kwetu, tunamiaka mingi tangu kuhamia hapa, nimekuja hata kusoma sijui mpaka leo bado tunahangaikia maji, tunachukua maji kwa wachina dumu moja hilo hilo ufulie pamoja na kunywa, hapo naomba mtusaidie” ...
Comments
Post a Comment