Mkoa wa Dodoma wamtakia heri ya kuzaliwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na. Dennis Gondwe, KIKOMBO
MKOA wa Dodoma
umempongeza na kumtakia heri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha marefu ili
aendelee kuwaongoza watanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule |
Pongezi hizo
zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika halfa ya
kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika
katika makao ya taifa ya kulelea watoto- Kikombo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Senyamule
alisema “sisi Mkoa wa Dodoma tunatoa pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza umri akiwa na nguvu na afya
njema na maono ya kuliongoza taifa. Chini ya uongozi wake tunafuraha na amani”.
Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma alimtaja Rais kuwa ni mtu mwenye hekima sana na mchapa kazi. “Mheshimiwa
Rais ametujengea uhusiano mzuri ndani na nje ya nchi. Hakika uongozi wake
umeifanya Tanzania kuwa nchi pendwa duniani. Ameonesha kuwa anapenda haki na
amefanya kila mtanzania aone furaha ya kuwa Mtazania, amekuwa mpatanishi wa
umoja wa kitaifa. Kazi kubwa anayoendelea kuifanya ni kulinda rasilimali za
watanzania” alisema Senyamule.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri |
Katika salamu za
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alisema kuwa Jiji la Dodoma
linajivunia kazi kubwa inayofanywa na Rais ya uwekezaji akisema kwa Dodoma ipo
katika moyo wa Rais.
Nae Mkuu wa Wilaya
ya Chemba, Gerald Mongella alisema kuwa watanzania wanajukumu kubwa la
kumuombea Rais awe na afya na maisha marefu ili aweze kutekeleza maono yake kwa
watanzania.
Hafla ya
kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ilihudhuriwa na
viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mamlaka za
serikali za mitaa, viongozi wa dini, vyama vya siasa na mwakilishi wa mfuko wa
Abbot Tanzania.
MWISHO
Comments
Post a Comment