MABARAZA YA ARDHI YANAMCHANGO KATIKA KUSULUHISHA MIGOGORO YA ARDHI
Na. Eleuteri Mangi, WANMM
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mabaraza
ya Ardhi na Nyumba imeshiriki uzinduzi wa Wiki ya Sheria jijini Dodoma
yakiongozwa na Mhe. Dkt. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Tanzania.
Uzinduzi huo umefanyika Januari 27, 2024 katika viwanja vya
Nyerere Square jijini Dodoma ukitanguliwa na matembezi ya uzinduzi wa Wiki ya
Sheria ambao umehusisha viongozi mbalimbali wa mahama, watumishi wa umma na
wananchi kutoka jiji la Dodoma.
Akizungumzia ushiriki wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, Mwenyekiti
wa Baraza la Ardhi Dodoma Bw. Jackson Kanyerinyeri amesema kuwa moja ya jukumu
lao ni kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hilo katika masuala ya
ardhi, migogoro ya ardhi namna inavyotatuliwa katika mabaraza hayo hadi
kutolewa hukumu.
Bw. Kanyerinyeri ameongeza kuwa wamepata wasaa mujarabu wa
kuwaeleza wananchi juu ya mabadiliko ya Sheria Na 3 ya 2021 ambayo imeondoa
mamlaka ya mabaraza ya Kata kusikiliza kesi za migogoro ya ardhi badala yake
mabaraza hayo yana jukumu la kusikiliza na kusuluhisha migogoro baina ya
wananchi ikishindikana migogoro hiyo iwasilishwe Baraza la Ardhi na nyumba la
wilaya na kupewa cheti ndani ya siku 30.
Aidha, Bw. Kanyerinyeri ameongeza kuwa wanaendelea kuwasistiza
wananchi wamalize migogoro ya ardhi kwa nyia ya mazungumzo na mapatano hatua
inayookoa muda, kuondoa uhasama na inawapa wananchi muda wa kufanya shughuli za
maendeleo na kuinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Wiki ya Sheria 2024 imeanza Januari 24 na inatarajiwa
kuhitimishwa Januari 30 yakiongozwa na kaulimbiu “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa
Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha Mfumo Jumuishi wa
Haki Jinai”
Comments
Post a Comment