UMISSETA kuandaa vijana katika sekta ya Michezo Dodoma

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

MASHINDANO ya Umoja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Tanzania (UMISSETA) ni takwa la kikanuni katika mitaala ya sekta ya elimu kwa lengo la kuwaandaa wanafunzi kuwa mahili katika sekta ya michezo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Peter Ititi alipokuwa akiongelea maandalizi ya michezo hiyo jijini Dodoma.

UMISSETA ni michezo muhimu kwa wanafunzi na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ujumla. “Michezo imetajwa kwenye mitaala ya elimu kutokana na umuhimu wake. Michezo hiyo inalenga kuibua vipaji na kuviendelea kwa maslahi mapana ya taifa. Michezo pia ni ajira na tumekuwa tukishuhudia vijana wetu wakishiriki katika ligi mbalimbali” alisema Ititi.

Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mwaka 2024 ilitoa wanafunzi 56 kati ya wanafunzi 120 waliochaguliwa kuunda timu ya UMISSETA ya Mkoa wa Dodoma iliyoshiriki kitaifa. “Mwaka huu matarajio yetu ni kuchukua makombe yote na tumejipanga kupeleka vijana wengi zaidi” alisema Ititi. 





MWISHO

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lapewa angalizo lishe bora kwa wananchi

RC Dodoma apongeza wafugaji kwa ushiriki wa Paredi ya Mifugo

Rais Samia: Tumieni kikamilifu Miundombinu, Teknolojia na mitaji iliyowekezwa katika Kilimo, Uvuvi na Mifugo