UMISSETA Jiji la Dodoma yaanza Dodoma Sec
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MASHINDANO
ya Umoja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya kanda za
Halmashauri ya Jiji la Dodoma yameanza katika viwanja vya Shule ya Sekondari
Dodoma kwa lengo la uunda timu ya jiji hilo itakayoshiriki katika mashindano
ngazi ya halmashauri ili kuunda timu ya Mkoa wa Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Peter Ititi alipokuwa akiongelea maandalizi ya michezo hiyo jijini Dodoma.
Ititi
alisema kuwa halmashauri iliunda kanda sita zikiwa na shule tofauti tofauti za
sekondari kwa lengo la kuzishindanisha. “Kila kanda ilitoa timu moja
inayoshiriki michezo yote. Hivyo, baada ya mashindano haya itaundwa timu ya Halmashauri
ya Jiji la Dodoma itakayoshindana na timu za halmashauri nyingine ili kuunda
timu ya Mkoa wa Dodoma” alisema Ititi.
Michezo
inayochezwa katika mashindano ya UMISSETA ni mpira wa miguu kwa wavulana na
wasichana, mpira wa mikono wavulana na wasichana, mpira wa wavu wavulana na
wasichana, mpira wa kikapu wavulana na wasichana, mpira wa meza wavulana na
wasichana, mpira wa pete wasichana. Michezo mingine ni fani za ndani
zinazohusisha ngoma, kwaya na muziki wa kizazi kipya pamoja na mashindano ya
usafi.
Comments
Post a Comment