DC DODOMA APONGEZA ZAHANATI YA KIKUYU KUBORESHA MANDHARI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameipongeza
Zahanati ya Kikuyu kwa kuboresha mandhari na kuyafanya ya kuvutia na kupanda
miti kwa lengo la kuwa na hewa safi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shemimweri akiongea na mamia ya wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini |
Pongezi hizo alizitoa alipoongoza zoaezi la usafi wa
mazingira na kupanda miti katika zahanati hiyo iliyopo katika Kata ya Kikuyu
Kaskazini jijini Dodoma.
Shekimweri alisema “niungane na Mheshimiwa Mbunge
kuwapongeza kwa dhati Zahanati ya Kikuyu ikiongozwa na Mganga Mfawidhi kwa wazo
la kuboresha mandhari ya zahanati yao. Ni dhamira yetu tutafute ‘model’ ya
uangalizi wa mazingira katika maeneo yetu ya kutolea huduma ya afya. Mbunge
amening’ata sikio kuwa atabadilisha paa siyo kwa kupaka rangi bali yeye ataleta
mabati mapya”.
Aidha, alitoa rai kwa vituo vingine vya afya kuboresha
mandhari yake. “Rai kwa vituo vingine vya afya katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma kuboresha mandhari. Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma upo hapa.
Ninakupongeza kwa kazi nzuru unayoifanya kwa kujenga timu nzuri kwenye
divisheni yako pametulia hapana mvutano, lililofanyika hapa likaakisi maeneo
mengine.
Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method aliyenyoosha mkono wa kuume |
Ikumbukwe kuwa Zahanati ya Kikuyu ilianza mwaka 1970
ikiwa ni moja ya zahanati kongwe katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
MWISHO
Comments
Post a Comment