WANANCHI CHAMWINO WAJITOKEZA USAFI WA MAZINGIRA
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO
KATA ya Chamwino iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma yatekeleza zoezi la usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa
wananchi kijitokeza kwa wingi na kufanya usafi katika maeneo ya jumuiya.
![]() |
Zoezi la usafi likiendelea |
Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema
kuwa zoezi la usafi wa pamoja wa kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi lilifanyika
katika mitaa minne ya kata hiyo. “Nikuhakikishie kuwa usafi wa Jumamosi ya
mwisho wa mwezi umefanyika katika mitaa yote minne ya Kata ya Chamwino. Mtaa wa
Nduka, Mailimbili, Sokoine na Mwaja” alisema Nkelege.
Akiongelea maeneo yaliyofanyiwa usafi wa pamoja, aliyataja
kuwa ni makorongo, kusafisha mitaro na maeneo ya biashara. “Mtaa wa Mwaja na
Nduka iliungana na kufanya usafi wa pamoja katika korongo. Usafi huo ulihusisha
kuondoa mifuko ya plastiki, kufyeka vichaka na nyasi zilizoota ndani ya
korongo. Mtaa wa Mailimbili usafi wa pamoja ulifanyika katika mtaro wa barabara
ya kwenda Arusha. Usafi huo ulihusisha kutoa taka ngumu kama makopo, mifuko ya
plastiki na kufyeka vichaka na vyasi zilizoota pembezoni mwa barabara na mtaro”
alisema Nkelege.
Aliongeza kuwa wakazi wa Kata ya Sokoine walifanya
usafi katika makazi yanayowazunguka na maeneo ya biashara.
Kata ya Chamwino iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi wake kushiriki mazoezi ya
usafi wa pamoja na kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa maelekezo ya
serikali.
MWISHO
Comments
Post a Comment