Posts

Showing posts from May, 2025

Shilingi Milioni 473 kutekeleza Mradi wa Ufungaji CCTV Kamera Jiji la Dodoma

Image
Na. Josephina Kayugwa, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesani mkataba na Kampuni ya Wisjane Smart Systems kwaajili ya ufungaji wa kamera za usalama barabarani (CCTV) unaogharimu shilingi 473,000,000 ikiwa ni mradi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu. Akitoa taarifa ya mradi, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa mradi huo utakwenda kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dodoma kwasababu kamera hizo zitafanya kazi masaa 24. “Mradi huu wa gharama ya shilingi 473,000,000 utahusisha ufungaji wa kamera kwenye barabara zinazoinga njia kuu lakini pia hapo baadae utakuja kuimarishwa zaidi kwa kuongeza sehemu nyingine za kuweka kamera lengo ni kupata picha zote za vyombo vya usafiri vitakavyokuwa vikiingia na kutoka katika Jiji la Dodoma” alisema Fungo. Aliongeza kuwa wana mpango wa kuunganisha mfumo huo na taasisi nyingine ili kuimarisha ulinzi na usalama. “Mfumo huu baada ya muda tuta...

Shule ya Sekondari ya Bil. 3.9 kujengwa Kata ya Chahwa

Image
Na. Emanuel Charles, CHAHWA Hafla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Chahwa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 baina ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkandarasi kutoka Gopa contractors Tanzanian Limited imefanyika katika Kata ya Chahwa ukilenga kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi. Mradi huo unatekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukiwa ni ujenzi wa shule ya ghorofa nne yenye madarasa 12, maktaba pamoja na maabara nne, chumba cha TEHAMA na jengo la utawala na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja. Akizungumza katika utiaji saini wa ujenzi wa shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuleta miradi mikubwa katika maeneo ya nje ya Mji wa Dodoma. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa mradi huu mkubwa kwasababu unaenda kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, ndugu zangu ni wakati sasa maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma yanufaike...

Soko la Sabasaba kuongozwa kwa misingi ya uongozi bora

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Kaimu Mkuu Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abdul Chacha amewaasa viongozi wa Soko la Sabasaba kuzingatia weledi katika kufanya kazi zao ili kuiishi dhana ya uongozi bora. Aliyasema hayo katika mafunzo waliyoandaa kwa viongozi wa Soko la Sabasaba yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo kikuu cha Mabasi Dodoma. Alisema kuwa sifa mojawapo kubwa ya kiongozi bora ni yule mwenye kuzingatia katiba au muongozo wa ushirika ili aweze kutenda haki. “Kiongozi bora ni yule anayejua namna ya kutuimia katiba vizuri. Labda niulize hapa, Katiba ya ushirika ipo? Kama ipo, je ilitumika wakati ule matatizo yameanza kutokea? Jibu litakua hapana. Nipende kuwaambia kuwa, ukiijua vizuri katiba na miongozo, ni rahisi sana Kutenda haki kwasababu utatenda haki kwa kuzingatia taratibu na hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa” alisema Chacha. Aliongeza kuwa zipo sifa zaidi ya 25 za kiongozi bora ambapo kila kiongozi wa soko la sabasaba anapaswa ...

Bima ya Taifa ya Afya yatoa huduma kieletroniki

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Maboresho ya huduma ya Bima ya Afya yamefanywa kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia ambapo wananchi wanaweza kujisajili kupata huduma za bima kupitia simu zao na vifaa vya kieletroniki vyenye ‘Internet’. Hayo yalisemwa na Afisa Wanachama Mwandamizi, Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma, Bakary Hamdun katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati akiwasilisha sheria ya afya na kanuni zake. Alisema kuwa kila mwanachama anaetarajia kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) anaweza kujihudumia kupitia simu ya mkononi “Mwanachama yeyote awe mtumishi au mwananchi wa kawaida anaweza kujisajili kupitia simu yake ya mkononi. Na anaweza kufanya hivyo bila kuwa na changamoto ya aina yoyote kwasababu huduma hii ni rahisi pia inafanyika kwa muda mfupi” alisema Hamdun. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe aliipongeza serikali kwa hatua kubwa ya uboresha...

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ahimiza matumizi ya mfumo NeST

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko aeleza kuwa mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma NeST katika kufanya manunuzi ya vifaa vya serikali ni mfumo rafiki unaorahisisha manunuzi na kuweka taarifa hizo katika hali ya usalama. Aliyazungumza hayo katika Baraza la Madiwani la kawaida liliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa madiwani. Alisema kuwa mfumo wa manunuzi wa NeST upo tayari kwa mujibu wa sheria na umeonyesha matokeo chanya. “Niwajulishe ndugu wajumbe ya kwamba, mfumo huu hatuna namna ya kuepuka kuutumia kwasababu ndio mfumo ambao tunapaswa kuwa nao ili kufanikisha manunuzi ya vifaa mbalimbali vya serikali” alisema Dkt. Sagamiko. Aliongeza kuwa mfumo haumlazimishi mnunuzi kununua kila kitu kwa wakati mmoja. “Mfumo huu unahitaji ushirikiano ili uweze kufanya manunuzi yako. Kikubwa ni wewe kuhakikisha unafahamu unafanya manunuzi ya kiwango gani. Hakikisha unafahamu...

Shule mpya ya Msingi Chinyoyo ya kwanza kujengwa Kata ya Kilimani

Image
Na. Emmanuel Charles, KILIMANI Mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Chinyoyo, Kata ya Kilimani unaogharimu shilingi 147,000,000 ni shule ya kwanza kujengwa katani hapo na itaondoa adha ya wanafunzi ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo. Haya yalisemwa na Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘Media Tour’ kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia 2021-2025 katika kata hiyo. Alisema kuwa kwasababu kata yake ipo mjini, miundombinu ikiwemo ya elimu ilichelewa kufika na sasa serikali ya awamu ya sita inajenga shule ya msingi ili kuwakwamua watoto wanaotembea umbali mrefu. “Kwa miaka yote ya nyuma, kata hii haikuwahi kuwa na shule yeyote na wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata masomo katika kata za jirani. Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuona na kuamua kutenga eneo la kujenga Shule ya Msingi Chinyoyo kwa gharama ya shilingi 147,000,000 ambapo ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili...

Kata ya Kilimani mbioni kujenga Ofisi kila Mtaa

Image
Na. Emmanuel Charles, KILIMANI Kata ya Kilimani yatenga kiasi cha shilingi 150,000,000 kwaajili ya ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa katika mwaka wa fedha 2025/2026 lengo ikiwa ni kusogeza huduma karibu kwa wananchi. Haya yalisemwa na Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko alipokua akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘Media Tour’ kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia mwaka 2021-2025. Diwani Mwaluko alisema kuwa Kata ya kilimani ina maeneo ya kutosha kwaajili ya kujenga ofisi za mitaa na wapo wananchi wametoa maeneo yao zijengwe ofisi za mitaa. “Katika yetu tumeazimia kujenga ofisi kwa kila mtaa, lengo letu ni kusogeza huduma kwa jamii. Kuna baadhi ya huduma mwananchi sio lazima aende ofisi ya kata kumfuata afisa mtendaji wa mtaa, ofisi ya mtaa ikiwepo ni rahisi na hatapoteza muda kupata huduma yake. Yupo pia mwananchi mwenye mapenzi mema na maendeleo ya kata, amejitolea eneo lake ijengwe ofisi, tunamshukuru sana” alisema Diwani Mwaluko. Al...

Uwanja wa Michezo Kilimani utumike kuboresha Afya za wananchi

Image
Na. Nancy Kivuyo, KILIMANI Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko amesema suala la michezo katika kata yake linapewa kipaumbele kupitia hamasa ya ugawaji wa jezi na mipira pamoja na kuhimiza wananchi kupenda michezo ili kulinda afya zao. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kata ya Kilimani kuona shughuli za michezo zinavyofanyika. “Sisi Kata ya Kilimani tunahamasisha sana vijana wetu na watu mbalimbali kushiriki michezo kwasababu tunatambua michezo ni ajira lakini pia michezo ni afya. Bonanza na michezo mingi imekuwa ikifanyika katika uwanja wetu hali inayoonesha ni namna gani kata yetu ni kielelezo bora katika kuhamasisha michezo” alisema Diwani Mwaluko. Aliongeza kuwa vijana wa katani hapo wamekuwa wakipewa jezi na mipira ili kuongeza hamasa ya kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali. “Jambo hili nimeweza kulisimamia kwa vitendo, kunapokuwa na changamoto ya vifaa nimekuwa nikiwapatia jezi pamoja na mipira ili waendeleze vipaji vyao...

Utunzaji Mazingira Kata ya Kilimani kielelezo bora cha kuigwa

Image
Na. Nancy Kivuyo, KILIMANI Kata ya Kilimani yaendelea kuhimiza kwa vitendo utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti mbalimbali ikiwemo ya kivuli pamoja na matunda ili kuweka mazingira safi na ya kuvutia jambo linalowafanya wananchi wake kufurahia mandhari na kuwa na lishe bora. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo kujionea utunzaji wa mazingira unavyofanyika Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko alisema kuwa wanajitahidi kupanda miti ili kuweka mazingira katika hali nzuri inayovutia. “Sisi hapa Kilimani tuna program za kupanda miti kila mwaka. Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kila mwaka inatupatia miche ya miti kwaajili ya kupanda katika kata yetu” alisema Diwani Mwaluko. Aliongeza kuwa wanatoa elimu ya utunzaji mazingira kwa wananchi wa kata hiyo ili kuhakikisha wanakuwa vinara na mfano wa kuigwa katika Jiji la Dodoma. “Kwa ujumla kata yetu inafanya vema katika utunzaji wa mazingira. Kama mnavyojionea sehemu kubwa ni kijani, kila kaya un...

Bonanza la Michezo lahamasisha Wananchi kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jiji la Dodoma

Image
Na. Nancy Kivuyo, UHURU Halmashauri ya Jiji la Dodoma yafanya bonanza la michezo la hamasa kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura awamu ya pili kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha ili wapate haki ya kupiga kura ifikapo mwezi Oktoba, 2025. Hayo yalisemwa na Afisa Mwandikishaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro kabla ya ufunguzi wa bonanza la hamasa kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika uwanja wa michezo wa Mtekelezo katika Kata ya Uhuru, jijini Dodoma. Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura. “Tunategemea kufanya maboresho ya uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili watu wapate sifa ya kupiga kura hapo mwezi Oktoba, 2025. Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina vituo 105 na uandikishaji unategemewa kuanza mnamo tarehe 16 – 22 Mei, 2025” alisema Kimaro. Aliongeza kuwa vituo vitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi n...

Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya maendeleo katika kata zao iliyopelekea uboreshaji wa huduma za kijamii kwa wananchi. Aliyazungumza hayo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa madiwani wamesimamia vizuri miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kata zote 41. “Sisi Halmashauri ya Jiji la Dodoma tulipanga kukusanya na kutumia shilingi bilioni 143, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 62.3 ni za mapato ya ndani. Kupitia mapato ya ndani tumetenga vilevile, kwa kuzingatia taratibu zetu asilimia 70 itumike kwenda kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa muktadha huo, ni busara sana tuwe na taarifa miradi hiyo imetekelezwaje” alisema Prof. Mwamfupe. Aliongeza kuwa katika mkutano huo wa robo ya tatu walijikita katika...

Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

Image
Na. Aisha Ibrahim, MADUKANI MIKOPO ya asilimia 10 isiyo na riba kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa na tija kwa vikundi vya wajasiriamali na kuwasaidia kukuza kipato na kuinua uchumi katika Kata ya Madukani. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Madukani, Asha Hussein alipokuwa akiongelea mikopo hiyo na umuhimu wake kwa wananchi wa kata ya madukani. Alisema kuwa katika kata hiyo kuna jumla ya vikundi 14 vilivyopatiwa mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 273, ambapo wanawake ni vikundi saba na walipata kiasi cha shilingi milioni 160 na vijana ni vikundi saba waliopokea kiasi cha shilingi milioni 113. Alisema kuwa kutokana na mikopo hiyo wanufaika wameweza kuanzisha shughuli mbalimbali zinazowaingizia kipato na kuweza kujiinua kiuchumi. “Asilimia kubwa wana vikundi na wameanzisha shughuli zao za kuwaingizia kipato. Mfano; kuna baadhi yao wanauza nguo, kuna vijana wamefungua duka la madawa, ufundi wa simu na baadhi ya wakina mama wanaji...

Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

Image
Na. Aisha Ibrahim, MADUKANI Wananchi wa Kata ya Madukani, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha huduma za afya katika Zahanati ya Chikande na kuwahakikishia matibabu bora na karibu. Zahanati hiyo imeboresha huduma mbalimbali zikiwemo vipimo vya maabara kama malaria, wingi wa damu, virusi vya UKIMWI na afya ya mama na mtoto ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma stahiki na elimu kuhusu lishe bora karibu na makazi yao. Akizungumza kuhusu uboreshaji wa huduma za afya, Edina Rungwa ambae ni muuguzi katika zahanati hiyo alieleza kuwa wanatoa kipaumbele haswa kwenye huduma ya afya ya mama na mtoto kwa kutoa elimu kuhusu lishe bora na njia za kufuata ili kuepuka magonjwa katika kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua. “Kuhusu huduma ya afya ya mama na mtoto, zahanati hii tunajitahidi kwa ukubwa kuhakikisha mama wajawazito wanapata elimu ya kutosha kuhusu lishe bora na njia sahihi za kufuata ili kuepuka magonjwa mbalimbali. Hivyo, ku...

Wazazi wapongezwa kuchangia chakula S/M Uhuru

Image
Na. Aisha Ibrahim, UHURU Wazazi na walezi wamekuwa na mchango mkubwa katika kupanda kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kutokana na juhudi kubwa wanayoifanya ya kutoa michango na nafaka shuleni ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora na kuongeza kiwango cha umakini jambo linalopelekea kupanda kwa kiwango cha ufaulu. Kauli hiyo ilitolewa na Mwl. Sospeter Ramadhan, kutoka Shule ya Msingi Uhuru wakati akifafanua kuhusu utekelezaji wa ajenda ya lishe shuleni na umuhimu wake kwa waandishi wa habari waliotembelea shule yake kuona utekelezaji wa agenda ya lishe. Alisema kuwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuelewa, shule hiyo imekuwa na ushirikiano wa hali ya juu na wazazi na walezi kutoa michango ya fedha na nafaka ili watoto wapate chakula, pia mchango wa mawazo kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu bora. “Wazazi na walezi wamekuwa mstari wa mbele kujitolea michango ya fedha na hata mawazo ili kuhakikisha watoto hawa wanapata chakula wawapo shuleni. Jambo hili ni hama...

Wanufaika wa mkopo wasisitizwa kufanya marejesho kwa wakati

Image
Na. Aisha Ibrahim, UHURU Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Uhuru, Saada Zahaze, amewasisitiza wanufaika wa mkopo wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuzingatia miongozo na sheria za utoaji mkopo ikiwa ni kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kufanya marejesho kwa wakati uliopangiwa kupitia mfumo jumuishi. Mfumo huo jumuishi unatekelezwa kwa mujibu wa sheria kwa kutoa mikopo ya asilimia 10 katika Jiji la Dodoma kwa uwiano wa 4-4-2 yaani wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili. Akitoa ufafanuzi kuhusu mgawanyo wa mikopo hiyo alisema kuwa Kata ya Uhuru wamesajili vikundi 52, kati ya hivyo 18 ni vya wanawake, 17 ni vijana na 17 ni vya watu mchanganyiko ambapo katika vikundi hivyo, 18 tayari vimeshapata mkopo huo. Aliongeza kuwa, mikopo iliyotolewa kuanzia mwaka 2021 ni shilingi milioni 423 taslimu. Wanawake walipata mkopo wa shilingi milioni 203 na vijana shilingi 220 ambapo marajesho mpaka sasa ni milioni 277.7. ...

Miundombinu S/M Uhuru chachu ya elimu bora

Image
Na. Aisha Ibrahim, UHURU Diwani wa Kata ya Uhuru, Halfan Kabwe, ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa ya kukuza sekta ya elimu kwa maendeleo ya Jiji la Dodoma na taifa kwa ujumla. Alitoa shukrani hizo wakati akitoa ufafanuzi wa pesa alizopokea katika kata yake kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Uhuru, uliogharimu shilingi milioni 76. Akitoa ufafanuzi wa kina kuhusu ukamilifu wa vyumba vya madarasa alisema, “kupitia serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitupatia kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo tuliweza kujenga madarasa 10 na baadae akatuongeza kiasi cha shilingi milioni 26 zilizotuwezesha kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo” alisema Diwani Kabwe. Katika hatua nyingine, alimpongeza mbunge kwa kuwa na moyo wa kujitolea kufuatia ujenzi wa uzio katika shule hiyo kwalengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kupitia mazingira rafiki. “Nichukue fursa ...

UMISSETA kuandaa vijana katika sekta ya Michezo Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MASHINDANO ya Umoja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Tanzania (UMISSETA) ni takwa la kikanuni katika mitaala ya sekta ya elimu kwa lengo la kuwaandaa wanafunzi kuwa mahili katika sekta ya michezo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Peter Ititi alipokuwa akiongelea maandalizi ya michezo hiyo jijini Dodoma. UMISSETA ni michezo muhimu kwa wanafunzi na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ujumla. “Michezo imetajwa kwenye mitaala ya elimu kutokana na umuhimu wake. Michezo hiyo inalenga kuibua vipaji na kuviendelea kwa maslahi mapana ya taifa. Michezo pia ni ajira na tumekuwa tukishuhudia vijana wetu wakishiriki katika ligi mbalimbali” alisema Ititi. Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mwaka 2024 ilitoa wanafunzi 56 kati ya wanafunzi 120 waliochaguliwa kuunda timu ya UMISSETA ya Mkoa wa Dodoma iliyoshiriki kitaifa. “Mwaka huu matarajio yetu ni kuchukua makombe yote na tumejipanga kupele...