Posts

Showing posts from 2026

Prof. Mohamed ahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwapongeza wazazi

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makutupora watakiwa kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ya kielimu na maisha kwa ujumla. Hayo aliyasema Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Said Mohamed wakati wa Uzinduzi wa Upandaji Miti mwaka 2025/2026 uliofanyika katika Shule ya Sekondari Makutupora Jijini Dodoma. Alisema kuwa juhudi za wanafunzi katika masomo ni msingi muhimu wa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla. “Msingi mzuri wa watoto ni kupata elimu hivyo niwasihi wanafunzi muendelee kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia ndoto zenu, kwasababu hapa kuna viongozi wa baadae ambao wataweza kuongoza taifa letu, lakini pia muwe na nidhamu kwasababu nidhamu ndio hupelekea kufika mbali hususan katika masomo yenu” alisema Prof. Mohamed. Aidha aliwapongeza wazazi kwa juhudi wanazozifanya katika malezi ya watoto. “Nipende kuwapongeza wazazi kwa namna ambavyo mnaendelea kuwalea watoto katika misingi bora, lakini pia nisisitize u...

EID Mubarak toka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma

Image
 

Meya Chaula atoa Salam za Eid Dodoma

Image
 

Jiji la Dodoma kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Image
 

Wanawake watakiwa kulipa kodi na kukuza uchumi katika Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wanawake wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, hususan wafanyabiashara na wajasiriamali, wametakiwa kuendelea kulipa kodi na tozo kwa wakati ili kuchangia maendeleo ya jiji pamoja na kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla. Wito huo ulitolewa na Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Zuzu, Pilly Hassan, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2026. Alisema kuwa ulipaji wa kodi ni moja ya njia muhimu inayosaidia serikali   kupata mapato ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu ya masoko, barabara na huduma nyingine muhimu kwa wananchi. “Wanawake wengi wa Jiji la Dodoma tunajishughulisha na shughuli za biashara na ujasiriamali. Hivyo, tunapaswa kuwa mfano mzuri kwa kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu wa kulipa kodi na tozo za serikali kwa hiari na kwa wakati. Kupitia kodi hii itaweza kutusaidia mambo mbalimbali na ya muhimu kama vile kujeng...

Mstahiki Meya Chaula ashauri Baraza kutumia mkakati wa hoja kwa hoja

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula ameshauri Baraza la Madiwani kujenga utaratibu wa kuwasilisha hoja moja na kuiazimia hadi itakapokamilika ndio hoja nyingine ifanyiwe kazi. Aliyazungumza hayo kwa msisitizo katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri jijini Dodoma. Alisema kuwa mkakati huo wa hoja moja ‘Focus Strategy’ ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo yanayoonekana na yenye tija kwa wananchi wanaowaongoza. "Ili tuwe na ufanisi, niwaombe kwa unyenyekevu mkubwa sana tuchague jambo moja na kuliazimia hadi mwisho. Kwa mfano, kama baraza linaona kipaumbele ni ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule zote za msingi katika jiji letu, basi nguvu, fedha, na usimamizi wetu wote uelekezwe hapo. Tukimaliza na kujiridhisha kuwa kila shule ina vyoo bora, ndipo tunahamia hoja nyingine ya msingi na kuendelea na mtiririko huo" alisema Chaula. Alimalizia kwa kutoa rai kuwa umoja na maamu...

Shule ya Msingi Mazengo ipo moto

Image

Huduma ya Lishe kwa Shule za Dodoma

Image
 

Stadi za Maisha Kuwa mkombozi kwa wanafunzi wa Sekondari jijini Dodoma

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Elimu ya Stadi ya Maisha imetajwa kuwa ni chachu ya mabadiliko chanya kwa wanafunzi katika kuwajengea uwezo wa kujitambua na kukabiliana na changamoto za maisha katika shule za sekondari jijini Dodoma. Hayo aliyasema Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Daniel Mapilya wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa stadi za maisha katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma. Alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wawezeshaji wanapata uelewa wa kutosha juu ya namna bora ya kuwafikia wanafunzi na kuwajengea misingi imara ya maisha. “Tunapozungumzia stadi za maisha, tunalenga kumsaidia mwanafunzi kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi. Elimu hii itawawezesha vijana wetu kuepukana na vishawishi vinavyoweza kuathiri masomo na mustakabali wa maisha yao” alisema Mapilya. Aliongeza kwa kusema kuwa changamoto nyingi zimekuwa zikiwakumba watoto wa kike. ”…zikiwemo shinikizo la rika na mazingira yasiyo rafiki, hivyo elimu hiyo it...

Utatuzi mgogoro wa Mahomanyika watangazwa

Image
Na. Nancy Kivuyo , NZUGUNI Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeunda timu mbili ya wataalam wa upangaji na upimaji na timu ya uhakiki kwaajili ya kutatua mgogoro wa ardhi wa muda mrefu katika eneo la Mahomanyika. Timu hizo zimeundwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mahomanyika, Kata ya Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa timu hizo zitaanza kazi mara moja ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa wakati. “Eneo la Mahomanyika ni la serikali kwahiyo , naagiza lipangwe na kupimwa kwaajili ya kutatua mgogoro huu na kuwa kielelezo cha utatuzi wa migogoro mingine iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma. Timu hizi zinapaswa kufanya kazi ndani ya siku 60 na kukamilisha zoezi hili ili kila mmoja ajue amepata nini na anaenda wapi” alisema Dkt. Akwilapo. A liongeza kuwa wale wote waliohusika kwenye kadhia ya mgogoro huo wa ardhi watachukuliwa kwaajili ya maho...

Timu ya ‘sustainability’ ya Jiji la Dodoma yaanza semina ya siku saba

Image
  Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Mafunzo maalum kuhusu viwango vipya vya uhasibu ‘ General Requirements for Disclosure of Sustainability-related Financial Information na Climate-related Disclosures’ (IFRS S1 na IFRS S2) yameanza rasmi kutolewa kwa timu ya ‘sustainability’ ikiwa ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya uendelevu ‘sustainabilty and ESG’ yanayolenga kuwajengea uelewa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa taarifa za kifedha. Akizungumza wakati wa semina hiyo ya siku ya kwanza, Mratibu wa Mafunzo ya ‘sustainability’ katika Jiji la Dodoma, Akida Huddu alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu ya jumla ya uendelevu ‘sustainability and ESG’ kwa washiriki ili kuwawezesha kusimamia kwa ufanisi shughuli zote zinazohusiana na uendelevu pamoja na kupata taarifa zitakazosaidia kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Aliongeza kuwa uelewa wa viwango vipya vya uhasibu ni muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma, hususan katika mazingira yanayoh...

Wawezeshaji Stadi za Maisha watakiwa kuwa na nidhamu na uwajibikaji

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wawezeshaji wa Stadi za Maisha katika Shule za Sekondari Jiji la Dodoma wametakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika mazingira ya shule watakazopangiwa pamoja na kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi. Hayo yalisemwa na Mwezeshaji mafunzo y a Stadi za Maisha wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tuvacal Mjema, wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma. Alisema kuwa wawezeshaji wanapaswa kuwa mfano bora kwa wanafunzi kwa kuzingatia maadili, kuwajibika ipasavyo na kuonyesha weledi katika utekelezaji wa majukumu yao. “Ni muhimu kwa wawezeshaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu wanapokuwa shuleni. Tunapaswa kuishi yale tunayowafundisha wanafunzi ili waweze kutuamini na kufuata miongozo tunayowapatia kwasababu ninyi ndio taa yao   inayo waangazia” alisema Mjema. Lakini pia aliongezea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uwezo wa kitaaluma na kisaikolojia wawezesh...

Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa ujio wa Bandari Kavu Ihumwa

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula apongeza Mkakati wa Uendelezaji Bandari Kavu na kuahidi kujipanga kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanapata fursa ya kufanya biashara katika eneo hilo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla. Akizungumza katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye Bandari Kavu Ihumwa iliyokuwa na lengo la kujiridhisha na mkakati wa uendelezaji wa miundombinu hiyo, alisema kuwa uongozi wa jiji utakaa kikao na kutathmini namna ya kuandaa mazingira rafiki ya biashara ili kuwawezesha wajasiriamali wa ndani kushiriki kikamilifu katika shughuli za upokeaji, uhifadhi na usafirishaji wa mizigo. Alieleza kuwa pamoja na fursa za moja kwa moja zitakazotokana na shughuli za bandari hiyo, jiji pia linatarajia kuimarisha sekta ya usafirishaji, uhudumu na biashara ndogondogo hivyo kuongeza ajira na kipato kwa wananchi. Aidha, Mstahiki Meya Chaula aliongeza kuwa jiji litafanya utaratibu wa kufanya mazungumzo na Mam...

Shule ya Viziwi Dodoma yapokea msaada wa matendo ya huruma

Image
Na. Emanuel Charles, DODOMA Shule ya Viziwi Dodoma yakabidhiwa msaada wa mahitaji muhimu ya kijamii yenye thamani ya shilingi 2,00,000 ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyoandaliwa na Dodoma Jiji Day kwa lengo la kuhimiza upendo, ushirikiano na mshikamano. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma ambapo alikabidhi mchele, sukari, vifaa vya usafi na taulo za kike. Alisema kuwa ipo tha wabu ya utoaji na kuwajali watu wenye mahitaji maalum. “Kutoa siyo utajiri, ni moyo. Japokuwa tulichotoa kinaweza kuonekana kidogo kwa namna moja ama nyingine, lakini naamini kitaenda kuwasaidia watoto hawa, hasa katika kupata chakula shuleni na kuboresha mazingira yao ya kujifunzia” a lisema Alhaj Shekimweri . Aidha, aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mpango wake wa kuibadilisha shule hiyo kuwa ya mchanganyiko ili kuwaunganisha watoto wenye mahitaji maalumu ya usikivu na wale wasio na changamoto, ha...

Watumishi wa Kanda Namba Tatu watembelea Zahanati ya Soweto

Image
  Watumishi wa Kanda Namba Tatu watembelea Zahanati ya Soweto jijini Dodoma ambayo imekamilika na imeanza kufanya kazi. Zahanati hiyo inajumuisha jengo la huduma ya wagonjwa wa nje (OPD), chumba cha daktari, chumba cha kujifungulia wanawake, maabara na huduma ya mama, baba na mtoto. Uwepo wa zahanati hiyo ni kusogeza huduma karibu na wananchi ambao walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika Kituo cha Afya Zuzu au kwenda Hospitali ya Mkoa General  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026, wakati wa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Samia alizaliwa tarehe 27 Januari, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026, wakati wa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Samia alizaliwa tarehe 27 Januari, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kikao cha wazazi Shule ya Sekondari Mtumba katika uhamasishaji wa upatikanaji chakula shuleni

Image
Afisa Lishe wa Jiji la Dodoma, Frida Mollel alitoa wito kwa wazazi ya juu ya faida ya chakula shuleni na jinsi kinavyoweza kusaidia kuongeza ufaulu na kupunguza ukatili wa kijinsia kwa watoto huku akisema kuwa shule zinazotoa chakula watoto hufanya vizuri kwenye masomo na ufaulu wao upo juu.  

DKT. MWIGULU ASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI, DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 27, 2026 ameshiriki zoezi la upandaji miti, mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma. Zoezi hilo ni sehemu ya hatua ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira. Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu akiwa ameambatana na mwenza wake Mama Neema Mwigulu, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha namna alivyo kiongozi mwenye maono, mbunifu na anayejali maslahi mapana ya Taifa. “Shughuli hii imekuwa na utofauti kwa kusababisha miti ipandwe kila kona ya nchi, kwenye vitabu vyetu vitukufu, kupanda mti ni moja ya ibada kwasababu wanufaika wa miti ni wengi” Kadhalika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa kupanda miti. “Tunapokuwa na jambo la kukumbuka la aina hii, tufanye kitu ambacho kinaweka alam...

Kampeni ya upandaji miti Jiji la Dodoma yafanikiwa S/M Mbwanga

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Jiji la Dodoma limeendelea kutekeleza kampeni ya upandaji miti ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Zoezi hilo limefanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo shule, taasisi za umma, barabara na maeneo ya makazi. Akizungumza katika Shule ya Msingi Mbwanga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alisema kuwa zoezi la upandaji miti ni muendelezo wa kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la kijani na pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Aliwataka wanafunzi, walimu na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kupanda na kutunza miti ili kulinda mazingira na kuhakikisha ustawi wa vizazi vijavyo. Alisisitiza kuwa upandaji wa miti shuleni una mchango mkubwa katika kuelimisha watoto kuhusu umuhimu wa mazingira tangu wakiwa wadogo. "Tunapanda miti hii kwasababu ya kuungana na Mhe. Rais, Dkt. Samia kumpongeza katik...