Posts

Showing posts from December, 2025

Madiwani Jiji la Dodoma wasisitizwa kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapongezwa kwa kuaminiwa na wananchi na kutakiwa kufanya kazi kwa uwajibikaji, ushirikiano na weledi wa hali ya juu. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji. Jabir Shekimweri wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri. Alisema kuwa anawataka madiwani kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utendaji wao, kusikiliza kero za wananchi na kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo inalenga kuleta manufaa kwa jamii nzima. “Dodoma kama makao makuu ya nchi inahitaji uongozi thabiti, wa mfano na wenye matokeo. Ni wajibu wenu kuhakikisha jiji linaendelea kuwa kioo cha maendeleo kwa taifa hasa kwa kuibua miradi yenye tija kwa wananchi na kuwapa kipaumbele zaidi wananchi kwa kusikiliza kero zao” alisema Shekimweri. Aidha, alisisitiza umuhimu wa madiwani kushirikiana na watendaji wa halmashauri katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresh...

Kihaga: Fanyeni matangazo ili kuwafikia wananchi wa maeneo mbalimbali

Image
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa z a mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na h almashauri ili kuhakikisha wananchi wanaifahamu na kunufaika nayo. Hayo aliyasema Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, Angelista Kihaga, wakati akitoa semina kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri katika ukumbi wa Dodoma Sekondari. Alisema kuwa kuna baadhi ya wananchi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu uwepo wa mikopo hiyo, jambo linalochangia kutokuitumia ipasavyo. “Ni muhimu maafisa Maendeleo ya Jamii m katoa elimu kwa ukaribu zaidi. Wananchi wengi bado hawana uelewa kuwa mikopo hii ipo na haina riba. Tukitoa elimu ya kutosha tutasaidia makundi mbalimbali hasa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kunufaika na fursa hii” alisema Kihaga. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kutumia matangazo na vipindi mbalimbali kwenye vyomb...