Kamati za kudumu zatakiwa kuchangia kasi utekelezaji miradi ya maendeleo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma,
Alimwoni Chaula alimtangaza Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Maadili ya
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa ni Omary Omary, Diwani wa Kata ya Makole,
aliyepata kura zote tano kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Alisema kuwa kamati hiyo ina jumla ya wajumbe watano
ambao ni Omary Omary (Diwani Kata ya Makole), Swalihina Athuman (Diwani Kata ya
Viwandani), Charles Ngh’ambi (Diwani Kaya ya Mbalawala), Judith Mushi (Diwani
Viti Maalum) na Mwamrisho Kasule (Diwani Viti Maalum).
Mstahiki Meya aliwasoma wajumbe wa kamati nyingine
kuwa ni Robert Njama, Diwani wa Kata ya Mkonze na Flora Liacho, Diwani wa Viti
Maalum kuwa wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini. Wengine ni
Elis Kitendya, Diwani Kata ya Chihanga na Emmanuel Manyono, Diwani Kata ya
Kikombo kuwa wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Mtumba.
Kwa upande wa Bodi ya Ajira, alimtangaza Leonard Ndama,
Diwani wa Kata ya Nzuguni na Samson Mkopi, Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu kuwa
Mjumbe wa Bodi ya Vileo.
Akitangaza wajumbe wa Kamati ya Kugawa Ardhi,
aliwataja kuwa ni Mugendi Kerenge, Diwani wa Kata ya Mnadani na Asma Karama,
Diwani Viti Maalum. “Kamati ya ALAT Mkoa itakuwa na Edward Magawa Diwani wa
Kata ya Ihumwa na Leticia Sanga, Diwani Viti Maalum” alisema Chaula.
Nae, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba
aliwapongeza madiwani hao kwa kula kiapo na kwa kuchaguliwa katika kamati
mbalimbali za kudumu. “Mimi sina mengi ya kusema, nawapongeza kwa hatua hii.
Sasa mkafanye kazi kwa weledi na kwa ushirikiano mkubwa. Hizi kamati zinasaidia
kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maana hiyo ni
imani yangu kuwa mtashauri na kufuatilia pale inapotakikana” alipongeza Mamba.
MWISHO
Comments
Post a Comment