Madiwani Jiji la Dodoma wasisitizwa kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapongezwa kwa kuaminiwa na wananchi na kutakiwa kufanya kazi kwa uwajibikaji, ushirikiano na weledi wa hali ya juu. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji. Jabir Shekimweri wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri. Alisema kuwa anawataka madiwani kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utendaji wao, kusikiliza kero za wananchi na kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo inalenga kuleta manufaa kwa jamii nzima. “Dodoma kama makao makuu ya nchi inahitaji uongozi thabiti, wa mfano na wenye matokeo. Ni wajibu wenu kuhakikisha jiji linaendelea kuwa kioo cha maendeleo kwa taifa hasa kwa kuibua miradi yenye tija kwa wananchi na kuwapa kipaumbele zaidi wananchi kwa kusikiliza kero zao” alisema Shekimweri. Aidha, alisisitiza umuhimu wa madiwani kushirikiana na watendaji wa halmashauri katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresh...