Posts

Showing posts from February, 2024

Afisa Elimu Jiji la Dodoma anunua jina la Rais Samia kwa Laki 5

Image
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI MKUU wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Zainab Abdallah amefurahishwa na uwezo wa mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, Angel Elias alipoandika jina la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia mdomo wake na kununua jina hilo kwa shilingi 500,000. Mwanafunzi Angel Elias wa shule ya Msingi Hombolo Bwawani anayeandika kwa kutumia mdomo Furaha hiyo aliionesha katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichoambatana na utoaji tuzo za kitaaluma na kufanyika katika Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo Miyuji jijini hapa. “Mheshimiwa Mwenyekiti kabla ya yote, ninaomba kwa ridhaa yako kama hautajari, hilo neno lililoandikwa na mtoto wangu Angel ‘I am so excited’. Nitalinunua kwa shilingi 500,000. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ni ukweli kwamba hata wale wanafunzi wasio na mahitaji maalum tunaowafundisha hawajifunzi haraka kama huyu anavyo fanya” alisisitiza Mwl. Abdallah. Akiunga mkono tukio hilo, Mkuu wa Di...

Dodoma Sec kuongeza ufaulu kula mwaka

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA SHULE ya Sekondari Dodoma imekuwa ikiongeza ufaulu kila mwaka ikifikisha zaidi ya asilimia 97 ya ufaulu wa jumla kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wanafunzi, uongozi wa shule na serikali. Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwl. Francis Tumaini alipokuwa akielezea mwenendo wa shule yake katika ufaulu Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwl. Francis Tumaini alipokuwa akielezea mwenendo wa shule yake kwa wageni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliotembelea shule hiyo kwa lengo la kujifunza. Mwl. Tumaini alisema “kwa hali ya ufaulu, tunaongeza ufaulu kila mwaka. Kwa mwaka juzi ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu, lengo la serikali tufikie asilimia 50. Sisi tulikuwa na asilimia 65. Mwaka jana tukawa na asilimia 67 na mwaka huu tuna asilimia 68. Kwa ufaulu wa jumla kwa mwaka huu tuna asilimia zaidi ya 97. Kwa matokeo ya kidato cha Nne, tulikuwa na wanafunzi 308 tuliowasajili, ...

Tamisemi yajivumia taaluma Bunge Sekondari

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inajivunia maendeleo ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya wasichana Bunge kufuatia uwekezaji waliofanya na serikali shuleni hapo. Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwl. Ernest Hinju (katikati) akisisitiza jambo Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwl. Ernest Hinju alipoongoza ujumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kutembelea shule hiyo. Mwl. Hinju alisema “leo tulikuwa katika ziara ya kuwakaribisha na kuwatembeza wageni wetu kutoka Zanzibar ambao ni Mkurugenzi wa Elimu Maandalizi na Msingi na Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari pamoja na wasaidizi wao. Lengo ni kuja kujifunza kwa pande mbili jinsi wanavyoendesha elimu. Katika shule ya sekondari ya wasichana Bunge pamoja na mambo mengine tumeweza kuongea na wanafunzi na tumewakuta wanafunzi wanapendeza na wanahari ya kujifunza. Shule ya Sekondari ya wasichana Bunge imejen...

Msalato Sekondari wamshukuru Rais, Dkt. Samia ujenzi wa mabweni

Image
  Na. Dennis Gondwe, MSALATO SHULE ya Sekondari ya Wasichana Msalato inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu na kuwatengenezea mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia wanafunzi kwa lengo la kukuza viwango vya taaluma nchini. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Msalato, Mwl. Mwasiti Msokola alipokuwa akiongelea juhudi za serikali katika ujenzi wa miundombinu Shukrani hizo zilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Msalato, Mwl. Mwasiti Msokola alipokuwa akiongelea juhudi za serikali katika ujenzi wa miundombinu mbele ya ugeni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar uliotembelea shule hiyo. “ Tunamshukuru sana Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande wa elimu Shule ya Sekondari ya wasichana Msalato ametuona kwa sababu mwaka jana ametuletea fedha shilingi 428,000,000 kutuwezesha kujenga mabweni mawili ya maadalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano. Vilevi...

Wanafuzi Dodoma Sec watakiwa kusoma kwa bidii

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Dodoma wametakiwa kusoma kwa bidii na kutumia mfumo wa teknolojia ya ufundishaji mubashara kwa manufaa yao na vizazi vijavyo. Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fatma Ramadhani alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fatma Ramadhani alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma walipotembelea shule hiyo kwa ajili kujifunza juu ya mfumo wa ufundishaji mubashara unavyofanya kazi. Ramadhani alisema kuwa mfumo wa ufundishaji mubashara unawarahisishia walimu kufundisha kwa wepesi na wanafunzi kuelewa zaidi kwa sababu wanakuwa wakisikiliza na kuona. “Hivyo, ni jukumu lenu sasa wanafunzi kuweza kuhakikisha mnaitumia vizuri teknolojia hii si kwa maisha yenu pekee, bali kwa vizazi vijavyo. Kwasababu leo n...

Prof. Mwamfupe apongeza wadau wa elimu

Image
Na. John Masanja , MIYUJI Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe awapongeza wadau wa elimu kwa jitihada zao kwenye kukuza sekta ya elimu na kuchangia ufaulu wa wanafunzi. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe Pongezi hizo alizitoa kwa walimu, wazazi na wadau mbalimbali wa elimu kwa ushirikiano mzuri katika kukuza na kuinua sekta ya elimu ndani ya Jiji la Dodoma kwenye kikao cha wadau wa elimu na utoaji tuzo za kitaaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper jijini Dodoma. “Natambua sana kuna changamoto nyingi ambazo mnakutana nazo wakati wa utendaji kazi wenu lakini hamjawahi kutuangusha na haya mafanikio tunayoyaona sasa hivi katika elimu ni matunda ya uwekezaji wa pamoja” alisema Prof. Mwamfupe. Vilevile, alipendekeza kufanyika kwa vikao vya wadau wa elimu kuanzia ngazi za chini ambako watu wengi hufikiwa katika kutoa ushauri na kuona namna gani mawazo yao yatakuwa na manufaa katika kuleta mab...

Jiji la Dodoma kinara taaluma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeendelea kufanya vizuri katika taaluma kwa kufaulisha kwa asilimia 93.18 wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi mwaka 2023 kutokana na ushirikiano mzuri baina ya halmashauri na wadau wa sekta ya elimu. Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za elimu Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za elimu katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo jijini Dodoma. Mwl. Myalla alisema  “Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia Divisheni ya Elimu Awali na Msingi imeendelea kufanya vizuri katika taaluma kupitia matokeo ya mitihani mbalimbali ya kuhitimu elimu ya msingi na Mtihani wa Upimaji Darasa la Nne. Aidha, shule binafsi zimeendelea kufa...

BenPaul achangia Elimu Dola 300

  Na. John Masanja, MIYUJI Dola 300 za BenPaul kwenda kuunga mkono jitihada za elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Mfuko la Lishe. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bernard Paul alimaarufu BenPol amechangia kiasi cha dola 300 za kimarekani ikiwa ni ushiriki wake katika kuunga mkono jitihada za elimu ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Msanii BenPol alichangia kiasi hicho wakati wa kikao cha wadau wa Elimu na utoaji wa tuzo za kitaaluma kilichoandaliwa na Ofisi ya Halmashauri Jiji la Dodoma na kufanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper jijini Dodoma. “Nitoe wito na ombi kwa wazazi, walimu na wadau wote, tuendelee kuwaunga mkono vijana wetu kwenye elimu lakini pia tusiwakataze wanapopenda kufanya sanaa kwasababu vyote viwili vinalipa. Elimu inalipa na sanaa ni ajira” alihitimisha BenPol. Sanjari na hayo msanii BenPol aliteuliwa na wajumbe wa kikao hicho kuwa Balozi wa Mfuko wa Lishe ndani ya Halmashauri ya Jiji la D...

CCDO Sichona apongeza Azimio Mfuko wa Lishe Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKUU wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona amepongeza azimio la kuanzisha Mfuko wa Lishe wa halmashauri na kusema kuwa utakwenda kutatua changamoto za lishe. Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona akipongeza Azimio la Mfuko wa Lishe Pongezi hizo alizitoa alipokuwa akichangia katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo jijini hapa. Sichona alisema “nikupongeze na kikao chako kwa kuja na azimio la kuanzisha mfuko wa lishe wa halmashauri. Mfuko huo utaenda kutatua matatizo ya lishe na hata ukatili kwa watoto. Mimi kazi yangu kubwa ni kuongea na makundi maalum na huwa tunaongea na watoto wa kike na unakuta wengi wanadanganyika kutokana na kuwa na njaa shuleni. Watoto wa kike wanadanganywa na vijana waendesha bodadoba, wanadanganywa na makondakta wa daladala na mafundi wa gereji”. Akiongele...

Walimu Dodoma waaswa uzalendo

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA WALIMU wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kutanguliza uzalendo katika kazi zao ili kuwafundisha wanafunzi na kuwasaidia katika kujenga taifa lao. Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Christian Mauya alipochangia katika kikao cha wadau wa elimu Kauli hiyo ilitolewa na Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Christian Mauya alipochangia katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya St. Gasper jijini Dodoma. Mauya alisema “mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, mimi binafsi Ndugu zangu walimu nataka kuzungumzia kipengele cha pili, kipengele cha uzalendo. Sisi, walimu tunakubaliana kabisa tunakutana na changamoto nyingi sana, lakini nilikuwa naomba sana tuishi katika uzalendo wetu, uzalendo Tanzania. Hautakaa sehemu yeyote katika maisha yako yawe yamenyooka, uzalendo kwanza, hebu pigania Tazania yako”. Aliwakumbusha kuwa wapo makao makuu Dodoma kwa ajili ya ku...

Wadau wa Elimu kukutana ngazi ya chini

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewashauri wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa vikao hivyo viwe vinaanzia ngazi ya mitaa na kata ili wananchi wengi waweze kushiriki katika maendeleo ya sekta ya elimu. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akisisitiza jambo Ushauri huo aliutoa katika kikao cha wadau wa elimu Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo jijini Dodoma. Prof. Mwamfupe alisema “nilidhani kwamba siku kama leo tutambue kwamba changamoto zinazotukabili katika sekta ya elimu ni za kienyeji zaidi (localized) ziko zaidi katika maeneo husika. Kama ndivyo, ili vikao vya wadau wa elimu viwe endelevu tuvishushe kutoka ngazi hii hadi katika maeneo yetu tukawape watu uhuru wa kuongea ili siku kama ya leo watu waje na mifano ya vikao katika maeneo mengi zaidi. Mchakato huu ni muhimu kuanzia ngazi za chini zaidi am...

Maeneo ya Shule kupimwa Dodoma

Na. Dennis Gondwe, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ameagiza maeneo yote ya shule yapimwe na kupatiwa hati miliki ili kuepuka migogoro ya Ardhi inayotokana na uvamizi wa mipaka ya shule. Alhaj Shekimweri aliagiza maeneo ya shule yaliyopo sasa yapimwe na kutengenezewa hati miliki. Alisema kuwa utekelezaji huo utasaidia kuepusha migogoro ya Ardhi inayosababishwa na wananchi kuvamia maeneo ya shule. Aidha, alishauri ujenzi wa shule katikati ya mji ujielekeze kwenye majengo ya maghorofa ili katika eneo dogo litumike vizuri. “Nichukue nafasi hii kuwashukuru wenzetu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wameanza kutuunga mkono. Lakini pia mapato ya ndani ya halmashauri wameanza kufanya hivyo” alisema Alhaj Shekimweri. MWISHO

DC Shekimweri ampa Tano Mkurugenzi John Kayombo

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutoa kipaumbele katika maendeleo ya sekta ya elimu kwa kutoa fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu. Alhaj Shekimweri alisema “nitakuwa nimekosa uungwana nisipomshukuru hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Lipesi Kayombo. Tulikuwa na mkutano wa viongozi wakuu wa Wilaya ya Dodoma, Mstahiki Meya, Mbunge, Mkurugenzi wa Jiji na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mzee Mamba. Akiwa mgeni tukataka tushirikiane nae kwenye dira ya wilaya na tukataka tufahamu vipaumbele vyake kama kijana ambae anataka kuacha alama katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Nataka niwaambie leo hadharani, Kayombo alisema mimi napokea maelekezo na ushauri wenu wote mnaonipatia kama viongozi wangu, lakini la kwangu lililo moyoni mwangu ninatamani niache alama katika sekta ya elimu”. Alisema kuwa mkurugenzi huyo ametoa fedha nyingi katika ...

Mbunge Mavunde kuwekeza zaidi Sekta ya Elimu

Image
Na. Dennis Gondwe Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde ameahidi kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi wa Dodoma kusoma vizuri na kufikia malengo yao. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akitoa salamu za Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini katika mkutano wa wadau wa elimu Wilaya ya Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya St. Gasper jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema “Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini anasema kuwa nitaendelea kuwekeza zaidi kwenye elimu ili kuwasaidia watoto wa Dodoma kufikia malengo yao. Nitashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuinua na kuboresha elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma hasa katika miundombinu na mazingira rafiki ya kusomea”. Akiongelea mapinduzi katika teknolojia, alisema kuwa Dodoma inaelekea kupiga mapinduzi makubwa kwenye elimu. “Dunia inakwenda kwenye mapinduzi makubwa ya teknolojia, lazima tutumie maendeleo hayo katika kurahisisha ufundisha...

Matukio katika Picha Kikao cha Wadau wa Elimu Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Mbunge Mavunde kuwekeza zaidi sektan ya Elimu Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde ameahidi kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi wa Dodoma kusoma vizuri na kufikia malengo yao. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akitoa salamu za Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akitoa salamu za Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini katika mkutano wa wadau wa elimu Wilaya ya Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya St. Gasper jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema “Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini anasema kuwa nitaendelea kuwekeza zaidi kwenye elimu ili kuwasaidia watoto wa Dodoma kufikia malengo yao. Nitashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuinua na kuboresha elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma hasa katika miundombinu na mazingira rafiki ya kusomea”. Akiongelea mapinduzi katika teknolojia, alisema kuwa Dodoma inaelekea kupiga mapinduzi makubwa kwenye elimu. “Dunia in...

Matukio katika picha Wataalam wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya na Mkoa wa Dodoma wakitoa elimu katika Mkutano wa Maaskofu 600 wa TAG Tanzania Bara na Visiwani

Image
 

Madiwani wa Jiji la Dodoma katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Joseph Fungo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

Muonekano wa Madiwani katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma

Image
 

Prof. Davis mwamfupe katika mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

JIJI LA Dodoma linajali wanafunzi

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inawaonea huruma na kuwajali wanafunzi kwa watengenezea mazingira mazuri ya kujifunzia. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la Diwani wa Hazina, Samwel Mziba aliyetaka kujua ni lini halmashauri itakuwa na huruma kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru kwa kuifanyia ukarabati mkubwa ili iendane na hadhi ya jiji. Fungo alisema kuwa halmashauri inawaonea huruma wanafunzi na kuwajali kwa wajengea miundombinu ili waweze kusoma katika mazingira bora na salama. “Mheshimiwa mwenyekiti, tulimpeleka mhandisi kufanya makadirio ya gharama za kufanya ukarabati wa madarasa yaliyochakaa katika shule hiyo na mipaka kwa ajili ya ujenzi wa uzio. Hadi sasa mbao na ‘gypsum board’ zimeshafika shuleni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa shule hiyo” alisema Fungo. Aidha, Mstahiki Meya alisema kuwa kuna utayari ...

Mchakato kugawa mitaa kuanzia kwenye mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wametaarifiwa kuwa mchakato wa kugawa maeneo ya mitaa ambayo yanaonekana makubwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akijibu maswali ya papo kwa papo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Diwani wa Kata ya Iyumbu, Richard Sutuchi aliyetaka kujua utaratibu wa wa kugawa maeneo ya mitaa ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Fungo, alisema kuwa utaratibu wa kugawa mitaa unaanzia katika mitaa husika. “Mapendekezo yanatoka katika mitaa husika na utaratibu huo unapelekwa katika kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hadi halmashauri. Hivyo, mchakato uanzie kwenye mtaa” alisema Fungo. MWISHO