Posts

Showing posts from November, 2025

Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma kwa siku mbili likiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi, kupitia sera mpya zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na kutoka na mpango kazi mpya wa kutekeleza katika maeneo yao ya kazi.

Image
  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma kwa siku mbili likiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi, kupitia sera mpya zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na kutoka na mpango kazi mpya wa kutekeleza katika maeneo yao ya kazi.

Maafisa Mazingira Kanda Namba Sita waanza ziara ya kutoa elimu ya usafi wa mazingira sambamba na uhamasishaji wananchi kuchangia ada ya uzoaji taka.

Image
  Maafisa Mazingira Kanda Namba Sita waanza ziara ya kutoa elimu ya usafi wa mazingira sambamba na uhamasishaji wananchi kuchangia ada ya uzoaji taka. ‎ ‎Watumishi Kanda Namba Sita waanza mkakati wa kuhakikisha kata zinazounda kanda hiyo usafi wa mazingira unaimarika. ‎ ‎Akizungumza katika kikao kilichofanyika baina ya watumishi wa Kanda na viongozi wa Mtaa wa Mbwanga, Afisa Afya Kanda Namba Sita, Zainab Iddi alisema kuwa kuishi kwenye mazingira safi ni haki na wajibu wa kila mwananchi ‎ ‎Alisema kuwa usafi wa mazingira husaidia afya kuwa imara na salama. "Mtaa wa Mbwanga ni mojawapo wa mitaa ambayo tunataka wananchi waimarike katika suala la usafi wa mazingira. Katika suala la kiafya hairuhusiwi kutunza taka kwa mda mrefu au kuzichoma kwasababu kuna baadhi ya kemikali zinaweza kuleta madhara kwa binadamu" alisema Iddi ‎ ‎Aidha aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali. ‎ ‎Akisoma sheria za usafi wa mazingira Afisa Mazingir...

Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wakípima bango kwaajili ya kutathmini kodi ya bango kwa mujibu Sheria ndogo ya Ada na Ushuru wa Mabango na Matangazo ya Mwaka 2017.

Image
  Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wakípima bango kwaajili ya kutathmini kodi ya bango kwa mujibu Sheria ndogo ya Ada na Ushuru wa Mabango na Matangazo ya Mwaka 2017. Sambamba na hilo wanaendelea kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi wanaowatembelea ili kuhakikisha halmashauri inakusanya mapato stahiki

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo. Miradi iliyotembelewa ni Shule ya Msingi Mahungu na Kituo cha Afya Kizota.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Kanda Namba Mbili ambapo wakati wa ukaguzi walisisitiza ubora, thamani ya fedha na kasi ya utekelezaji kwa manufaa ya wananchi.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Kanda Namba Mbili ambapo wakati wa ukaguzi walisisitiza ubora, thamani ya fedha na kasi ya utekelezaji kwa manufaa ya wananchi.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Moja kukagua miradi ya maendeleo. Mradi uliotembelewa ni Shule ya Msingi Kaloleni wenye thamani ya shilingi 151,000,000 ambapo mradi huo upo katika utekelezaji

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Moja kukagua miradi ya maendeleo. Mradi uliotembelewa ni Shule ya Msingi Kaloleni wenye thamani ya shilingi 151,000,000 ambapo mradi huo upo katika utekelezaji

Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wamefanya ziara katika Migahawa mikubwa kwa lengo la kukagua Leseni za Biashara na pia ulipaji wa Kodi ya Huduma yaani Service Levy huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati

Image
  Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wamefanya ziara katika Migahawa mikubwa kwa lengo la kukagua Leseni za Biashara na pia ulipaji wa Kodi ya Huduma yaani Service Levy huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati

"Lakini kwenye uwezeshaji Wananchi kiuchumi tunapoliangalia kundi la Maendeleo ya Jamii,tunaona kuwa ni watu ambao wanatakiwa kuona mabadiliko ya kijamii kwa ujumla ya kiuchumi yanatokea kutokana na kazi zao".

Image
  "Lakini kwenye uwezeshaji Wananchi kiuchumi tunapoliangalia kundi la Maendeleo ya Jamii,tunaona kuwa ni watu ambao wanatakiwa kuona mabadiliko ya kijamii kwa ujumla ya kiuchumi yanatokea kutokana na kazi zao". Ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifungua kikao kazi cha siku 2 cha Maafisa Maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo. Miradi iliyotembelewa ni Hospitali ya Jiji la Dodoma yenye ujenzi wa Jengo la Upasuaji wenye thamani ya shilingi 337,889,130 zilizoingizwa tarehe 30 Agosti, 2025. Mradi huo umefikia asilimia 38. Mradi mwingine uliotembelewa ni pamoja na Jengo la Wodi ya Wanawake lenye thamani ya shilingi 252,426,200 na ujenzi wa jengo la kufulia lenye thamani ya shilingi 209,684,670.

Maadhimisho ya Wiki ya Lishe kupitia Dodoma FM jijini DOdoma

Image
  Maafisa Lishe Jiji la Dodoma wamefanya shughuli mbalimbali katika Wiki ya Lishe ikiwemo utoaji wa elimu ya lishe kupitia vyombo vya habari na kwa kutembelea vituo vya kulelea watoto kwaajili ya kupima afya. ‎ ‎Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa ambayo yalianza tarehe 17 Novemba 2025 yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 21 Novemba, 2025. ‎ ‎Akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kinachorushwa na Kituo cha Redio Dodoma Fm, Afisa Lishe Kituo cha Afya Makole, Frida Mollel alisema kuwa kila mmoja anatakiwa kuzingatia makundi sita ya chakula. "Katika maisha ya kawaida ya binadamu makundi sita ya chakula yanapatikana kiurahisi mfano mboga za majani, matunda, dagaa hata mafuta ya kupikia. Jambo la kuzingatia ni kwamba kuna baadhi ya vyakula havitakiwa kuliwa kwa pamoja kwasababu vinafanya kazi moja" alisema. ‎ ‎Mollel alisisitiza kwa mifano juu ya aina ya vyakula vinavyopaswa kuepukwa kuliwa kwa pamoja na vyenye kazi moja kwenye mwili wa binadanu. "Mfano viazi, ndiz...

Sungura kitoweo cha gharama nafuu

Image
‎Na. Mwandishi Wetu, HOMBOLO MAKULU ‎ ‎Maadhimisho ya Wiki ya Lishe katika Jiji la Dodoma yafanyika kupitia zoezi la ugawaji wa Sungura kwa kaya zenye kipato cha chini kwa lengo la kuzisaidia kupata makundi yote ya chakula bila kuathiriwa na kipato kidogo walichonacho. ‎ ‎Maadhimisho hayo yalianza tarehe 17 Novemba, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 21 Novemba, 2025. ‎ ‎Akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi hilo lililofanyika Kata ya Hombolo Makulu, Daktari wa Mifugo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dr. Innocent Kimweri alisema kuwa ufugaji wa Sungura hauna gharama ya kuwatunza na ni kitoweo kizuri kwaajili ya lishe bora. ‎ ‎Aliongeza kuwa, suala la lishe wanalihamasisha katika kaya zenye kipato cha chini ili kuwapa elimu ya kutosha kufahamu makundi muhimu ya chakula. "Suala la lishe ni mtambuka, pamoja na kwamba sisi ni maafisa mifugo, tunazingatia ulaji wa mlo kamili. Sungura ni rahisi kutunza kwasababu wanakula tu majani, mabaki ya vyakula na h...

Jiji la Dodoma laendesha kampeni ya elimu kwa wakulima

Image
  Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wakulima katika kuelekea msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026 ambapo wakulima wameelekezwa kulima mazao yanayostahimili mvua kidogo kama vile mtama, uwele na mihogo. Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo katika Kata ya Chihanga, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Agnes Woisso alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia ushauri wa kitaalam wanaopewa ili wavune mazao mengi. Alishauri kuwa wakulima wote wanapaswa kuachana na kilimo cha mazoea kwasababu kinawarudisha nyuma na kuwakosesha mavuno yenye tija. Alisema kuwa kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa mvua zitakuwa za wastani na chini ya wastani ambapo zitaanza kunyesha wiki mbili za kwanza za mwezi Disemba na zitaisha wiki ya tatu na nne za mwezi Aprili.

Jiji la Dodoma laendesha zoezi la Upimaji Afya na Lishe Tehillah Daycare Centre

Image
  Mtaalamu wa Lishe kutoka Kituo cha Afya Makole, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Frida Mollel ametembelea kituo cha kulelea watoto chini ya miaka mitano cha Tehillah Daycare Centre na kufanya vipimo vya hali ya Afya na Lishe kwa watoto hao ili kubaini maendeleo ya lishe na kutoa ushauri stahiki kwa walezi.

Mazoezi ni msingi imara kwa Afya bora

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuzingatia afya zao kwa kufanya mazoezi na kufuata kanuni bora za kiafya, ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameendelea kuongezeka katika jamii. Alitoa wito huo mara baada ya kukamilika kwa Mbio za Kuhamasisha Kupima Afya, mbio hizo zilianzia katika O fisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na kuhitimishwa katika Bustani ya Mapumziko ya Nyerere Square, amba p o kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Upimaji Magonjwa y asiyoambukiza kilifanyika. A lisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha anajilinda dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. “Nipende kuwasisitiza tu kuwa afya ndio msingi imara na mtaji wa masikini ni nguvu yake mwenyewe . H ivyo , tupambane na tuweke afya zetu vizuri kwa kufanya mazoezi na kupima afya zetu mara kwa mara” alisema Alhaj Shekimweri. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma , Dkt. Pima Sebastian alisema kuwa...

DC Shekimweri aongoza mazoezi ya Kilomita 5

Image
    Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri apongeza Umoja wa Klabu za Mbio za Pole kwa kujitokeza na kuhamasisha upimaji wa afya na matibabu bure kwa magonjwa yasiyoambukiza.   Mbio hizo zilianzia katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na kuhitimishwa katika bustani ya mapumziko Nyerere Square ambapo maadhimisho hayo ya Wiki ya Upimaji Magonjwa yasiyoambukiza yalitamatika. Alisema kuwa anawashukuru waandaji wa kliniki hiyo kwa kutoa huduma bora. “Siku ya kwanza walipokea wananchi 450 waliojitokeza kupata vipimo na matibabu, jana walihudumia wananchi zaidi ya 300. Kwahiyo, kwa ujumla wamehudumia jumla ya wananchi 1,500. Nimefurahi sana kusikia mwitikio ni mkubwa pia ni imani yetu kuwa baada ya zoezi hili kutamatika, tutafanya upembuzi ili kuona namna tunaweza kufanya zoezi hili kuwa endelevu tukihusishanisha na mazoezi’’ alisema Alhaj Shekimweri. Pia aliwashukuru wananchi wote waliofuatilia Hotuba ya Rais Dkt. Samia waka...

Lishe bora yahamasishwa Kliniki ya Magonjwa Yasiyoambukiza Nyerere Square

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mamia ya wananchi wamejitokeza kupima afya zao katika kliniki maalum ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuongeza uelewa kuhusu uchunguzi wa mapema, lishe bora na kuzuia magonjwa yanayoendelea kuongezeka nchini. Taarifa hiyo ilitolewa na Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii, Dr. Peter Daud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika bustani ya mapumziko Nyerere Square ambapo maadhimisho ya wiki ya Upimaji Magonjwa yasiyoambukiza yakitamatika. Dr. Daud alisema kuwa mwamko mkubwa ulioonekana ni ishara kuwa elimu ya lishe na uchunguzi wa mapema inawafikia wananchi kwa ufanisi. “Sehemu kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza inahusiana na lishe. Tunawahimiza wananchi kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi, kula kwa uwiano sahihi na kufanya mazoezi. Hii ni kinga muhimu sana” alisema Dr. Daud. Aliongeza kwa kutoa wito kuwa wananchi waache tabia bwete kwa kuhakikisha wanafanya mazoezi, kutembea umbali mdogo kwaajili ya kuweka mwili na misuli t...

Chupa 41 za damu zakusanywa Nyerere Square, wananchi wahimizwa kuendelea kuchangia

Image
Na. Nancy Rogers, DODOMA Jumla ya chupa 41 za damu zilikusanywa kutoka kwa wachangiaji waliojitokeza kwa hiari katika siku ya kwanza ya Kliniki ya Upimaji Magonjwa y asiyoambukiza inayoendelea katika bustani ya mapumziko Nyerere Square jijin Dodoma . Uchangiaji huo wa damu umehimizwa kufanyika kila wakati kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu kwa dharura hospitalini, huku wakazi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo muhimu la kuokoa maisha. Hayo yalielezwa na Mkuu wa Timu za Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Leah Kitundya ambae alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu mara kwa mara, kwasababu mahitaji ya damu katika hospitali yanaongezeka kila siku. “Tunaendelea kuhimiza jamii kuchangia damu kwa hiari, kwa kuwa damu ni uhai na inaweza kuokoa maisha ya mama wajawazito, wagonjwa wa upasuaji na wa ajali” alisema. Mmoja wa wachangiaji damu na Mkazi wa Miyuji, Rehema J...

Changia Damu kuokoa maisha

Image
  ‎Na. Mwandishi Wetu, DODOMA ‎ ‎Wananchi wahimizwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wale wanaopata dharura ya kuhitaji huduma ya kuongezewa damu. ‎ ‎Hamasa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Timu za Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati, Dr. Leah Kitundya katika kliniki ya upimaji wa bure wa magonjwa yasiyoambukiza inayoendelea katika bustani ya mapumziko Nyerere Square jijini Dodoma. ‎ ‎Alisema kuwa kila mwananchi anawajibu wa kuchangia damu kwasababu inasaidia wakati wa uhitaji. "Wananchi mliopo hapa Nyerere Square tunawaomba na kuwakumbusha kuchangia damu kwasababu itatusaidia sote wakati wa uhitaji. Damu yako inaweza kumsaidia mtu ambae hukutegemea ingemfikia. Changia kuboresha afya za wengine" alisema Dr. Kitundya. ‎ ‎Aliwaita wananchi kuchangia damu huku akiwakumbusha kujitokeza kwa wingi kujitolea kwasababu zinapotokea ajali ama dharura za kuhitaji damu kwaajili ya kuokoa maisha wapo pia ndugu na jamaa wa karibu wanaweza kukumbwa na kadhia hiyo. ‎ ‎"Ndugu z...