Maadhimisho ya Wiki ya Lishe kupitia Dodoma FM jijini DOdoma
Maafisa Lishe Jiji la Dodoma wamefanya shughuli mbalimbali katika Wiki ya Lishe ikiwemo utoaji wa elimu ya lishe kupitia vyombo vya habari na kwa kutembelea vituo vya kulelea watoto kwaajili ya kupima afya.
Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa ambayo
yalianza tarehe 17 Novemba 2025 yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 21
Novemba, 2025.
Akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live
kinachorushwa na Kituo cha Redio Dodoma Fm, Afisa Lishe Kituo cha Afya Makole,
Frida Mollel alisema kuwa kila mmoja anatakiwa kuzingatia makundi sita ya
chakula. "Katika maisha ya kawaida ya binadamu makundi sita ya chakula
yanapatikana kiurahisi mfano mboga za majani, matunda, dagaa hata mafuta ya
kupikia. Jambo la kuzingatia ni kwamba kuna baadhi ya vyakula havitakiwa kuliwa
kwa pamoja kwasababu vinafanya kazi moja" alisema.
Mollel alisisitiza kwa mifano juu ya aina ya
vyakula vinavyopaswa kuepukwa kuliwa kwa pamoja na vyenye kazi moja kwenye
mwili wa binadanu. "Mfano viazi, ndizi, wali na ugali ni vyakula ambavyo
ni aina ya wanga na vinafanya kazi moja ya kuupa mwili nguvu hivyo mtu
anashauriwa kuchagua kimojawapo" alisisitiza
Alimalizia kwa kuelezea namna mtoto mchanga
anapaswa kupatiwa lishe bora kutoka kwa Mama. "Pia mtoto mchanga anatakiwa
kunyonya kwa muda wa miezi sita bila kupewa chakula kingine baada ya hapo
atatumia uji wenye virutubisho vya lishe ili kumjenga kiafya" alimalizia
Mollel.
MWISHO
Comments
Post a Comment