Jiji la Dodoma laendesha kampeni ya elimu kwa wakulima

 

Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wakulima katika kuelekea msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026 ambapo wakulima wameelekezwa kulima mazao yanayostahimili mvua kidogo kama vile mtama, uwele na mihogo.






Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo katika Kata ya Chihanga, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Agnes Woisso alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia ushauri wa kitaalam wanaopewa ili wavune mazao mengi.

Alishauri kuwa wakulima wote wanapaswa kuachana na kilimo cha mazoea kwasababu kinawarudisha nyuma na kuwakosesha mavuno yenye tija. Alisema kuwa kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa mvua zitakuwa za wastani na chini ya wastani ambapo zitaanza kunyesha wiki mbili za kwanza za mwezi Disemba na zitaisha wiki ya tatu na nne za mwezi Aprili.




Comments

Popular Posts

Agenda ya Lishe yaongeza Ari ya usomaji S/M Dodoma Makulu

Miaka minne ya Dkt. Samia, Kizota yanufaika mikopo ya asilimia 10

Halmashauri ya Jiji la Dodoma Kuhudumia Majimbo Mawili ya Uchaguzi