Diwani Gombo kuongoza Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Diwani wa Kata ya Ipagala, Gombo Dotto apata ushindi mnono nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Mipango Miji na Mazingira kwa kuibuka na kura 20 akiwaacha kwa mbali wagombea wawili. Akitangaza matokeo ya nafasi ya Mwenyekiti, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, alisema kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Mipango Miji na Mazingira ni Mheshimiwa Gombo Dotto. “Kamati ya kudumu ya Mipango Miji ilikuwa na wagombea watatu wa nafasi ya mwenyekiti. Mheshimiwa Leonard Ndama, Diwani wa Kata ya Nzuguni alipata kura moja, Mheshimiwa Theobalt Mahina, Diwani wa Kata ya Ntyuka alipata kura moja na Mheshimiwa Gombo Dotto alipata kura 20” alitangaza Mstahiki Meya Chaula. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliwapongeza viongozi wote waliochaguliwa katika nafasi za kamati za kudumu na kuwaasa kutumia nafasi hizo kuhakikisha wanasimami...

Comments
Post a Comment