Posts
Showing posts from September, 2024
SEMINA YA MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA AKIWAAPISHA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
SEMINA YA MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA NA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa kutoa elimu kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha Mbwa
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Asteria Frank, DODOMA Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani yanalenga kuelimisha jamii juu ya kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa pamoja na kutowa chanjo kwa paka na mbwa ili kuwakinga na ugonjwa huo. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ofisi za kituo za huduma za mifugo kanda ya kati Dodoma mjini ambapo wamefahamisha kuhusu kichaa cha Mbwa Pamoja na kutoa chanjo, dawa ya kuzuia viroboto na dawa za Minyoo kwa Mbwa na Paka. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hussein Nyenye katika maadhimishi ya siku ya kichaa cha mbwa duniani yaliyofanyika katika Kituo cha Huduma za Mifugo Kanda ya Kati, kilichopo jijini Dodoma. Nyenye alisema kuwa ni muhimu kwa wafugaji wa mbwa na paka kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuweza kuwapatia mbwa na paka chanjo kwa wakati sahihi kuzuia magojwa mbalimbali kwa wanyama hao na wafugaji wenyewe. Alisema kuwa shughuli ya kudhibiti kichaa cha mbwa haiwezakani kufanyika na watu wa mifugo...
Uboreshaji daftari la wapiga kura chini ya dakika 5
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufika katika vituo vya kuandikishia wapiga kura ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura mapema kwa sababu zoezi linafanyika chini ya dakika tano. Faraja Mbise baada ya kujiandikisha Ushauri huo ulitolewa na Faraja Mbise, mkazi wa Mtaa wa Chang’ombe, Kata ya Ihumwa, Halmashauri ya Jiji la Dodoma alipofanya mahojiano maalum baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Msuguri. Mbise alisema “wito wangu kwa wananchi ambao bado hawajafika katika vituo vyao vya kujiandikisha, wafike mapema kwa sababu zaidi ya siku ya leo zitakuwa zimebaki siku mbili tu. Wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa sababu zoezi linaenda vizuri sana na kwa haraka. Ni zoezi ambalo halichukui hata zaidi ya dakika tano”. Aidha, akiongelea utendaji wa maafisa uandikishaji, alisema kuwa wanafanya kazi vizuri. “Maafisa uandikish...
Vijana wahamasishwa kujiandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga kura
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MAKULU VIJANA wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili waweze kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Magdalena Samwel, mkazi wa Mtaa wa Mwangaza Kata ya Dodoma Makulu Ushauri huo ulitolewa na Magdalena Samwel, mkazi wa Mtaa wa Mwangaza Kata ya Dodoma Makulu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma muda mfupi baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo kilichopo Shule ya Sekondari Kisasa leo asubuhi. Samwel alisema “leo nimewahi hapa kituoni kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili niwahi kazini. Nimejiandikisha nikiwa mtu wa pili, ulinitangulia wewe ndugu mwandishi. Nimekuja ili nipate uhalali kwa kushiriki uchanguzi mkuu ujao kama mtanzania”. Aidha, alitoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. “Napenda kuwashauri vijana wajitokeze kwa w...
RC Senyamule afafanua uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Asteria Frank, DODOMA Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa ufafanuzi wa dhana mbalimbali kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unaoendelea katika Wilaya ya Dodoma, Chamwino, Bahi na Kongwa. Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule Kauli hiyo aliitoa alipokuwa mbele ya vyombo vya habari leo katika ukumbi wa mkutano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhusu juhudi za kuelimisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuhusu mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unaoendelea katika Wilaya ya Dodoma, Chamwino, Bahi, na Kongwa. Alisema “napenda kutoa ufafanuzi kuhusu dhana mbalimbali zilizojengeka miongoni mwa wananchi. Kuna taarifa zisizo sahihi zinazozungumziwa kuhusu gharama za uandikishaji, muda wa vitambulisho vya kupiga kura na mchakato wa uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura”. Aliongeza kuwa uboreshaji taarifa za wapiga kura ni bure, wananchi hawatakiwi kulipa pesa yeyote katika mchakato huo. Dhana ya kwamba kuna gharama zinazohusi...
Maekelezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 yatolewa Jiji la Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Asteris Frank, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko ametoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 kwa umma. Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa umma Akizungumza mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake leo tarehe 26 Septemba, 2024 kuhusu maekelezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 alisema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi amepewa mamlaka ya kutoa maelekezo kuhusu uchaguzi. “Maelekezo haya yanatolewa siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi, kwa lengo la kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa na kwamba wapiga kura Pamoja na wagombea wanapata taarifa zote zinazohitajika kwa wakati. Maelekezo haya yanafafanua hatua zitakazo ongoza mchakato wa uchaguzi, kuanzia uandikishaji wa wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea, uteuzi wa wagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi. Maelekezo haya yanalenga kuto...
Msimamizi wa Uchaguzi Jiji la Dodoma atoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba, 2024 ili kuchagua viongozi bora. Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 akiwa amezungukwa na timu ya waratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Ushauri huo ulitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 26 Septemba, 2024. Dkt. Sagamiko alisema “niwahamasishe wananchi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kujitoleza kwa wingi siku ya uchaguzi ambayo ni jumatano ya tarehe 27 Novemba, 2024 ili kuchagua viongozi bora watakaoongoza”. Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa wananchi wenye sifa za kushiriki wanatakiwa kushiriki. “Ninatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki ki...
Ubalozi wa Sweden kuendelea kushirikiana na Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Macias ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu kutoka ofisi hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. Katika mazungumzo hayo, Balozi Macias alisema wanashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Mpango wa kunusuru Kaya Masikini nchini (TASAF), elimu na katika Taasisi za kidemokrasia. Balozi Macias aliongeza kwa kusema kuwa watashirikiana katika kutoa ujuzi na teknolojia katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aliualika Ubalozi wa Sweden kuja kuwekeza makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Aliwaeleza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo masuala ya kilimo cha zabibu kwasababu ndio kipaumbele cha Mkoa wa Dodoma. Ziara hiyo iliambatana na zoezi la kutembelea Mji wa Serikali Mtumba, maeneo yaliyotengwa...
DC Shekimweri ahamasisha wananchi kushiriki uboreshaji daftari la wapiga kura
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Alhaj Shekimweri, aliyasema hayo katika Bonanza la wadau lililofanyika katika viwanja vya Sheli Complex iliyopo Mtaa wa Mailimbili, Kata ya Chamwino jijini Dodoma. Akizungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali Alhaj Shekimweri alisema “Kwa Jiji la Dodoma ukizingatia takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na wakazi karibu Laki tano kasoro, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 lilikuwa na wakazi 798,000 na ukizingatia ongezeko karibu la 3% kwa mwaka tunakaribia kufikia Milioni Moja kasoro. Takwimu zinaonesha idadi ya wapiga kura kwenye wilaya yetu ni 502,000”. Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa utoaji wa elimu kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utakuwa ni endelev...
DC Dodoma akagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Asteria Frank, DODOMA Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kishirikiana na Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) inatekeleza mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato. Kiwanja hiko cha Ndege cha kimataifa Cha Msalato kinajegwa kwa awamu kwa kufuata mpango mkakati wa utekelezaji wa mradi huo ukiwa na lengo la kurahisisha usafiri kati ya Tanzania na nchi jirani pamoja na uboreshaji wa usafiri wa ndani. Mkuu wa Wilaya wa Jiji la Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri alifanya ziara katika mradi huo ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja na alisema kuwa Suma JKT wanadhamana na ujenzi huo kwaajili ya ulinzi kwa kudhibiti matendo ya wizi unaofanyika. Alisema kuwa amefarijika sana kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi na juhudi kwenye ‘package one’ ni asilimia 75 na jitihata ya ‘package’ ya pili ni asilimia 43.6. "Sehemu ya taarifa kulikiwa na changamoto na moja wapo ni udokozi wa kwenye mradi na tumepata nafasi ya kufanya mjadala mpana na kwa ...
Jiji la Dodoma latoa Kilo 790 za sukari kwa shule 150
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa kilo 790 za sukari kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha kupata uhakika wa chai wanapokuwa shuleni ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inatumika katika taasisi mbalimbali. Kilo hizo zilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago wakati wa hafla ya ugawaji mitungi ya gesi na majiko 1,000 kwa shule, zahanati, vituo vya afya, vituo vya watoto yatima na mama na baba lishe tukio lililofanyika katika uwanja wa Nyerere square jijini Dodoma. Naibu Meya Chibago alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imechangia kilo 790 za sukari kwa shule za msingi na sekondari 150. Shule za msingi zilizopewa sukari hiyo ni 104 na shule za sekondari ni 46 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, aliongeza. Akiongelea zoezi la utoaji wa majiko na mitungi...
Wananchi wa Dodoma watakiwa kutumia nishati safi kupikia
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Valeria Adam, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aeleza faida za nishati safi kwa matumizi ya kupikia na kuwataka wananchi wa Dodoma kuacha kutumia nishati chafu kwa matumizi ya nyumbani na sehemu za kazi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aeleza faida za nishati safi Aliyasema hayo katika halfa ya ugawaji wa mitungi ya gesi na majiko 1,000 kwa shule, zahanati, vituo vya afya, vituo vya makao ya watoto na mama na baba lishe huku akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia, kuboresha afya za watumiaji na kulinda mazingira. Alisema kuwa nishati safi ina faida kubwa kwa watumiaji na mazingira hatua hiyo inalenga kuimarisha matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia, kuboresha afya za watumiaji, na kulinda mazingira. “Faida za nishati safi ni pamoja na matumizi bila kuathiri afya za watumiaji. Pia, itapelekea hewa ya oksijeni kuongezeka na miti kuendelea kukua, na hivyo, Dodoma itaendelea kuwa salam...
Mbunge Mavunde awakumbuka mama lishe Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde, ameahidi kuwatengenezea mazingira mazuri na rafiki ya kufanyia biashara mama lishe waliopo pembezoni mwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Mavunde alizungumza hayo mara baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa jengo la kupumzikia wananchi lilipo nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Aidha, Mavunde aliahidi kuwaboreshea na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kufanya biashara ya chakula na kukarabati miundombinu kama vile kuwatengenezea meza na viti za kufanyia biashara pamoja na kuweka maeneo nadhifu. Mavunde alisema “sambamba na hilo nafahamu ya kwamba, asilimia kubwa ya wanaokaa pale hawavimudu vyakula ambavyo watu wengi hapa tunavimudu vyakula vya mahotelini...”. Hata hivyo, Mavunde aligusia wananchi wa kipato cha chini wasioweza kumudu gharama kubwa za kununua chakula kwa ajili ya wagonjwa wao hivyo kuahidi kuwasaidia mama lishe kuboresha maeneo yao ya kufanyia kazi kuwa safi na sal...
Mkuu wa Wilaya Apongeza Ujenzi wa Madarasa Mtumba
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Valeria Adam, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ametembelea miradi ya serikali iliyopo Kata ya Mtumba na kusisitiza elimu kuwa agenda ya kudumu. Akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtumba alitoa wito kwa jamii kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kitaaluma, ufundishaji na ujifunzaji ili kuhakikisha majengo mazuri yaliyojengwa yanaakisi ubora wa elimu. Alisema kuwa ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na yenye tija, na kwamba walimu wana nafasi kubwa katika kufanikisha hilo. “Nisisitize agenda hii ya elimu iwe ni ya kudumu, fuatilieni kwa karibu maendeleo ya kitaaluma, ufundishaji ili kusudi majengo haya mazuri tuliyojengewa yaakisi katika ubora wa elimu” alisema Alhaj Shekimweri. Aidha, aliwapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka waendelee kuwafundisha watoto kwa upendo na kwa kuwajali ili kuwasaidia watoto kujifunza vizuri bila kuhofia chochote. “Walimu muwafundishe watoto kwa upendo, muwaele...
Mtumba yapata madarasa mapya kwa kidato cha Tano na Sita
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Valeria Adam, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu bora na kufuatiliwa kwa karibu ili wafaulu. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akitoa wito kwa Jumuiya ya Shule ya Sekondari Mtumba Aliyazungumza hayo katika ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Mtumba jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisisitiza umuhimu wa kuwapeleka watoto shule na kusimamia maendeleo yao ili kuwawezesha kufaulu kwa kiwango cha juu. “Tupeleke watoto wetu shule na sio tu kuwapeleka shule, tuwasimamie pia wafaulu. Kama dhamira ni kufanya watoto wetu wasome hapahapa, ni vema waje na watoto wa nje wajichanganye na watoto wetu ili kufundishana tamaduni mbalimbali na tutajenga watanzania wenye umoja” alisema Alhaj Shekimweri. Mkuu wa Wilaya alisisitiza pia umuhimu wa kuweka uzio kwenye shule hiyo ...