Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa kutoa elimu kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha Mbwa
Na. Asteria Frank, DODOMA
Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa
duniani yanalenga kuelimisha jamii juu ya kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa pamoja
na kutowa chanjo kwa paka na mbwa ili kuwakinga na ugonjwa huo.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika
ofisi za kituo za huduma za mifugo kanda ya kati Dodoma mjini ambapo
wamefahamisha kuhusu kichaa cha Mbwa Pamoja na kutoa chanjo, dawa ya kuzuia
viroboto na dawa za Minyoo kwa Mbwa na Paka.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hussein Nyenye katika maadhimishi ya siku ya
kichaa cha mbwa duniani yaliyofanyika katika Kituo cha Huduma za Mifugo Kanda
ya Kati, kilichopo jijini Dodoma.
Nyenye alisema kuwa ni muhimu kwa
wafugaji wa mbwa na paka kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuweza
kuwapatia mbwa na paka chanjo kwa wakati sahihi kuzuia magojwa mbalimbali kwa wanyama
hao na wafugaji wenyewe.
Alisema kuwa shughuli ya kudhibiti
kichaa cha mbwa haiwezakani kufanyika na watu wa mifugo peke yake bali kwa
ushiriki wa sekta nyingine kama Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Sekta ya Afya na
Sekta ya Elimu na ndio maana maafisa wanatoa elimu hii hata shuleni kwa watoto
wetu na jamii kwa ujumla ili waweze kujikinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
“Lakini wakati huohuo, tunatoa elimu
kwa wafugaji juu ya ufugaji bora wa mbwa. Mbwa kwa kawaida anatakiwa afugwe
ndani na apewe tiba ikiwa ni pamoja na chanjo ya kichaa cha mbwa, dawa za
minyoo na dawa za kuzuia wadudu kama viroboto, kupe na kadhalika ambao wanaleta
usumbufu kwa wanyama na sio mbwa kudhurura mitaani” alisema Nyenye.
Nae Kaimu Afisa Mfawidhi, Kituo cha Huduma
za Mifugo Kanda ya Kati, Dkt. Dioniz Ibrahim alisema kuwa maadhimisho ya siku
ya kichaa cha mbwa yanafanyika tarehe 28 septemba, duniani pamoja na kuongeza
uwelewa juu ya udhibiti wa ugojwa wa kichaa cha mbwa.
Dkt. Dioniz Ibrahim ambae pia ni Daktari
wa Mifugo Kanda ya Kati alisema kuwa kituo hicho kipo chini ya Wizara ya Mifugo
na Uvuvi kikihudumia mikoa miwili ya Dodoma na Singida na majukumu yake makuu
ni udhibiti wa magonjwa ya wanayama ikiwemo kichaa cha mbwa.
“Katika maadhimisho haya tunafanya utoaji
wa chanjo ya kwa mbwa na paka. Pamoja na kuwa maadhimisho haya yamefanyika hapa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Kalange kwa upande wa Singida, halmashauri
zote 15 ambazo ndizo zinatengeneza kanda ya kati zinaendelea na maadhimisho
haya na hivi sasa na zinafanya zoezi ya janjo kwa mbwa na paka” alisema Dkt. Ibrahim.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa
Umoja Wafugaji Mbwa Dodoma, Francisi Macha alisema kuwa zoezi la kuchanja mbwa
ni muhimu sana na pia wapo wafugaji wengi sana na changamoto ya kichaa cha mbwa
ni changamoto kubwa sana kwa maisha ya binadamu ya kila siku. ”Ni vizuri sana
watu kuelewa umuhimu wa kuchanja mbwa wetu kwasababu idadi ya mbwa katika jiji letu
imekuwa kubwa. Hivi ninavyoongea kwenye umoja wetu kuna wanachama wasio pungua
218 kwahiyo, unaweza kuona kwamba ni kwa namna gani tutaongeza nguvu kwenye uelewa
wa hili zoezi kwa ujumla” alisema Dkt. Ibrahim.
Nae Mfugaji wa mbwa Mtaa wa Chang’ombe,
John Katema alisema kuwa nimeenda kuchanja mbwa wake kuwapa dawa ya minyoo pamoja
na dawa ya kuzuia wadudu kama viroboto. “Kwasababu cha kwanza, nawajali afya
zao na pili, napenda kuwashauri wafugaji wenzangu wa mbwa ambaye hajaweza
kufika katika utowaji chanjo aweze kufika kwa maana zoezi hili ni la siku saba.
Hivyo, ningependa kuwaambia kwamba ukiwa na mbwa ni lazima umjali na kumpenda
kwa faida yake pamoja na wewe mwenyewe unajilinda kutokana na madhara kama
endapo ikatokea akakudhuru” alisema Katema.
Ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kichaa cha
mbwa unakadiriwa kusababisha vifo vya watu 55,000 duniani na watu wapatao 1,500
nchini kila mwaka kutokana na ugonjwa huo wakati dunia ikilenga kuutokomeza
ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.
Comments
Post a Comment