Ubalozi wa Sweden kuendelea kushirikiana na Tanzania
Na. Faraja Mbise, DODOMA
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta
Macias ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kufanya mazungumzo na viongozi
wakuu kutoka ofisi hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary
Senyamule.
Katika mazungumzo hayo, Balozi Macias alisema wanashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Mpango wa kunusuru Kaya Masikini nchini (TASAF), elimu na katika Taasisi za kidemokrasia.
Balozi Macias aliongeza kwa kusema kuwa
watashirikiana katika kutoa ujuzi na teknolojia katika maeneo mbalimbali ya
uwekezaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Rosemary Senyamule aliualika Ubalozi wa Sweden kuja kuwekeza makao makuu ya
nchi jijini Dodoma. Aliwaeleza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo masuala ya
kilimo cha zabibu kwasababu ndio kipaumbele cha Mkoa wa Dodoma.
Ziara hiyo iliambatana na zoezi la kutembelea
Mji wa Serikali Mtumba, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mabalozi na Ofisi ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Rais Utumishi
na Utawala bora.
MWISHO
Comments
Post a Comment