DC Dodoma akagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato
Na. Asteria Frank, DODOMA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kishirikiana na Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) inatekeleza mradi wa
ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato.
Kiwanja hiko cha Ndege cha kimataifa Cha
Msalato kinajegwa kwa awamu kwa kufuata mpango mkakati wa utekelezaji wa mradi
huo ukiwa na lengo la kurahisisha usafiri kati ya Tanzania na nchi jirani
pamoja na uboreshaji wa usafiri wa ndani.
Mkuu wa Wilaya wa Jiji la Dodoma, Alhaji Jabir
Shekimweri alifanya ziara katika mradi huo ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa
uwanja na alisema kuwa Suma JKT wanadhamana na ujenzi huo kwaajili ya ulinzi
kwa kudhibiti matendo ya wizi unaofanyika.
Alisema kuwa amefarijika sana kupokea taarifa
ya utekelezaji wa mradi na juhudi kwenye ‘package one’ ni asilimia 75 na
jitihata ya ‘package’ ya pili ni asilimia 43.6.
"Sehemu ya taarifa kulikiwa na
changamoto na moja wapo ni udokozi wa kwenye mradi na tumepata nafasi ya
kufanya mjadala mpana na kwa bahati na sisi tulikiwa na taarifa hizi za awali. Kwahiyo,
tulihakikisha wadau wanaohusika na usalama wa eneo la mradi tunao katika ziara
hii tupo na Suma JKT kwakutoa dhamana kwenye eneo hili. Mkandarasi pia anawajibika
pamoja na mteja ila kila mmoja akisimama kwenye nafasi yake matukio ya udokozi
hayatatokea" alisema Alhaj Shekimweri.
Aliongeza kuwa ujenzi wa uzio unaweza kutatua
changamoto ya udokozi ila pia kutoa elimu ya uzalendo kwa vijana kuhusu kufahamu
maana ya kushiriki kwenye miradi ya kimkakati kama hiyo na kupunguza ubora
kwenye udokozi. Aliongeza kuwa ni ngumu sana mtu ambae hausiki na ujenzi huo kufahamu
maeneo ambayo vifaa vya ujenzi vinahifadhiwa.
“Tunaelekea kwenye uchaguzi na kunawafanya
kazi ambao ni watanzania na wanahaki ya kupiga kura na kuna watu wengi ambao
wapo hapa na wengine walihama kwenye maeneo yao ya kiuchaguzi. Hivyo, inabidi
wakaboreshe taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura”, alisema.
MWISHO
Comments
Post a Comment