Jiji la Dodoma lasafisha korongo la Kishoka kuondoa kero ya mafuriko kwa wananchi

Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imesikia kilio cha wakazi wa Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe cha kero ya kuziba kwa korongo linalopitisha maji ya mvua na kusababisha mafuriko katika makazi yao. Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga akiongelea zoezi la kuondoa taka katika korongo la Mtaa wa Kishoka Katika utatuzi wa kero hiyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepeleka mtambo (JCB Backhoer) kwa ajili ya kufukua korongo hilo na kuondoa taka ngumu zilizotupwa kwenye korongo na kusababisha maji ya mvua kushindwa kupita. Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga alisema kuwa lengo la zoezi la kusafisha korongo hilo ni kuyawezesha maji ya mvua yaweze kupita vizuri na kutosababisha mafuriko katika makazi ya watu. “Kama mnavyoona hapa tunaendelea na shughuli ya siku tatu ya usafishaji wa korongo la maji ya mvua katika Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe. Lengo kubwa ni...