Mnadani wakumbushwa kuchukua tahadhari ya athari za mvua
Na. Dennis Gondwe, MNADANI
WANANCHI wa Mtaa wa Mnadani
wametakiwa kuchukua tahadhari ya athari inayoweza kusababishwa na mvua kwa
kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na mitaro ya kupitisha maji ya mvua
haijaziba ili kuepusha mafuriko kwenye makazi ya watu.
![]() |
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa mnadani |
Tahadhari hiyo ilitolewa na Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa alipokuwa akiwahutubia mamia ya
wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa
huo.
Wawa alisema “tupo katika
kipindi cha mvua, katika kipindi hiki milipuko ya magonjwa mbalimbali huwa
inatokea. Ni vizuri tujitahadhari na mazingira ambayo ni hatarishi. Kama
tulivyojadili suala la usafi wa mazingira linagusa kila mmoja wetu. Hivyo,
tuchukue tahadhari kadri inavyohitajika. Kipindi hiki kuna watu kuharibiwa
nyumba zao na vitu vyao kutokana na maji ya mvua. Tuhakikishe mitaro ya
kupitishia maji ni safi na haijaziba. Toeni taarifa na sisi tutazifikisha
sehemu husika, tukifanya hivyo, tutakuwa tumejijali wenyewe na kunusuru maisha
ya ndugu zetu. Toeni taarifa sahihi na sisi tutafikisha taarika kwenye eneo
husika, serikali ya mama Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inachukua hatua”.
MWISHO
Comments
Post a Comment