SIKU 100 ZA WAZIRI SILAA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Na Eleuteri Mangj, WANMM
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanya kikao na Makamishna wa
Ardhi Wasaidizi mikoa yote Tanzania Bara kutathmini siku 100 za uongozi wake
tangu ameanza kuiongoza wizara hiyo.
Kikao hicho
kimefanyika leo Desemba 21, 2023 jijini Dodoma ambapo Mhe. Waziri Silaa
amekutana Menejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa
kujitatnmini katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kuhusu matumizi bora ya ardhi.
"Hiki ni kikao
kazi cha kutathmini siku 100 na kutengeneza mpango wa kutekeleza maagizo ya
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi na
kuwahudumia wananchi wetu" amesema Mhe. Waziri Silaa.
Waziri Silaa
amewasisitiza Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuwa wana kazi ya
kusimamia watumishi walio chini yao kwa kujipanga vizuri na wana uwezo
kubadilisha jinsi sekta ya ardhi inavyoendeshwa nchini kote.
Waziri Silaa ameongeza
kuwa Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wanachapa kazi vizuri katika mikoa yote,
utendaji kazi wao utafanya taswira ya Wizara iende mbele kutekeleza maelekezo
ya viongozi wa kifaifa na kuleta tija kwa watanzania.
Aidha, Waziri Silaa
amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii na wataendelea kupokea na kuheshimu ushauri
wanaoutoa kuhusu shughuli za sekta ya ardhi nchini.
Awali akimkaribisha
Mhe. Waziri kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga
amesema kuwa Menejimenti ya Wizara na taasisi zilizochini ya Wizara kwa
kushirikiana na Makamishna Wasaidiza wa mikoa wapo tayari kupokea maelekezo ya
Mhe. Waziri kwa kuwa ndiye mwongoza njia ili kufikia malengo ya Serikali ya
kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.
Mhe. Waziri Silaa
ametimiza siku 100 katika nafasi hiyo ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 30, 2023 na kuapishwa Septemba 01,
2023.
Comments
Post a Comment