Posts

Showing posts from October, 2023

KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DODOMA YAHUDUMIA WANANCHI 3,056 NDANI YA SIKU 5

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA KLINIKI ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imehudumia wananchi 3,056 waliokuwa na kero za muda mrefu kuhusiana na sekta ya Ardhi yakiwa ni mafanikio makubwa kwa   wananchi wengi kuhudumiwa kwa muda mfupi. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo Takwimu hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake. Kayombo alisema “zoezi hili limetoa matokeo chanya kwa ujumla. Wananchi 3,056 walisikilizwa. Hati 1,474 zilitolewa papo hapo. Maombi mapya ya hati 561 yalipokelewa, namba za malipo 1,674 zilitolewa, viwanja 645 vilipandishwa kwenye mfumo, migogoro ya ardhi 774 ilisikilizwa, wananchi 149 walipata huduma za Mipango Miji na wananchi 221 walipata huduma za upimaji” alisema Kayombo. Akiongelea kliniki hiyo, alisema kuwa ililenga kutatua changamoto za Ardhi kwa haraka. “Zoezi hili ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa mkakati wa Mkoa wa Dodoma wa kumaliza changamoto za Ard...

WIZARA YA ARDHI KUBORESHA MFUMO WA ILMIS

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kuboresha mfumo wa kieletroniki wa kutunza taarifa za Ardhi (ILMIS) ili kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa hati milki ikiwa niutekelezaji maelekezo ya serikali. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Slaa alisema “tarehe 3 Oktoba, 2023 serikali ilitoa maelekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Maelekezo hayo yalihusu mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa sekta ya Ardhi. Wizara inaendelea na uboreshaji wa mfumo wa kieletroniki wa kutunza t...

JIJI LA DODOMA LAPEWA HADHI YA MKOA WA ARDHI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yaipa Halmashauri ya Jiji la Dodoma hadhi ya kuwa Mkoa wa Ardhi kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu kuboresha huduma za sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza. Slaa alisema “Wizara imeifanya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa Mkoa wa Ardhi kiutendaji ikiwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi ambae atahudumia eneo hilo na halmashauri nyingine kuwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mwingine”. Waziri huyo alisema kuwa wizara imeandaa utaratibu wa kutoa huduma kwa pamoja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma utaratibu ambao utasimamiwa na wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia tarehe 30 Oktoba,...

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA TATU YA KLINIKI YA ARDHI DODOMA

Image
 

WANANCHI WAASWA KUIBUA MALALAMIKO YA ARDHI YALIYOFUNGWA JIJI LA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuacha tabia ya kufanya bahati nasibu ya kupata haki isiyostahili baada ya kuwa malalamiko yao yamekwisha tatuliwa kwa mujibu wa taratibu na sheria. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiongea na wananchi waliojitokeza kupata huduma ya Ardhi katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kutatuliwa kero na malalamiko yao kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika siku yake ya tatu jijini hapa. Senyamule alisema “nisisitize tunaposhughulikia kero hizi niombe wananchi wa Dodoma na kutoa wito najua kuna watu wanajirudiarudia kila wakati ambao kero zao zilishafungwa ila wanajaribu bahati nasibu nyingine. Nitoe rai wale ambao kero zao zilishafungwa huna haja ya kutumia masaa yako hapa, utapata jibu lilelile ambalo ulishalipata. Tukimaliza tatizo lako tunalifunga na tunapeana taarifa, naka...

DODOMA ISIYO NA KERO ZA ARDHI YATAJWA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu yasiyokuwa na kero wala migogoro ya Ardhi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kushoto) akikabidhi moja ya Hati zilizotolewa siku a tatu ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudumiwa na kutatuliwa kero zao katika Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya tatu jijini Dodoma. Senyamule alisema “niwahakikishie Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama mwenye upendo na mama anayewapenda watanzania, jambo hili halitaki na anatamani wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu ya Dodoma na watafurahia kama watapa haki zao. Ndiyo maana amekuwa akituagiza kutatua kero zao hasa za Ardhi katika Jiji la Dodoma. Kama mkoa baada ya kupokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wametuagi...

JIJI LA DODOMA LATAMBUA JITIHADA ZA MWANAMKE WA KIJIJINI

Image
Na. Dennis Gondwe, CHIHANGA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inatambua jitihada zinazofanywa na mwanamke wa kijijini katika uzalishaji wa chakula na kusimamia lishe ya familia. Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Charity Sichona Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona alipokuwa akiongea maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini ofisini kwake leo ambayo yatafanyika katika Kata ya Chihanga jijini Dodoma. Sichona alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaadhimisha siku hiyo kwa lengo la kuendelea kutambua jitihada za mwanamke anayeishi kijijini. “Wanawake wanaoishi vijijini wanamchango mkubwa katika kuzalisha chakula na kuchangia uwepo wa chakula katika familia na nchi nzima. Hivyo, serikali imeamua kutambua jitihada zao za kilimo, ufugaji na shughuli za kiuchumi na kuwatia moyo ili waendelee kuzalisha wakati serikali ikiendelea kutatua changamoto zinawakabili” alisema Sichona. Sichona alisema ku...

WASIMAMIZI KLINIKI YA ARDHI WATAKIWA KUJALI MAKUNDI MAALUM

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WASIMAMIZI wa Kliniki ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kutoa kipaumbele kwa makundi maalum yanapokwenda kupata huduma katika kliniki hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabr Shekimweri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alipotembelea Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika siku yake ya pili jijini hapa ya kutatua migogoro ya Ardhi. Shekimweri alisema “niwaombe sana, mkusanyiko huu una watu mchanganyiko wapo wa umri wa kati, watu wazima, wazee, wenye changamoto za malazi, wajawazito na wenye ulemavu. Pamoja na utaratibu uliopangwa tuheshimu mahitaji ya haya makundi maalum” alisema Shekimweri. Aidha, aliwataka wananchi wanaokwenda kupata huduma katika kliniki hiyo kwenda na nyaraka kamili ili kuwasaidia wataalam katika kutatua kero za ardhi. “Wakati wa kuwasilisha changamoto na kero tujitahidi kuja tukiwa tumekamilisha nyaraka za...

JIJI LA DODOMA LAPONGENZWA KLINIKI YA ARDHI ILIYOWATOA WATAALAM OFISINI KUHUDUMIA WANANCHI

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kuanzisha Kliniki ya Ardhi iliyowafanya wataalam kutoka ofisini na kuweka kambi kuwahudumia wananchi eneo moja ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo eneo la Manispaa ya zamani alipotembelea na kukagua maendeleo ya Kliniki ya Ardhi inayotoa huduma jijini hapa. Shekimweri alisema “kipekee nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, niliyasema haya wakati tunakupokea hapa Dodoma baada ya kuteuliwa. Mimi nakufahamu unavyofanya kazi. Ninafahamu ni mtu unaejali sana watu na matatizo ya wananchi. Nilikuwa nawaambia wananchi ninajua kuna mkurugenzi atawasilikiza kwa nafasi na kwa staa na atawashughulikia matatizo yenu yaliyowasumbua kwa muda mrefu”. Alisem...

JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA MBADALA 1,105 KWA WANANCHI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa viwanja mbadala 1,105 kwa wananchi katika kutekeleza mkakati wake wa kumaliza migogoro ya Ardhi jijini hapa. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo akongea na waandishi wa habari Mamia ya wananchi wakiwa katika mahema kupata huduma katika Kliniki ya Adhi Jiji la Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya pili ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa. Kayombo alisema kuwa wakati anafika Dodoma kulikuwa na wananchi takribani 4,000 wanaodai viwanja mbadala. “Yaani kiwanja kimoja kimegawiwa kwa mwananchi zaidi ya mmoja. Lakini mpaka sasa tumeshatoa viwanja 1,105 kufidia wale wananchi. Mpaka sasa tunadaiwa viwanja 2,895. Matarajio mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka huu tutakiwa tumekamilisha kutoa viwanja hivyo 2,895. Kwa sababu kuna zoezi kubwa linaendelea la kupima eneo...

HATI 240 ZATOLEWA SIKU YA KWANZA YA KLINIKI YA ARDHI JIJINI DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA SIKU ya kwanza ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yapokea wananchi 1,014 ikitoa Hati miliki 240 baada ya kusikiliza wananchi 514. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo akiongea na waandishi wa habari kuhusu siku tano za Kliniki ya Ardhi katika Jiji la Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Kliniki ya Ardhi iliyoanza siku ya pili katika jiji hilo kutatua migogoro ya Ardhi. Kayombo alisema kuwa siku ya jana walipokea wananchi 1,014. “Wananchi tuliofanikiwa kuwasikiliza jana ni 514. Katika wananchi 514 tumefanikiwa kutoa Hati 240. Tulifanikiwa kusikiliza watu wenye migogoro 209. Wale waliobaki jana tumeendelea nao leo asubuhi. Leo watu ni wengi kuliko jana na wameshapewa namba na huduma zinaendelea vizuri” alisema Kayombo. Akiongelea matarajio ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa ni kutatua migogoro ya Ardhi...

SERIKALI YAANZISHA KLINIKI YA ARDHI DODOMA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI imeanzisha kliniki maalum ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya awamu ya sita. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu alipotembelea siku ya kwanza ya utekelezaji wa majukumu ya kliniki hiyo na kuongea na mamia ya wananchi waliojitokeza katika eneo la iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya zamani jijini hapa. Gugu alisema “hii ni kliniki maalum ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akishirikiana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma na Katibu Tawala Msaidizi anayehusika na Miundombinu akiiwakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Lengo ni kuwasikiliza na kutambua kero zenu kwenye masuala ya Ardhi katika Jiji la Dodoma. Tumekuja kuwasilikiza tutambue kero zenu na wananchi wanaotaka kuhakiki maeneo yao na hati miliki tuweze kuwapatia”. Alisema kuwa kliniki hiyo inaashiria dhamira y...

JIJI LA DODOMA KINARA MWENGE WA UHURU 2023 KANDA YA KATI

Image
 

MKOA WA DODOMA WAPATA HATI SAFI KATIKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023

Image
Na. Mwandishi Maalum, KITETO Mkoa wa Dodoma wapata hati safi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 baada ya miradi yake 45 kukubaliwa na katika wilaya saba na halmasahuri nane za mkoa huo.   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Mkoani Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule leo tarehe 7 Oktoba, 2023  wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga katika uwanja wa Shule ya Msingi Dosidosi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.    Senyamule akitoa taarifa ya hitimisho kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkoa wa Dodoma, alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa kwa takribani kilometa 1893 na kupitia jumla ya miradi ya maendeleo 45.   Miradi 15 iliwekewa jiwe la msingi, miradi 19 ilizinduliwa na 11 ilitembelewa yote ikiwa na jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 16. Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya sekta za elimu, a...

WILAYA YA DODOMA ILIKUSANYA 44,454,939,022 MWAKA 2022/2023

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WILAYA ya Dodoma ilikusanya mapato ya shilingi 44,454,939,022 kupitia mifumo ya kieletroniki na kutekeleza miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2022/2023. Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa. Ukusanyaji wa k odi na m apato kwa mfumo wa TEHAMA umeendelea kuimarika. “ Mheshimiwa Rais; w ilaya kwa mwaka wa fedha 2022/ 20 23 ilifanikiwa kupata m ashine za kielektroniki za kukusanyia mapato ( POS ) 304 na shilingi 44,454,939,022.82 zilikusanywa na kutumika kwenye miradi ya maendeleo ” alisema Mbugi . Kuhusu sekta ya biashara alisema malipo yote yanafanyika kupitia benki. “ Mheshimiwa Rais; Wilaya ya Dodoma imefanikiwa kusajili wafanyabiashara kwenye mfumo wa s erikali za m itaa wa ukusanyaji m apato na mali...

SHILINGI 9,539,477,529 ZACHANGIA KUONGEZA UFAULU DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WILAYA ya Dodoma ilipokea shilingi 9,539,477,529 kwa ajili ya maendeleo zilizotumika kujenga miundombinu ya elimu msingi na sekondari na kuchangia katika ukuaji sekta hiyo na kuongeza ufaulu. Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa. Mbugi alisema “ Mheshimiwa Rais; k atika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023, Wilaya ilipokea shilingi 9,539,477,529.06 kwa ajili ya maendeleo ya s ekta ya e limu.   Kati ya fedha hizo, shilingi 3,456,608,415.29 za e limu bila malipo kwa s hule za m singi na s ekondari na shilingi 6,082,869,113.77 zilitumika kujenga miundombinu katika s hule za m singi na s ekondari ” . Akiongelea uboreshaji mazingira ya kujifunzia na kufundishia alisema kuwa yameboreka. “ Mheshimiwa Rais; kuboreshw...