WILAYA YA DODOMA ILIKUSANYA 44,454,939,022 MWAKA 2022/2023
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WILAYA ya Dodoma ilikusanya mapato ya shilingi 44,454,939,022
kupitia mifumo ya kieletroniki na kutekeleza miradi ya maendeleo katika mwaka
wa fedha 2022/2023.
Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa
akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule
ya Msingi Chamwino jijini hapa.
Ukusanyaji
wa kodi na mapato kwa mfumo wa TEHAMA umeendelea kuimarika. “Mheshimiwa Rais; wilaya kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilifanikiwa kupata mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS) 304 na shilingi 44,454,939,022.82 zilikusanywa na kutumika kwenye miradi ya
maendeleo” alisema Mbugi.
Kuhusu sekta ya biashara alisema malipo yote yanafanyika kupitia benki. “Mheshimiwa Rais; Wilaya ya Dodoma imefanikiwa
kusajili wafanyabiashara kwenye mfumo wa serikali za mitaa wa ukusanyaji mapato na malipo yote ya ada za leseni
za biashara yanafanyika benki. Mwaka 2022/2023
wilaya ilifanikiwa kutoa leseni za biashara
11,794 na leseni za vileo 1,034 zilizoingiza shilingi 1,979,525,035.90 sawa na asilimia 61.8 ya lengo” alisema Mbugi.
Akiongelea
hali
ya ulinzi na usalama
kwa raia na mali zao alisema kuwa ni shwari na hakuna matukio makubwa ya
uhalifu. “Wilaya ya Dodoma ina fursa nyingi zikiwemo viwanja vya makazi na biashara, eneo la
viwanda Nala, miundombinu mizuri ya barabara za lami, ujenzi wa Reli ya mwendo
kasi na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato na vyuo vinavyotoa huduma za
elimu” alisema Mbugi.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2023 unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa
vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
MWISHO
Comments
Post a Comment