SHILINGI 9,539,477,529 ZACHANGIA KUONGEZA UFAULU DODOMA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WILAYA
ya Dodoma ilipokea shilingi 9,539,477,529 kwa ajili ya maendeleo zilizotumika
kujenga miundombinu ya elimu msingi na sekondari na kuchangia katika ukuaji
sekta hiyo na kuongeza ufaulu.
Taarifa
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa
akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia
Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja
wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa.
Mbugi
alisema “Mheshimiwa Rais; katika kipindi cha Julai
2022 hadi Juni 2023, Wilaya ilipokea shilingi 9,539,477,529.06 kwa
ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu. Kati ya fedha hizo, shilingi
3,456,608,415.29
za elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na shilingi
6,082,869,113.77 zilitumika kujenga
miundombinu katika shule za msingi na sekondari”.
Akiongelea uboreshaji
mazingira ya kujifunzia na kufundishia alisema kuwa yameboreka. “Mheshimiwa Rais; kuboreshwa kwa mazingira ya
kujifunzia na kufundishia kumeongeza ufaulu shule za msingi
kutoka asilimia 89.2 mwaka 2021
hadi asilimia 89.9 mwaka
2022. Pia wanafunzi 13,667 waliandikishwa kwa mwaka 2023 kujiunga na darasa la awali, sawa na asilimia 89.7, wanafunzi 19,508
waliandikishwa kwa mwaka 2023 kujiunga na Darasa la kwanza sawa na asilimia 103.3.
Katika shule za sekondari
udahili wa wanafunzi wa kidato
cha kwanza uliongezeka
kutoka asilimia 86 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 88.7 mwaka
2023, Kidato cha Nne ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 92.8 mwaka 2021 hadi asilimia 95.2 mwaka 2022 na kidato cha Sita umeongezeka kutoka asilimia 99.9 mwaka 2022 hadi asilimia 100 mwaka 2023” alisema Mbugi.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2023 unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa
vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
MWISHO
Comments
Post a Comment