Posts

Showing posts from 2023

Jiji la Dodoma lasafisha korongo la Kishoka kuondoa kero ya mafuriko kwa wananchi

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imesikia kilio cha wakazi wa Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe cha kero ya kuziba kwa korongo linalopitisha maji ya mvua na kusababisha mafuriko katika makazi yao. Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga akiongelea zoezi la kuondoa taka katika korongo la Mtaa wa Kishoka Katika utatuzi wa kero hiyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepeleka mtambo (JCB Backhoer) kwa ajili ya kufukua korongo hilo na kuondoa taka ngumu zilizotupwa kwenye korongo na kusababisha maji ya mvua kushindwa kupita. Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga alisema kuwa lengo la zoezi la kusafisha korongo hilo ni kuyawezesha maji ya mvua yaweze kupita vizuri na kutosababisha mafuriko katika makazi ya watu. “Kama mnavyoona hapa tunaendelea na shughuli ya siku tatu ya usafishaji wa korongo la maji ya mvua katika Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe. Lengo kubwa ni...

Jiji la Dodoma kuendelea kusafisha makorongo ya maji ya mvua kuzuia mafuriko katika makazi ya wananchi

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma itaendelea kuyafanyia usafi kwa kuondoa taka ngumu makorongo yote ili yaweze kupitisha maji vizuri na kuondoa kero ya mafuriko wakati mvua zinaponyesha. Mkuu wa Kitengo cha usafi na uthibiti wa kata ngumu, Dickson Kimaro akielezea ukubwa wa kazi ya kusafisha kongoro na kuondoa taka ngumu katika Mtaa wa Kishoka Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha usafi na uthibiti wa kata ngumu, Dickson Kimaro alipokuwa akiongelea mipango ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kuhakikisha wananchi hawaathiriki na mafuriko yatokanayo ma maji ya mvua kushindwa kupita kwenye makorongo. Kimaro alisema “Halmashauri ya Jiji la Dodoma itaendelea kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha wananchi hawapati kero kama hizi zinazoonekana. Kama mnavyoona kule mbele kuna eneo ambalo maji yakifika darajani yanagota na kurudi kuingia katika makazi ya watu. Hapa Mtaa wa Kishoka tunasafisha korongo hili kwa kuondoa taka ngumu na kuliongezea kina il...

Kata ya Chamwino yatekeleza agizo la RC la usafi wa Mazingira

Image
KATA ya Chamwino imetekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule la kufanya usafi kila jumamosi kwa lengo la kuliweka Jiji la Dodoma safi. Akiongelea utekelezaji wa agizo hilo, Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa usafi huo ulifanyika katika maeneo ya korongo la Mailimbili na Mwaja. Usafi huo ulihusisha kufyeka vichaka na nyasi, kuokota makopo na mifuko ya plastiki iliyozagaa katika korongo na kuzibua mitaro ya maji yenye urefu wa mita 100, aliongeza. Alisema kuwa kata yake ilitumia zoezi hilo la usafi wa pamoja kuwahimiza wananchi kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na makazi pamoja na kuhakikisha wanatunza mazingira katika msimu huu wa sikukuu. Usafi wa pamoja katika Kata ya Chamwino ulishirikisha Afisa Mtendaji Kata, Wenyeviti wa mitaa, mabalozi na wananchi.  

WAZIRI SILAA ASIMAMISHA MATUMIZI YA KITUO CHA MAFUTA CHA BARREL DAR ES SALAAM

Image
Na Eleuteri Mangi, WANMM   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam na kupiga marufuku ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchi nzima vinavyojengwa kwenye makazi ya watu hatua inayohatarisha usalama wa watu na mali zao.   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akiozungumza na wananchi wa Mikocheni wakati akisimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni Desemba 23, 2023 jijini Dar es salaam Waziri Silaa ametoa agizo hilo Desemba 23, 2023 alipoenda kukagua eneo kilipojengwa kituo hicho na aliambatana na Kamati ya ulizi na usalama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.   "Kufuatia agizo hili, nawaagiza Wakuu wote wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji nchi nzima wafanye uhakiki wa vituo vya mafuta kwa maana ya viwanja, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, mchakato uliotumika, ukubwa wa viw...

WIZARA YA ARDHI YAZINDUA MFUMO RASMI WA KUWAHUDUMIA WANANCHI “ARDHI APP”

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua mfumo rasmi wa kuwahudumia wananchi popote walipo kupitia simu ya kiganjani “Ardhi App” wa kuwasilisha malalamiko ama migogoro ya ardhi katika wizara hiyo.   Akizindua mfumo huo  Desemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa  amesema, mfumo huo ni rafika na utawarahisishia wananchi kupata huduma wakiwa katika maeneo yao popote walipo. “Mfumo huu wa “Ardhi App” utakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wetu, utapunguza gharama na muda wa wananchi kupata huduma katika maeneo mbalimbali nchini, badala yake mwananchi atapata huduma za ardhi kiganjani mwake” amesema Waziri Silaa. Kwa mujibu wa Waziri Silaa, mfumo huo pia utawasaidia wananchi kutoa mrejesho wa ubora wa huduma walizopatiwa pamoja na kuwasilisha tena malalamiko husika pale ambapo hawajaridhika...

SIKU 100 ZA WAZIRI SILAA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Image
Na Eleuteri Mangj, WANMM   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanya kikao na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi mikoa yote Tanzania Bara kutathmini siku 100 za uongozi wake tangu ameanza kuiongoza wizara hiyo.   Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 21, 2023 jijini Dodoma ambapo Mhe. Waziri Silaa amekutana Menejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kujitatnmini katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi bora ya ardhi.   "Hiki ni kikao kazi cha kutathmini siku 100 na kutengeneza mpango wa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi na kuwahudumia wananchi wetu" amesema Mhe. Waziri Silaa.   Waziri Silaa amewasisitiza Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuwa wana kazi ya kusimamia watumishi walio chini yao kwa kujipanga vizuri na wana uwezo kubadilisha jinsi sekta ya ardhi inavyoendeshwa nchini kote.   Waziri Sil...

Vikundi vyapatiwa Mil. 215 Kata ya Mnadani

Image
  Na. Dennis Gondwe, MNADANI VIKUNDI ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu 18 vimepata mikopo ya shilingi 215,000,000 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2023 katika Kata ya Mnadani. Picha kutoka maktaba ya Jiji la Dodoma Takwimu hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Mnadani, Caroline Massawe alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Mnadani. Massawe alisema kuwa sekta ya maendeleo ya jamii imepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka mitatu na kuwainua wananchi wa kata hiyo. “ Kuanzia mwaka 2021 hadi sasa katika Kata ya Mnadani, vikundi 18 vimepata mikopo na shilingi 215,000,000 zimetolewa. Kati ya vikundi hivyo, vikundi sita ni vya wanawake vilivyokopeshwa shilingi 49,000,000. Vikundi tisa vya vijana vimekopeshwa shilingi 142,000,000 na vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu vimekopeshwa shilingi 24,000,000 na kufanya jumla ya shilingi 215,000,000. Mikopo hii imekuwa na manufaa...

Marufuku mifugo kuzurura Kata ya Mnadani

Image
Na. Dennis Gondwe, MNADANI WAFUGAJI wa Kata ya Mnadani wametakiwa kuacha tabia ya kuzurulisha mifugo yao na kufanya ufugaji wa ndani ili kwenda sambamba na mahitaji ya hadhi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Kata ya Mnadani, Elizabeth Shirima alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara. Shirima alisema kuwa kata hiyo inakabiliwa na ufugaji holela. “Mifugo inayozuzura ovyo ni ile ya ufugaji huria, Dodoma sasa ni Jiji hivyo, hakuna utaratibu wa kuzurulisha mifugo hasa katika barabara za lami na mitaa. Naomba wafugaji kama hamuwezi kufugia ndani mnashauriwa kuhamisha mifugo kutoka Jiji kwenda maeneo yanayokubalika hasa ufugaji wa wanyama wakubwa kama ng’ombe, mbuzi, punda, na ngamia. Kuna wakati gari la kubeba wagonjwa linakimbiza mgonjwa hospitali inabidi lisimame kusubiri mifugo ipite barabara kuu. Halmashauri ya Jiji imetenga maeneo kwa ajili ya wafugaji. Unapohitaji kununua eneo la kufuga mifugo nen...

KATA YA CHAMWINO YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA

Image
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO Timu ya wataalam kutoka Kata ya Chamwino yajikita katika utoaji wa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa makundi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha uelewa mpana katika mapambano hayo unaenea kwa jamii. Akielezea maeneo yaliyopewa  kipaumbele na timu hiyo katika kutoa elimu, Afisa Mtendaji kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kipaumbele ni kutoa elimu kwa jamii. Alisema kuwa timu hiyo ilijikita katika kuelezea wajibu wa wazazi na walezi katika makuzi ya watoto na sheria inayomlinda mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maeneo mengine yaliyopewa msisitizo ni umuhimu wa ulinzi wa watoto wa kiume na madhara kwa watoto hao endapo hawatapewa uangalizi wa karibu na hatua za kufanya pale mtoto amapofanyiwa ukatili. Aidha, wazazi na walezi walitaarifiwa uwepo wa kituo cha huduma za pamoja na msaada kwa watoto waliofanyiwa ukatili (one stop center). Nkelege alisema kuwa timu shirikishi ya wataalamu ya Kata ya Chamwino iliongozwa na Afisa Mtendaj...

Bodaboda ni kazi, epukeni uhalifu

Image
Na. Dennis Gondwe, MNADANI VIJANA waendesha Pikipiki (bodaboda) katika Kata ya Mnadani wametakiwa kuichukulia kazi ya kuendesha pikipiki kama kazi nyingine na kujiepusha na kujiunga kwenye makundi ya uhalifu. Picha kutoka mtandaoni Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Focus Ishika alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo. Mkaguzi Msaidizi Ishika ambae pia ni Polisi Kata ya Mnadani alisema kuwa vijana waendesha bodaboda wanakosa elimu ya umuhimu wa kazi wanayofanya. “Vijana wetu wa bodaboda wanakosa elimu juu ya umuhimu wa kuichukulia kazi ya bodaboda kama kazi nyingine. Wazazi wenye watoto wanaoendesha pikipiki toeni elimu kwa vijana wenu ajira ya udereva pikipiki waichukulie kama yule anayeamka asubuhi na kwenda benki au kwenda kufundisha (mwalimu) wanatakiwa kuifanya kazi hiyo kwa moyo na bidii. Kwa hiyo makosa tunayo sisi. Mwanao anatoka asubuhi na pikipiki hujui anapaki kituo gani, hujui rafiki zake n...

Afisa Mifugo Kata ya Mnadani anaupiga mwingi

Image
Na. Dennis Gondwe, MNADANI KATA ya Mnadani inajivunia utendaji kazi wa Afisa Mifugo kwa kuhakikisha wananchi wanakuwa na mifugo yenye afya kutokana na kupata huduma zote za chanjo kwa wakati. Afisa Mifugo Kata ya Mnadani, Elizabeth Shirima Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Mnadani, Caroline Massawe alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Kata ya Mnadani kwa kipindi cha miaka mitatu (2021-2023) katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Mnadani. Massawe alisema “nikiwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mnadani, napenda kumpongeza Afisa Mifugo wa Kaya ya Mnadani, anajitahidi kwa kweli kutekeleza majukumu yake ya kazi anajituma na ni muwajibikaji mzuri sana. Kwa wale wanaofuga natumaini wanalitambua hilo, anawatembelea wananchi kuchanja mifugo yao kwa wakati na mbwa wanaozurura anawachanja pamoja na majukumu mengine, mama huyu anaupiga mwingi”. Akiongelea mafanikio ya sekta ya mifugo, alisema kuwa sekta hiyo imefanikiwa kudhibiti magonjwa ya mlipuko na magonjwa mengine...

Serikali awamu ya sita yaipaisha Mnadani

Image
  Na. Dennis Gondwe, MNADANI SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu kwenye Kata ya Mnadani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za msingi zinazojengwa kwenye Kata ya Mnadani hii imesaidia kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Mnadani, Caroline Massawe alipokuwa akielezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Mnadani uliofanyika katika ofisi ya kata hiyo. Massawe alisema kuwa kwa asilimia kubwa mafanikio mengi ya sekta ya elimu katika Kata ya Mnadani yametokana na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mafanikio katika sekta ya elimu ni uongezekaji wa miundombinu shuleni, idadi ya wanafunzi imeongezeka, shule mpya kuanzishwa, mafunzo ya walimu kazini, al...

Mnadani yaweka kipaumbele ulinzi na usalama

Image
  Na. Dennis Gondwe, MNADANI WAKAZI wa Mtaa wa Mnadani katika Kata ya Mnadani wametakiwa kuweka kipaumbele swala la ulinzi na usalama ili jamii iwe salama katika kipindi cha sherehe za mwisho wa mwaka. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa akisisitiza jambo Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo. Wawa alisema “tunapoelekea katika sherehe za Krismasi na mwaka mpya, niwaombe sana wananchi wangu msiache makazi bila mtu anayebaki nyumbani. Kipindi hicho kina mkesha, unakuta watu wamefunga nyumba wameenda kwenye mkesha, unarudi nyumbani unakutana na kitu ambacho hukutegemea. Tuchukue tahadhari, kama mnaenda kwenye mkesha mjipe ratiba, wengine waende kwenye mkesha na wengine wabaki waende ibada ya asubuhi. Ulinzi unaanzia kwako mwenyewe kujilinda wewe na mali yako. Niwaombe sana tulisimamie hili ili kuepuka changamoto zinazoweza kudhibitiwa”...

Mnadani wakumbushwa kuchukua tahadhari ya athari za mvua

Image
  Na. Dennis Gondwe, MNADANI WANANCHI wa Mtaa wa Mnadani wametakiwa kuchukua tahadhari ya athari inayoweza kusababishwa na mvua kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na mitaro ya kupitisha maji ya mvua haijaziba ili kuepusha mafuriko kwenye makazi ya watu. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa mnadani Tahadhari hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnadani, Hema Wawa alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo. Wawa alisema “tupo katika kipindi cha mvua, katika kipindi hiki milipuko ya magonjwa mbalimbali huwa inatokea. Ni vizuri tujitahadhari na mazingira ambayo ni hatarishi. Kama tulivyojadili suala la usafi wa mazingira linagusa kila mmoja wetu. Hivyo, tuchukue tahadhari kadri inavyohitajika. Kipindi hiki kuna watu kuharibiwa nyumba zao na vitu vyao kutokana na maji ya mvua. Tuhakikishe mitaro ya kupitishia maji ni safi na haijaziba...