‘Team Aprili’ wapanda miti Shule ya Msingi Mahungu kusherehekea siku yao ya kuzaliwa
Na. Nancy Kivuyo, KIZOTA Watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejumuika pamoja kusherehekea mwezi wa kuzaliwa kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Mahungu. Wakitoa hisia zao za furaha walipotembelea shule hiyo mpya, watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiwemo Afisa Elimu Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mwl. Prisca Mgalula alisema kuwa wameichagua Shule ya Msingi Mahungu ili kuongeza uzuri wa mandhari ya shule hiyo mpya. “Mimi nimezaliwa tarehe 26 Aprili na tumeichagua shule hii kusherehekea kwa kupanda miti takribani 100. Kwa maana hiyo tunaendelea kuhamasisha agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma la ‘Mti wangu, Birthday yangu’ kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kutunza mazingira, lakini pia itawasaidia kujifunzia kwa vitendo hapo baadae" alisema Mwl. Mgalula. Nae, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahungu, Onesphory Massawe alianza kwa kusema kuwa wanafurahi kuwapokea watumushi hao na wanaahidi kuitunza miti hiyo ili ipendezeshe mandhari ya eneo...