Posts

Showing posts from August, 2024

Baraza la Madiwani la Jiji la Dodoma lapitisha Hesabu za Mwaka 2023/2024

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA Baraza la Madiwani la Jiji la Dodoma limefunga rasmi hesabu za mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2024, baada ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya ufungaji wa hesabu za halmashauri. Kwa mujibu wa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Jiji, CPA. David Rubibira alisema chanzo kikuu cha mapato ya halmashauri hiyo ni tozo, faini na ushuru mbalimbali. Mapato mengine yanatokana na michango ya afya, uwekezaji, pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu, aliongeza. "Mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri ni pamoja na mapato yenye tozo (kodi) ambayo ni kiasi cha shilingi bilioni 34.7, faini na tozo ni shilingi bilioni 2.6, Mapato mengineyo ni shilingi bilioni 6.6. Michango mengineyo ya afya ni shilingi bilioni 1.9, mapato yapatikanayo kwenye uwekezaji ni shilingi bilioni 5.5 na mapato toka serikali kuu ni shilingi bilioni 83.08 ambapo jumla ya mapato na matumizi yote ya ndani ya halmashauri ni shilingi bilioni 134.4" alisema CPA. Rubibira. Kwa upan...

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapokea taarifa ya ufungaji hesabu mwaka 2023/2024

Image
Na. Jackline Patrick na Emmanuel Lucas, DODOMA Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwaajili ya kujadili taarifa ya ufungaji hesabu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 umepokea, kujadili na kupitisha taarifa hiyo. Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira akichangia taarifa ya kufunga hesabu za halmashauri Mkutano huo ulifanyika leo tarehe 29 Agosti, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Wakati akichangia taarifa hiyo, Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira alisema kuwa taarifa hiyo imeandaliwa vizuri. “Mstahiki Meya, kwanza tumeipokea taarifa na niipongeze timu ya wataalamu kwa kuandaa na kuwasilisha hii taarifa. Lakini la pili, Mstahiki Meya taarifa hii imetupa dira ya mwaka huu wa fedha kwenye yale mapungufu yaliyojionesha kwenye taarifa hii katika utekelezaji wa shughuli zetu za halmashauri, tukayafanyie kazi ili taarifa ya mwaka unaokuja basi haya mapungufu yaweze kupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa hii itup...

Mstahiki Meya Jiji la Dodoma ahimiza Uwajibikaji

Image
Na. Francisca Mselemo, DODOMA Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kupokea na kujadili taarifa ya kufunga hesabu hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2024. Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA David Rubibira Akiwasilisha taarifa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA David Rubibira alisema kuwa taarifa hiyo inawasilishwa kwa mujibu wa sheria. “Mheshimiwa Mstahiki Meya, hesabu hizi sio ngeni. Naomba Baraza lako tukufu lifahamu kwamba ni zilezile ambazo huwa tunakutana na kuzijadili kila robo, za mapato na matumizi. Hii ni kwamba tu ni takwa la kisheria. Tunatakiwa tuziandae katika mpango wa uwasilishaji wa kimataifa. Umuhimu wa hizi hesabu ni kwamba ni takwa la kisheria, kwa maana tunapomaliza mwaka, kwa Halmashauri tunatakiwa kuwa na hesabu za mwaka husika, ambazo katika kipindi kisichozidi miezi mitatu baada ya mwaka kuisha, zinatakiw...

Madiwani Jiji la Dodoma wapitisha taarifa ya ufungaji hesabu za mwaka 2023/2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limepokea taarifa ya ufungaji wa hesabu kuishia tarehe 30 Juni, 2024 na kushauri kuwa changamoto zilizojitokeza katika mwaka ulioisha zitatuliwe ili zisijitokeze katika ufungaji hesabu ujao. Mwenyekiti wa Mkutano huo, Prof. Davis Mwamfupe akifungua mkutano Baada ya taarifa ya ufungaji wa hesabu kuishia tarehe 30/6/2024 kuwasilishwa kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa ya ufungaji wa hesabu iliyowasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wajumbe waliipokea. Mwenyekiti wa Mkutano huo, Prof. Davis Mwamfupe aliwahoji wajumbe kama wanaipokea taarifa hiyo na kwa kauli moja waliipokea taarifa hiyo. Alisema kuwa taarifa hiyo imehusisha mapendekezo ya Kamati ya Fedha na Utawala kama walivyoshauri. Akiwasilisha taarifa ya ufungaji hesabu za halmashauri kuishia tarehe 30 Juni, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu, CPA Da...

Mikakati ya Usalama Barabarani inalenga kudhibiti ajali

Image
Na. Flora Nadoo, DODOMA Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo ameitaja mikakati ya usalama barabarani kuwa inalenga kudhibiti madereva walevi, wazembe na wanaoendesha kasi Pamoja na mambo mengine. Alizungumza hayo tarehe 26 Agosti, 2024 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani na Miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Sillo aliwataka madereva na wananchi wawe waangalifu na vyombo vya moto pamoja na sheria za barabarani ili kuepuka ajali za barabarani zisizo za lazima. “Mkakati wa Usalama Barabarani unalenga maeneo yafuatayo uthibiti wa madereva walevi na wanaoendesha kwa uzembe, uthibiti wa mwendokasi kwa madereva, kuwashirikisha wamiliki wa vyombo vya moto katika dhana ya uwajibikaji. Hii ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na madereva wenza kwa mabasi ya masafa marefu. Vilevile, kuthibiti uendeshaji wa magari bila sifa au kutokuwa na leseni...

Pikipiki zaendelea kuchangia vifo ajali za barabarani

Image
Na. Anna Stanley, DODOMA SERIKALI imeeleza kuwa vyanzo vya ajali zinazosababishwa na pikipiki zimeendelea kuchangia vifo ya watu wengi wakati mwaka 2023 zikisababisha vifo wa watu 376 na kupoteza nguvu kazi ya taifa wakati wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu. Kauli hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa na miaka 50 ya Baraza la Usalama Barabarani yaliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Dkt. Mpango alisema "ndugu wananchi na waheshimiwa viongozi, Pikipiki ni miongoni mwa vyombo vya moto vinavyotoa huduma ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria mijini na vijijini, ajali zinazohusu pikipiki zimekuwa nyingi mno zinaongezeka mwaka hadi mwaka kwa mfano katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Desemba mwaka jana 2023, kulikuwa kuna jumla ya matukio 435 ya ajali za pikipiki yalioripotiwa katika kipindi hicho, idadi ya vifo vilivyotokana na ajali...

Timu ya Veterani kutoka Zanzibar yaibuka mshindi katika Bonanza Dodoma

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA Timu ya mpira wa miguu ya Veterani kutoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar imefanikiwa kuibuka mshindi katika Bonanza la mpira wa miguu lililofanyika katika uwanja wa Magereza jijini Dodoma na kupewa kombe. Mkuu wa Gereza kuu la Isanga, Zephania Neligwa (kulia) akimkabidhi kombe kepteni wa timu ya mpira wa miguu ya Veterani kutoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar Bonanza hilo lilifanyika tarehe 24 Agosti, 2024 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani na kuleta burudani kwa mashabiki. Katika mchezo wa fainali, timu ya Veterani kutoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar ilionesha kiwango cha juu, hasa katika eneo la ulinzi ambapo waliweza kuzuia mashambulizi mengi ya wapinzani wao. Mchezaji wa timu ya Veterani kutoka Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Haji Ramadhani alisema kuwa ushindi wao ulitokana na juhudi za pamoja na umakini wa kila mchezaji, huku wakionesha nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja. “Bonanza limekuwa zuri, kuanz...

Makamu wa Rais azungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma

Image
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Philip Mpango ameiagiza Serikali ngazi ya Mkoa wa Dodoma kuendelea kutafutia ufumbuzi migogoro ya ardhi iliyokithiri hususan fidia kwa ardhi iliyotwaliwa na utekelezaji wa mgawanyo wa ardhi wa 70% kwa 30%.  Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma katika Mkutano uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amesema changamoto hiyo ya ardhi mkoani Dodoma kwa kiasi kikubwa imewafanya wanachama pamoja na wananchi kuwa na manung’uniko na hata kufikia hatua ya kususia uchaguzi. Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kushirikiana na Waziri wa Ardhi kwa pamoja na uongozi wa Jiji la Dodoma kuongeza nguvu zaidi katika kushughulikia migogoro hiyo. Dkt. Mpango amewahimiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani ...

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024

Image
Na. Anna Stanley, DODOMA Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa ametoa tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka na uchaguzi utafanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa Mchengerwa aliyasema hayo katika viwanja vya Chinangali park, jijini Dodoma wakati akizungumza na wananchi na kuwahamasisha kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa na kujitokeza kupiga kura. "Tangazo hili limetolewa chini ya Kanuni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya mwaka, 2024 pamoja na matangazo ya serikali Na. 571, Na. 572, Na. 573, Na. 574 ya mwaka 2024" alisema Mchengerwa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 145 na Ibara ya 146, inaeleza uwepo wa Serikali za Mitaa pamoja na madhumuni yake ambapo miongoni mwa madhumuni ni pamoja na kupeleka madaraka kwa wananchi, alisema. “Sheria za Serikali za Mitaa, Mam...

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini Novemba, 2024

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza rasmi ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa alitoa tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo alieleza kuwa tangazo hilo limetolewa chini ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2024 pamoja na matangazo ya Serikali namba 571, 572, 573 na 574 ya mwaka 2024. "Mtiririko wa tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni utangulizi, masharti muhimu ya uchaguzi na ratiba ya uchaguzi. Kwa wagombea wa nafasi za uongozi, wanatakiwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu. Uteuzi wa wagombea utafanyika siku 19 kabla ya uchaguzi na endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee kwa nafasi husika, atateuliwa moja kwa moja” alisema Mchengerwa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza...

Diwani Fundikira adhamiria kumaliza Kero za Wafanyabiashara wa Soko la Mavunde

Image
Na. John Masanja, CHANG’OMBE Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Bakari Fundikira amefanya kikao na viongozi wa Soko la Mavunde chenye dhamira ya kuziangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara wa soko hilo na kuzifanyia utatuzi. Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Bakari Fundikira akiongea na waandishi wa habari Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kata ya Chang'ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kikao hicho, Diwani Fundikira alisema moja ya changamoto walizozitambua ni pamoja na changamoto ya uwelewa wa mikataba pia kutozingatia sheria na taratibu za uendeshaji wa shughuli za kibiashara ndani ya soko. “Lengo letu sisi viongozi ni kuhakikisha kuna uelewa mzuri kwa wafanyabiashara hawa kuhusu jinsi ya kuendesha shughuli zao wakiwa kwenye mazingira rafiki kwa kuzingatia sheria na taratibu. Pia serikali yetu iweze kukusanya mapato pasipo mtu kushurutishwa wala kulazimishwa” alisema D...

Diwani Fundikila awataka wananchi kuendeleza amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Emmanuel Lucas, CHANG’OMBE Diwani wa Kata ya Chang`ombe, Bakari Fundikira amewataka wananchi kuendelea kutunza amani, upendo na mshikamano hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa kutoa tamko la uchaguzi wa serikali za mitaa. Diwani wa Kata ya Chang`ombe, Bakari Fundikira akisisitiza jambo Kauli hiyo aliitoa kwa waandishi wa Habari baada ya kikao na viongozi wa Soko la Mavunde kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kata ya Chang'ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Diwani Fundikira alisema “kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa ameshatoa tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa tarehe 27 Novemba, 2024. Rai yangu kwa wananchi wa Kata ya Chang`ombe na wananchi wengine, itakapofika wakati wa uandaaji wa daftari la wapiga kura cha kwanza tujitokeze wananchi wote wenye sifa tujiandikis...

CCM yawataka wanachama kushiriki uchaguzi ujao

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Philip Mpango amehizima wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi na kushiriki ili kuhakikisha ushindi katika chama chao. Kauli hiyo aliitoa katika hafla ya kumpokea iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Dkt. Mpango ambae ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema kuwa ni muhimu kwa wanachama wa CCM kujitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Uchaguzi ni muhimu na lazima kwa kila mwananchi kushiriki aliongeza kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni jambo la msingi kwa mafanikio ya watanzania na chama hicho, aliongeza. “Tarehe 27 Novemba, mwaka huu tutafanya uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao tutafanya uchaguzi mkuu. Ili kukipa chama chetu ushindi katika chaguzi hizi ni lazima tujipange ili kuhakikisha tunapata ushind...

Kata ya Zuzu yajivunia mafanikio ya utekelezaji miradi ya maendeleo

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA SERIKALI yapongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi wa Kata ya Zuzu ikiwa na matokeo chanya. Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah Pongezi hizo zilitolewa na Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Diwani Abdallah alisema kuwa miradi ya ujenzi wa madarasa mapya, visima vya maji na barabara za lami inakwenda sambamba na malengo ya serikali ya kuhakikisha huduma bora kwa wananchi. Miradi hiyo imeanza kutoa matokeo chanya na wananchi wanaendelea kunufaika nayo. "Kwanza tunatekeleza mradi mkubwa wa Kituo cha Afya Zuzu kitakachogharimu shilingi milioni 550 na mpaka sasa takribani shilingi millioni 320 tumeshazipokea na ujenzi unaendelea. Tumejenga madarasa nane, matundu 16 ya vyoo na ofisi za walimu kwa ajili ya kidato cha tano na sita ambao tunatarajia mwaka unaofuatia tutaanza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita. "Lakini pia tunaj...