CCM yawataka wanachama kushiriki uchaguzi ujao
Na. Valeria Adam, DODOMA
Kuelekea katika uchaguzi wa serikali
za mitaa mwaka 2024 Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Philip
Mpango amehizima wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi na kushiriki ili
kuhakikisha ushindi katika chama chao.
Kauli hiyo aliitoa katika
hafla ya kumpokea iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi na kufanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Dkt. Mpango ambae ni Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema kuwa ni muhimu kwa
wanachama wa CCM kujitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga
kura. Uchaguzi ni muhimu na lazima kwa kila mwananchi kushiriki aliongeza kuwa
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni jambo la msingi kwa mafanikio ya watanzania
na chama hicho, aliongeza.
“Tarehe 27 Novemba, mwaka
huu tutafanya uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao tutafanya uchaguzi
mkuu. Ili kukipa chama chetu ushindi katika chaguzi hizi ni lazima tujipange
ili kuhakikisha tunapata ushindi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wabunge, madiwani na viongozi wote katika ngazi za serikali za mitaa.
Lakini pia kwa kutekeleza
ipasavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 na kutoa hamasa ya kutosha kwa
wanachama wenzetu ili wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura na kushiriki michakato yote ya taifa. Haitoshi tu kujiandikisha ni
lazima kushiriki uchaguzi” alisema Dkt. Mpango.
Katika kuimarisha uchumi wa
CCM, alihimiza kwa viongozi wa chama kuwa waadilifu katika kusimamia miradi na
mapato ya chama. “Viongozi msimamie miradi na mapato ya chama kwa uadilifu
pamoja na kuhakikisha mali zote za CCM zinatumika kwa manufaa ya chama ili
kuimalisha uchumi wa chama chetu na kuepuka kuathiri uendeshaji wa shughuli za
chama” alisema Dkt. Mpango.
MWISHO
Comments
Post a Comment