Diwani Fundikila awataka wananchi kuendeleza amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Na. Emmanuel Lucas, CHANG’OMBE
Diwani wa Kata
ya Chang`ombe, Bakari Fundikira amewataka wananchi kuendelea kutunza amani,
upendo na mshikamano hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za
mitaa 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa kutoa tamko la uchaguzi wa serikali za mitaa.
Diwani wa Kata ya Chang`ombe, Bakari Fundikira akisisitiza jambo
Kauli hiyo
aliitoa kwa waandishi wa Habari baada ya kikao na viongozi wa Soko la Mavunde kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi
ya Kata ya Chang'ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Diwani
Fundikira alisema “kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Waziri mwenye
dhamana Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa ameshatoa tarehe ya uchaguzi ambayo
itakuwa tarehe 27 Novemba, 2024. Rai yangu kwa wananchi wa Kata ya Chang`ombe
na wananchi wengine, itakapofika wakati wa uandaaji wa daftari la wapiga kura
cha kwanza tujitokeze wananchi wote wenye sifa tujiandikishe ili tuwe na sifa
ya kuchagua na kuchaguliwa”.
“Kimsingi
kwenye suala la ulinzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi katika kata
kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwasababu kuna Polisi Kata, tunakamati
ya ulinzi ya kata lakini pia tunazidi kutoa elimu kwenye ngazi za mitaa
kuhusiana na suala la kutunza amani, upendo na mshikamano” aliongeza Fundikira.
MWISHO
Comments
Post a Comment