Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024
Na.
Anna Stanley, DODOMA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi
Mchengerwa ametoa tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka na uchaguzi utafanyika
tarehe 27 Novemba, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa
Mchengerwa
aliyasema hayo katika viwanja vya Chinangali park, jijini Dodoma wakati
akizungumza na wananchi na kuwahamasisha kugombea nafasi za uongozi wa serikali
za mitaa na kujitokeza kupiga kura.
"Tangazo
hili limetolewa chini ya Kanuni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya mwaka, 2024
pamoja na matangazo ya serikali Na. 571, Na. 572, Na. 573, Na. 574 ya mwaka
2024" alisema Mchengerwa.
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 145 na Ibara ya 146,
inaeleza uwepo wa Serikali za Mitaa pamoja na madhumuni yake ambapo miongoni
mwa madhumuni ni pamoja na kupeleka madaraka kwa wananchi, alisema.
“Sheria
za Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya, sura Na. 287 ya Serikali za Mitaa, Mamlaka
kamili, sura Na. 288 zinaelekeza kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, lengo
ni kufanya serikali za mitaa ziongoze kidemokrasia. Kwa mujibu wa kifungu cha
201 ‘A’ cha Sheria za Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya, sura Na. 287 na
kifungu Na. 77A, huongoza uchaguzi huo wa serikali za mitaa, na viongozi
wanaochaguliwa katika ngazi hii ni, wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa halmashauri
ya vijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji,
wagombea wote katika ngazi mbalimbali za uongozi wanatakiwa kuwa wanachama wa
vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu" alisema Mchengerwa.
Uchaguzi
wa mwisho wa serikali za mitaa ulifanyika mwezi Novemba, 2019. Hivyo, uchaguzi
mwingine unatakiwa kufanyika mwezi Novemba, 2024, uandikishaji na uandaaji wa
orodha ya wapiga kura utaanza siku 47 kabla ya tukio la uchaguzi, aliongeza.
Kwa
tangazo hilo, wananchi wote wanaobwa kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha
kupiga kura, kugombea na kushiriki katika uchaguzi huo ili kupata viongozi wa serikali
za mitaa kwa maendeleo ya nchi wakati kampeni zitaanza tarehe 20–26 Novemba, 2024
na uchaguzi utafanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Comments
Post a Comment