Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapokea taarifa ya ufungaji hesabu mwaka 2023/2024
Na. Jackline Patrick na Emmanuel Lucas, DODOMA
Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani
kwaajili ya kujadili taarifa ya ufungaji hesabu za Halmashauri ya Jiji la
Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 umepokea, kujadili na kupitisha taarifa
hiyo.
Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira akichangia taarifa ya kufunga hesabu za halmashauri
Mkutano huo ulifanyika leo tarehe 29
Agosti, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Wakati akichangia taarifa hiyo, Diwani
wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira alisema kuwa taarifa hiyo imeandaliwa
vizuri. “Mstahiki Meya, kwanza tumeipokea taarifa na niipongeze timu ya
wataalamu kwa kuandaa na kuwasilisha hii taarifa. Lakini la pili, Mstahiki Meya
taarifa hii imetupa dira ya mwaka huu wa fedha kwenye yale mapungufu yaliyojionesha
kwenye taarifa hii katika utekelezaji wa shughuli zetu za halmashauri, tukayafanyie
kazi ili taarifa ya mwaka unaokuja basi haya mapungufu yaweze kupunguzwa kwa
kiasi kikubwa. Taarifa hii itupe dira ya utekelezaji wa shughuli za halmashauri
katika kuhakikisha tunaweka mambo sawa. Hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali atakapokuja, haya mambo mengine tuwe tumeshayatatua” alisema Diwani
Fundikira.
Mkutano
maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kujadili ufungaji wa
hesabu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuishia tarehe 30 Juni 2024, ulihudhuriwa
na madiwani, viongozi wa CCM, Kamati ya Usalama ya Wilaya, wakuu wa taasisi, wakuu
wa divisheni na vitengo na waandishi wa habari.
MWISHO
Comments
Post a Comment