Dodoma Jiji FC inafukuza Mwizi Kimya Kimya
Na. Mussa Richard, DODOMA Timu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, imeendelea na maandalizi ya kujiwinda na michezo ya Ligi kuu ya NBC Tanzania bara, kwasasa imekita kambi mkoani Arusha, na imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Mbuni FC, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Dodoma Jiji FC kuchomoza na ushindi wa bao 1-0. Akizungumza baada ya mchezo kutamatika Kocha wa Viungo wa Dodoma Jiji FC, Fransis Mkanula alisema “tumekuja hapa Arusha kuweka kambi ya siku tano, tumekuja hapa kupata mechi za kirafiki kwasababu timu imetoka kwenye mapumziko, baada ya ratiba kutoka tukaamua kuja hapa Arusha kucheza mechi za kirafiki ili kurudisha utimamu wa miili kwa wachezaji pia ukizingatia tuna maingizo mapya kwenye timu. Kwahiyo, tumekuja kutengeneza mazingira ya kuzoeana na wenzao na kuingia kwenye mfumo wa timu”. Nae, Nahodha wa Dodoma Jiji FC, Augustin Nsata akaelezea hali ya kambi na maandalizi ya timu kuelekea kwenye michezo ...