CCM CHANG’OMBE YAMPONGEZA DIWANI FUNDIKILA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe kimempongeza Diwani wa kata hiyo Bakari Fundikila kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Chang’ombe. Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvi jijini Dodoma. Iddy alisema kuwa Kata ya Chang’ombe inapiga hatua ya maendeleo kwa kasi kutokana na Diwani wake kusimamia maendeleo. “Maendeleo haya tunayoyaona ni baada ya Diwani kusimama na kuizungumzia na kuitetea Chang’ombe. Mheshimiwa Diwani umekwenda kufanya harakati za namna gani wananchi wa Kata ya Chang’ombe wanaenda kupata huduma bora za kijamii. Leo tumekuwa na Kituo cha Afya Chang’ombe ambacho ni kituo cha mfano kwa ubora wa majengo, ukubwa wa eneo na huduma. Pale kuna jengo la mama na mtoto na huduma za upasuaji mdogo zitapelekwa” alisema Iddy. Diw...