Posts

Showing posts from February, 2026

Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa ujio wa Bandari Kavu Ihumwa

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula apongeza Mkakati wa Uendelezaji Bandari Kavu na kuahidi kujipanga kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanapata fursa ya kufanya biashara katika eneo hilo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla. Akizungumza katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye Bandari Kavu Ihumwa iliyokuwa na lengo la kujiridhisha na mkakati wa uendelezaji wa miundombinu hiyo, alisema kuwa uongozi wa jiji utakaa kikao na kutathmini namna ya kuandaa mazingira rafiki ya biashara ili kuwawezesha wajasiriamali wa ndani kushiriki kikamilifu katika shughuli za upokeaji, uhifadhi na usafirishaji wa mizigo. Alieleza kuwa pamoja na fursa za moja kwa moja zitakazotokana na shughuli za bandari hiyo, jiji pia linatarajia kuimarisha sekta ya usafirishaji, uhudumu na biashara ndogondogo hivyo kuongeza ajira na kipato kwa wananchi. Aidha, Mstahiki Meya Chaula aliongeza kuwa jiji litafanya utaratibu wa kufanya mazungumzo na Mam...

Shule ya Viziwi Dodoma yapokea msaada wa matendo ya huruma

Image
Na. Emanuel Charles, DODOMA Shule ya Viziwi Dodoma yakabidhiwa msaada wa mahitaji muhimu ya kijamii yenye thamani ya shilingi 2,00,000 ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyoandaliwa na Dodoma Jiji Day kwa lengo la kuhimiza upendo, ushirikiano na mshikamano. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma ambapo alikabidhi mchele, sukari, vifaa vya usafi na taulo za kike. Alisema kuwa ipo tha wabu ya utoaji na kuwajali watu wenye mahitaji maalum. “Kutoa siyo utajiri, ni moyo. Japokuwa tulichotoa kinaweza kuonekana kidogo kwa namna moja ama nyingine, lakini naamini kitaenda kuwasaidia watoto hawa, hasa katika kupata chakula shuleni na kuboresha mazingira yao ya kujifunzia” a lisema Alhaj Shekimweri . Aidha, aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mpango wake wa kuibadilisha shule hiyo kuwa ya mchanganyiko ili kuwaunganisha watoto wenye mahitaji maalumu ya usikivu na wale wasio na changamoto, ha...