Sekondari Zuzu yapongezwa na CCM Mkoa
Na. Dennis Gondwe, ZUZU KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imewashukuru walimu wa Shule ya Sekondari Zuzu kwa kazi ya ufundishaji na kusimamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu shuleni hapo. Shukrani hizo zilitolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Donald Mejiti alipoongoza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba nane na matundu 10 ya vyo Shule ya Sekondari Zuzu. Mejiti alisema “nianze kwa kutoa pongezi kwa kazi nzuri mliyofanya na inaonekana. Walimu wetu tunawashukuru sana kwa kazi ya kufundisha wanafunzi na kusimamia ujenzi wa miundombinu katika shule hii. Nia ya mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga majengo haya ni kuwawezesha watoto wetu wasome katika mazingira bora na salama. Watoto wetu wakisoma fursa za ajira zinakuwa nyingi. Lakini pia amejenga vyuo vya VETA ili kuongeza wigo kwa watoto wetu, bahati nzuri VETA ada yake ni nafuu sana”. Aidha, alimpongeza Mkurugenzi wa Halm...