RC Senyamule aagiza utengenezaji Viti uende sambamba na ujenzi wa madarasa Sekondari Mtumba
Na. Dennis Gondwe, MTUMBA MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza ujenzi wa madarasa uende sambamba ya utengenezaji wa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi ili vyote vikamilike pamoja na kuanza kutoa huduma. Kauli hiyo aliitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mtumba iliyopo Kata ya Mtumba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Baada ya kukagua hatua ya ujenzi wa miundombinu hiyo alihoji hatua ya utengenezaji wa viti na meza ambao ulikuwa haujaanza. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliagiza utaratibu wa kutengeneza viti na meza uanze ili uende sambamba ya ujenzi wa miundombinu hiyo na kukamilika pamoja ili isicheleweshe utoaji wa huduma. Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2024/2025 Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtumba, Mwl. Stephen Moshi alisema kuwa ujenzi unaendelea vizuri. “Shule ilipokea shilingi 201,000,000 tarehe 6 Ja...