Posts

Showing posts from March, 2025

Waziri Mavunde asisitiza miradi mikubwa ya madini iliyopewa leseni kuanza kazi haraka

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza miradi mikubwa na ya kati ya Madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa na kutimiza azma ya serikali kutoa leseni hizo. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde Aliyasema jijini Dodoma wakati akizungumza katika mkutano maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya Madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla. Waziri Mavunde alisema serikali inataka kuhakikisha kuwa miradi yote ya uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa sekta binafsi kuchukua hatua kwa upande wao. “Serikali imefanya kazi yake, tumeondoa vikwazo vingi na kurahisisha utaratibu. Sasa ni juku...

Shule shikizi Ipala, mkombozi kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu

Image
Na. John Masanja, IPALA Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa, aishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya elimu msingi katika kata hiyo kwa kujenga shule shikizi ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi wenye umri mdogo kupata elimu bora. Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Ipala kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Diwani Magawa alisema kuwa katika miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita, elimu katika Kata ya Ipala imekuwa kwa kasi. “Serikali yetu tukufu imetuletea elimu hadi kwenye kata yetu. Tuna shule shiziki mbili zimeanzishwa kwa lengo la kusaidia wanafunzi wadogo wanaotembea umbali mrefu karibu kilomita tano kufuata elimu. Sasa hivi uwepo wa madarasa haya matatu nafuu imekuwa kubwa sana kwa kuwapunguzia watoto wadogo kutembea umbari mrefu” ...

Nyumba ya mtumishi kuchangia huduma masaa 24 Zahanati ya Ipala

Image
Na. Nancy Kivuyo, IPALA Mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Ipala uliogharimu kiasi cha shilingi 55,000,000, umeleta maboresho katika utoaji wa huduma ya afya katika kata hiyo. Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Ipala Hayo yalielezwa na Muuguzi kutoka Zahanati ya Ipala, Tumain Sanga alipokuwa akiwaelezea waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika kata hiyo kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Alisema kuwa anatoa pongezi kwa serikali kuwajengea nyumba hiyo ili kurahisisha utoaji wa huduma za afya katika kata hiyo. “Tunaipongeza serikali kutujengea nyumba ya mtumishi, uwepo wa nyumba hii imeturahisishia kutendaji wa kazi mzuri. Laiti tungekuwa mbali tungeshindwa kuwahudumia wananchi vizuri na kwa wakati, lakini sasa wagonjwa wanaweza kuja muda wowote na wakatukuta na tukawahudumia kwa masaa 24. Tunaishukuru sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tuna...

Wananchi wa Mtaa wa Mwaja, Jiji la Dodoma washiriki kufanya usafi wa mazingira wa Jumamosi ya mwisho wa Mwezi, Machi, 2025

Image
Leo tarehe 29.03.2025, wananchi wa Mtaa wa Mwaja, Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki zoezi la usafi wa Mazingira wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa lengo la kuweza mazingira safi kwa ajili ya afya zao. Usafi huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwaja, Athumani Makuka ambaye aliambatana na Afisa Mtendaji wa Mtaa, Mwanaasha Mani. Zoezi hilo la usafi lilifanyika katika mtaro unaopita pembezoni mwa Shule ya Msingi Chinangali ambao umehusisha kuzibua mtaro wenye urefu wa mita 100 sambamba na kutoa taka ngumu kama makopo na mifuko kwenye mtaro huo ili kuruhusu maji yaliyotuwama kwa sababu ya mvua kutiririka pasina kizuizi chochote.

Ukarabati tanki la Maji Kata ya Ipala waleta neema kwa wananchi

Image
Na. John Masanja, IPALA Ukarabati mradi wa tanki la maji la Lita 90,000 katika Kata ya Ipala, waleta ahueni kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji kwa matumizi mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Ipala kuanzia mwaka 2021 hadi 2025, Diwani George Magawa aliishukuru serikali kwa kutoa fedha shilingi 43,406,300 kwaajili ya ukarabati wa tanki la mradi mkubwa wa Maji Ipala. “Wananchi sasa wanapata maji safi na salama. Kwahiyo, tunaishukuru serikali, tunamshukuru sana mbunge wetu na wataalam mbalimbali. Kata imechimba visima vinne kwaajili ya kupata maji safi na kupunguzia wananchi adha ya kutumia maji yasiyo salama. Hivi visima vinapunguza adha ya kwenda umbali mrefu kufuata maji ambayo mara nyingi siyo salama. Hivyo, wananchi wa kata yetu tatizo hili la uhaba wa maji limepungua sana” alisema Magawa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Hombo...

Mikopo ya 10% yawanufaisha vijana wa Kata ya Ipala

Image
Na. John Masanja, IPALA Halmashauri ya Jiji la Dodoma yakipatia kikundi cha Kazi iendelee Ipala mkopo usio na riba wa shilingi 17,000,000 kwa ajili ya kuongeza mtaji kwa shughuli ya bodaboda na kutengeneza ajira kwa vijana ili waweze kujitegemea kimaisha. Hayo yalielezwa na Mhasibu wa Kikundi cha Kazi iendelee, Peter Mhaka mbele ya waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika kata hiyo kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. “Kikundi kilipata mkopo huu ili kujikwamua kiuchumi. Mwaka 2023 tulichukua mkopo wa shilingi 17,000,000 tukiwa watano, tukanunua bodaboda tano ambazo zimetunufaisha kwa kusomesha watoto, tumejiingiza kwenye kilimo na tumepunguza utegemezi yote hii ili kujikwamua zaidi kiuchumi” alisema Mhaka. Aidha, aliiomba serikali kuendelea kuhamasisha vijana ili wafahamu umuhimu wa mikopo hiyo. “Nawashauri vijana wenzangu wachangamkie fursa ya mikopo hii isiyoumiza, watembelee ofisi za kata ili kupata elimu ya mikopo h...

Shule shikizi Ipala, mkombozi kwa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu

Image
Na. John Masanja, IPALA Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa, aishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya elimu msingi katika kata hiyo kwa kujenga shule shikizi ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi wenye umri mdogo kupata elimu bora. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Ipala kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Diwani Magawa alisema kuwa katika miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita, elimu katika Kata ya Ipala imekuwa kwa kasi. “Serikali yetu tukufu imetuletea elimu hadi kwenye kata yetu. Tuna shule shiziki mbili zimeanzishwa kwa lengo la kusaidia wanafunzi wadogo wanaotembea umbali mrefu karibu kilomita tano kufuata elimu. Sasa hivi uwepo wa madarasa haya matatu nafuu imekuwa kubwa sana kwa kuwapunguzia watoto wadogo kutembea umbari mrefu” alisema Magawa. Pia, aliongeza kuwa...

Zaidi ya Shilingi Bil 1 zaijenga Kata ya Matumbulu

Image
 

Shilingi Bil. 2.5 zaiboresha Kata ya Makole

Image
 

Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Kata ya Kikuyu Kaskazini katika Mtaa wa Kigamboni

Image
  #Afya yako, Mtaji wako. Zingatia unachokula

Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Mtaa wa Kawawa, Kata Matumbulu

Image
Na. Mwandishi Wetu, MATUMBULU Kata ya Matumbulu yaadhimisha Siku ya Afya na Lishe (SaLiKi) kwa mitaa ya Kawawa, Nyerere na Mwongozo. Lengo ni kutoa elimu ya lishe na malezi ili kuepuka udumavu na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa. #Afya yako, Mtaji wako. Zingatia unachokula 

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapitisha rasimu ya Sheria ndogo tano

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago amesema kuwa mchakato wa kuandaa Sheria ndogo za halmashauri yake ilizingatia miongozo inayoelekeza uandaaji wa sheria hizo kwa maslahi ya wananchi wa Dodoma. Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago, akifafanua jambo   Alitoa kauli hiyo katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia rasimu za Sheria ndogo za Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Naibu Meya Chibago alisema kuwa baraza lake limejiridhisha kuwa kila hatua imepitiwa vizuri ya mchakato wa kuandaa Sheria ndogo za halmashauri. Mchakato ulikuwa shirikishi na ulianzia hatua za mwanzo kwa mujibu wa miongozo. Kamati za Maendeleo za Kata hadi vikao vya juu vya halmashauri. “Tumejadiliana kwa kina na kuheshimu maoni ya kila mtu. Nawahakikishia kuwa yale tuliyojadili leo, vielelezo vyote vipo kwa mujibu wa miongozo kutokana na umakini wa baraza hili” alise...

Kata ya Makole

 

Mradi wa maji Matumbulu, wananchi wanafurahia kilimo cha umwagiliaji

Image
Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU Shilingi 360,746,830 zimetumika kuboresha tanki la maji la lita 90,000 na kuweza kuwahudumia wakazi wa mitaa ya Kata ya Matumbulu huduma ya maji kwa saa 24. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo la tanki hilo likiwa moja ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi sasa katika Kata ya Matumbulu, Mhasibu wa Maji, Colleta Kapinga alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya wakazi wa mitaa mitatu ya Nyerere, Mwongozo na Kawawa. “Maji haya yanapatikana masaa 24 na kuna baadhi ya watu wanayatumia kumwagilia kilimo cha mbogamboga. Huduma hii imemtua mama ndoo kichwani. Kwahiyo, ni msaada mkubwa kwa wananchi” alisema Kapinga.   Nae Afisa Kilimo Kata ya Matumbulu, Aneth Mnana alisema kuwa upatikanaji wa maji umewashawishi wananchi kushiriki kilimo cha muda mfupi kama mbogamboga ili kujihakikishia mahitaji ya vyakula muhimu. “Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha...

Kilimo cha Zabibu ni ajira kwa vijana kujikwamua kiuchumi

Image
Na. Nancy Kivuyo,   MATUMBULU Vijana wa Kata ya Matumbulu wameendelea kunufaika na fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuweza kujikwamua kiuchumi.   Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kikundi cha Kaunda kinachojishughulisha na kilimo cha zabibu, Isack Benjamin alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliofanya media tour kufuatilia wanufaika wa mikopo hiyo katika kata ya matumbulu.   Benjamin alisema kuwa mikopo ya asilimia nne inayotolewa na   halmashauri imekua mkombozi kwa vijana wanaopenda kujishughulisha na kuingiza kipato ili kuboresha maisha yao. “Kikundi chetu kilipata mkopo wa shilingi milioni 20, ambapo tupo vijana watano. Tuliwekeza kwenye kilimo cha zabibu kwasababu tuna maeneo makubwa huku na kilimo cha zabibu kinakubali sana. Kiukweli, faida tuliiona, tunasomesha watoto, tunapata mahitaji muhimu na kubwa zaidi tumeweza kuongeza tena ekari tano ...

Kikundi cha Kilasara chanufaika mkopo wa halmashauri

Image
Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU MIKOPO isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu imekuwa chachu ya kusukuma maendeleo katika sekta za kilimo, ufugaji na ujasiriamali.   Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kikundi hicho kufuatilia manufaa ya mikopo hiyo kwa jamii, Mwenyekiti wa Kikundi cha Kilasara, Judika Urio alisema kuwa wanawake hao wamenufaika na mkopo huo usio na riba. “Kikundi chetu tupo watano, tulipata takribani shilingi milioni 20 ambazo tuliwekeza katika ufugaji wa kuku, bata mzinga, bata bukini na sungura. Baada ya mafanikio ya ufugaji huo, tulipata faida ambayo ilituwezesha kuanzisha mradi mwingine wa uzalishaji wa samaki kama mnavyoona kwenye mabwawa haya, tumeweka mbegu ya samaki wapatao elfu 10 ambao tunategemea baada ya mwaka ndio tuvune” alisema Urio.   Alimshukuru Rais, kwa kuyajali makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, na kusema kuwa amewainua ...