Mradi wa maji Matumbulu, wananchi wanafurahia kilimo cha umwagiliaji
Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU
Shilingi
360,746,830 zimetumika kuboresha tanki la maji la lita 90,000 na kuweza
kuwahudumia wakazi wa mitaa ya Kata ya Matumbulu huduma ya maji kwa saa 24.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo la tanki hilo likiwa moja ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi sasa katika Kata ya Matumbulu, Mhasibu wa Maji, Colleta Kapinga alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya wakazi wa mitaa mitatu ya Nyerere, Mwongozo na Kawawa. “Maji haya yanapatikana masaa 24 na kuna baadhi ya watu wanayatumia kumwagilia kilimo cha mbogamboga. Huduma hii imemtua mama ndoo kichwani. Kwahiyo, ni msaada mkubwa kwa wananchi” alisema Kapinga.
Nae
Afisa Kilimo Kata ya Matumbulu, Aneth Mnana alisema kuwa upatikanaji wa maji
umewashawishi wananchi kushiriki kilimo cha muda mfupi kama mbogamboga ili
kujihakikishia mahitaji ya vyakula muhimu. “Tunaishukuru serikali inayoongozwa
na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huu mradi wa maji kwasababu ni
mkombozi wa kilimo na unafanya kazi yetu sisi wataalam kufanyika vizuri
kwasababu elimu ya vitendo inafanyika katika kuiboresha sekta ya kilimo cha
kisasa” alisema Mnana.
Kwa
upande mwingine mkulima wa Alizeti, Mussa Mlilima, aliishukuru serikali kwa
kuwawekea mradi wa maji wenye tija na unaokidhi mahitaji. “Tunaishukuru sana
serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru pia
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde na Diwani wa Kata yetu, Emmanuel
Chibago kwa maendeleo wanayotuletea, tunawaombea kheri na afya njema ili
waendelee kuchagua miradi mingine ya kugusa wananchi moja kwa moja ili
kuzidisha maendeleo katika kata yetu” alishukuru Mlilima.
MWISHO
Comments
Post a Comment