Posts

Showing posts from September, 2023

KATA YA CHAMWINO YATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE

Image
  Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino imetakiwa kusimamia utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa mujibu wa maelekezo ya serikali ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Chamwino, Jumanne Ngede aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Mtaa wa Mailimbili aliyofanyika katika mtaa wa Mailimbili. Ngede alisema kuwa ni jambo zuri kwa wataalam na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino kusimamia suala la Lishe kutokana na umuhimu wake katika jamii. Alisema kuwa kutokana na umuhimu wake, serikali ilisaini mkataba wa Lishe na makundi mbalimbali ili watekeleze mkataba huo kwa kuhakikisha elimu ya Lishe inatolewa na utekelezaji wa mkataba huo. Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa suala la utekelezaji wa mkataba wa Lishe ni maelekezo ya serikali yanayotakiwa kutekelezwa kwa uzito mkubwa. “Tumeshasaini mkataba wa Lishe, utakumbuka Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Has...

WAKAZI WA KATA YA NALA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIGA KURA KABLA YA SAA 10 JIONI

Image
  Na. Theresia Nkwanga, NALA MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo amewataka wakazi wa Kata ya Nala kujitokeza na kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura kumchagua mwakilishi wao. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo akimsikiliza mpiga kura katika moja ya kituo cha kupigia kura Kata ya Nala Kayombo alisema hayo katika kituo cha Sengu chini apokuwa akitoa muhtasari wa hali ya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala unaoendelea katika vituo 12 vya kata hiyo. “ Leo tarehe 19 Septemba, 2023 Kata ya Nala inafanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Diwani aliyefariki. Zoezi la kufungua vituo lilifanyika kama sheria inavyotaka saa 1:00 asubuhi. Mpaka sasa saa 6 mchana zoezi la upigaji wa kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kuchagua mwakilishi wao. Niwaombe wananchi waendelee kujitokeza muda bado sasa ni saa 6 mchana hadi saa 10 jioni ndio tunafunga vituo” alisema Kayombo. Aidha, aliwataka wananchi wa...

JIJI LA DODOMA LAPELEKA MIL. 20,000,000 KUMALIZIA MAABARA

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepeleka shilingi 20,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la maabara katika Shule ya Sekondari Wella iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo katika hafla fupi ya kupokea vifaa vya maabara vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini. Kayombo alisema “Mheshimiwa mbunge hapa tayari unaona ujenzi unaendelea kwenye maabara yetu kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, na sisi hatuwezi kukuangusha kwa sababu tunafanya kazi kwa kushirikiana. Tumeshaleta shilingi 20,000,000 hapa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na inaenda kumaliziwa. Tunataka wanafunzi wetu waweze kufanya majaribio ya sayansi kwa vitendo. Mheshimiwa mbunge kwa maelekezo yako ya juzi ulituelekeza tutafute fedha na tumeshapata shilingi 8,000,000 kwa ajili ya kukamilisha matundu saba ya vyoo. Miongoni mwa changamoto am...

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI VIFAA VYA MAABARA VYA SH. 9,000,000/=

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI ELIMU ndiyo mkombozi kwa vijana wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuwasaidia kutoa mchango katika maisha yao na maendeleo ya taifa la Tanzania. Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akiongea na mamia ya walimu, wanafunzi na wananchi waliojitokeza katika hafla ya kugawa vifaa vya Maabara  Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akiongea na wanafunzi na walimu wa shule za sekondari katika hafla ya kugawa vifaa vya maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi tukio lililofanyika Shule ya Sekondari Wella iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini. Mavunde ambae pia ni Waziri wa Madini alisema “elimu ninaamini kwamba ndiyo mkombozi wa kweli kwa vijana wetu na elimu hii itawasaidia kwenda kuwafanya wakatoe mchango wao na kulitumikia taifa la Tanzania na wao pia katika maisha yao. Baada ya kubaini tunachangamoto katika maabara zetu nyingi za vifaa, nikasema nianze na awamu ya kwanza na hii haitakuwa mwis...

MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO KATA YA NALA YAKAMILIKA

Na. Dennis Gondwe, Dodoma WANANCHI wa Kata ya Nala wametakiwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kujitokeza kwa wingi kumchagua Diwani ili awawakilishe na kutetea maslahi yao. Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo alipotembelea na kukagua vituo vya kupigia kura katika Kata ya Nala. Kayombo alisema “maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata ya Nala yamekamilika. Jumla ya vyama 11 vilichukua na kurejesha fomu na kupata nafasi ya uteuzi wa kugombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Nala. Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo mimi ndiyo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma mjini na Kata ya Nala tumejiandaa vizuri na hatuna mapungufu yoyote”. Alisema kuwa jumla ya wapiga kura wanaopaswa kupiga kura ni 3,741.  “Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi ili kutumiza haki yao ya msingi kumchagua mwakilishi wao ambae ni Diwani wa Kata ya Nala” alisema Kayombo. Kata ya Nala inafanya uchaguzi mdogo kufuatilia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kat...

KATA YA CHAMWINO YAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI

Image
  Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino yaadhimisha maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo. Akiongelea maadhimisho hayo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya usafi wa mazingira katika barabara inayotoka makutano ya Wajenzi mpaka kona ya Viva la vida. Alisema kuwa usafi huo ulihusisha kusafisha mtaro wenye urefu wa mita 1,500. “U safi wa mazingira pia ulifanyika katika mitaro yote inayozunguka Shule ya Sekondari ya Hijra na wananchi walijitokeza na kufanya usafi katika korongo karibu na uwanja wa Shell Complex. Zaidi ya kusafisha mitaro, usafi huo ulihusisha kutoa taka ngumu na kuokota makopo na mifuko kwenye mtaro na maeneo ya pembezoni mwa barabara na korongo” alisema Nkelege . Akiongelea mafanikio ya maadhimisho Siku ya Usafi Duniani, alisema kuwa yametokana na ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali. “Napenda kutoa shukurani ...

CHANG’OMBE WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA KUZUIA WAHALIFU

Image
Na. Dennis Gondwe, WAKAZI wa Kata ya Chang’ombe wametakiwa kudumisha usafi wa mazingira kwa lengo la kuzuia maficho ya wahalifu na kulinda afya zao ili waweze kufanya shughuli za kujitelea maendeleo. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe, Tunu Dachi alipoongoza uzinduzi wa kampenzi ya usafi wa mazimgira katika kata hiyo tukio lililofanyika katika Mtaa wa Mazengo jijini Dodoma. Dachi alisema “nilipofika Kata ya Chang’ombe niligundua kuwa kata yetu ni chafu sana. Na katika kufanya vikao na wadau wa usafi wa mazingira tulikubaliana kuwa Mtaa wa Mazengo ndio mtaa mchafu kuliko mitaa yote. Leo nataka tushirikishane jambo rahisi sana, vikundi vya uzoaji taka vimeridhia kwamba kila Jumamosi wataungana kwa umoja wao na jamii ya mtaa husika kuja kufanya usafi wa maeneo ambayo mwenyekiti atakuwa amependekeza”. Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mazoezi ya usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi. “Kwa hiyo, mwananchi akisema anaenda kumfanyia ...

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini, John Kayombo akiwaapisha wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kwa uchaguzi wa Diwani Kata ya Nala

Image
 

WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGIZI NDOGO WA DIWANI KATA YA NALA WAASWA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WASIMAMIZI wa vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala wametakiwa kufanya kazi kwa nidhami, hekima na uzalendo na kuepuka kuisababishia serikali hasara. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo akiwaapisha wasimamizi wa vituo vya uchaguzi mdogo Kata ya Nala Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi kwenye vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala, Jimbo la Dodoma mjini yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma. Kayombo ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “niwaombe sana wasimamizi wa vituo, uchaguzi ni suala nyeti sana sikiliza kwa makini maelekezo ya viongozi na fuata taratibu na sheria zilizopo, ukikosea utaitia serikali katika hasara kubwa. Kuweni na nidhamu, hekima na uzalendo kwa kiwango cha juu sana. Baadhi yenu mlishasimamia chaguzi nyingi ila uchaguzi hauhitaji mazoe...

MAKARANI UCHAGUZI MDOGO KATA YA NALA WAHIMIZWA UADILIFU

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MAKARANI wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Nala, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu ili kufanikisha uchaguzi huo. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo alipokuwa akifungua mafunzo kwa makarani wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Nala yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “ninyi makarani tumewaamini, tumewapa ridhaa muende mkafanye kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa kabisa. Wakati tunawachagua tuliangalia sifa zenu, mliomba wengi. Mheshimiwa Jaji waliomba watu 1,500 lakini kupata hawa 12 ni mchakato ambao tumeufanya usiku na mchana mpaka kupata hawa 12 na wa akiba wawili. Siyo kwamba wale wengine hawana sifa hapana. Sifa moja wapo lazima awe raia wa Taznania, awe ...

KAMATI YA UJENZI, MANUNUZI NA MAPOKEZI JIJI LA DODOMA ZATAKIWA KUWA NA WATAALAM

Image
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo ameagiza kamati zinazohusika na ujenzi, manunuzi na mapokezi ya vifaa kuwa na wataalam wa fani husika ili kwenda sawa na matakwa ya mwongozo wa matumizi ya ‘force account’ katika kutekeleza miradi ya ujenzi. Agizo hilo alilitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Miyuji inayojengwa katika Kata ya Miyuji jijini Dodoma. Kayombo alisema kuwa mwongozo wa matumizi ya ‘force account’ unaelekeza ziundwe kamati zenye mchanganyiko wa wajumbe na wataalam. Kamati hizo ni ujenzi, manunuzi na mapokezi ya vifaa. “Katibu wa Kamati ya Manunuzi lazima awe mtaalam wa Manunuzi. Lengo ni kuwaongoza wajumbe kwenye taratibu za Manunuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. Kamati ya Ujenzi katibu wake anatakiwa kuwa Mhandisi na Kamati ya Mapokezi inatakiwa kuwa na mtu mwenye ujuzi wa mapokezi na utunzaji wa vifaa. Hivyo, maelekezo yangu wataalam hao waingizwe kwenye kamati ili kam...