Posts

Showing posts from July, 2025

JIJI LA DODOMA LATOA HERI YA SABASABA

Image
 

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

Image
  Lugha ya kiswahili na utamaduni wa mtanzania vimeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali wa kimataifa waliotembelea banda la Tanzania katika Wiki ya utamaduni na Kiswahili inayoendelea kwenye maonesho ya biashara ya dunia (Expo 2025) yanayofanyika Osaka, Japan. Kuelekea maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani yanayofanyika kila ifikapo tarehe 7 Julai lugha ya Kiswahili inaendelea kuwafikia watu wengi duniani na mwaka huu 2025 maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kiswahili kwa amani na mshikamano”. Viongozi waandamizi wa mataifa mbalimbali, wametembelea banda hilo ikiwemo Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Japani, Bw. Koichiro Gemba, Mfalme wa Lesotho, Mhe. Letsie III na Mhe. Prudence Sebahizi, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda. Viongozi hao wameonesha kuvutiwa kwa kiasi kikubwa na lugha ya Kiswahili na Utamaduni kupata nafasi katika Maonesho hayo ya Dunia yenye hadhi kubwa. Akizungumza wakati alipotembelea banda hilo Mhe. Sebahizi alie...

MAGEUZI YA ELIMU TANZANIA YAVUTIA NCHI NYINGINE KUJIFUNZA

Image
Mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu nchini, hususan mafunzo ya Amali yameanza kuvutia mataifa mengine barani Afrika kuja kujifunza namna yalivyofanyika na utekelezaji wake. Hayo yalibainishwa jijini Dodoma kufuatia ziara ya Waziri wa Elimu ya Juu, Utafiti, Sayansi na Teknolojia kutoka Jamhuri ya Gambia, Prof. Pierre Gomez ambaye alisema kuwa lengo la kufika Tanzania ni kujifunza mbinu zilizotumika katika kufanya maboresho na maugezi makubwa katika sekta ya elimu. Waziri huyo alisema kuwa Benki ya Dunia iliishauri nchi hiyo kuja Tanzania ili kujionea namna utekelezaji wa Sera, mikakati na miradi mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuwawezesha kutekeleza miradi yao kwa ufanisi na tija. “Tumeshuhudia ujenzi wa miundombinu na mifumo ya mafunzo ya vitendo yenye tija katika vyuo mbalimbali ikiwemo DIT, VETA na Taasisi, tunaamini kunufaika zaidi kupitia ushikiano katika nyanja mbalimbali za mafunzo” alisema Prof. Gomez. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzan...

DKT. BITEKO ASEMA TANZANIA INA USALAMA WA CHAKULA, AWAPONGEZA WAKULIMA

Image
* Asema Serikali inatambua Vyama vya Ushirika ni muhimu kuunganisha nguvu za wananchi na kujiendeleza kiuchumi * Mauzo ya nje ya kahawa na tumbaku 2023/2024 yaongezeka hadi Dola za Marekani 19,300,000 * Maono ya Rais Samia yaanza kuonekana sekta ya kilimo yachangia GDP asilimia 26 * Aziagiza Wizara za Fedha na Kilimo kupata ufumbuzi wa bei za mazao   Na. Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewapongeza wakulima nchini kwa jitihada zao za kuzalisha mazao kwa wingi na hivyo kusaidia nchi kuwa na usalama wa chakula ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.  Dkt. Biteko alitoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani. “Leo sekta ya kilimo ina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunazungumza mchango wa GDP wa asilimia 26, tunazungumza mazao ambayo yanatupa usalama wa ch...

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA UPADIRISHO JIMBO KATOLIKI DODOMA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki kushiriki katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma.  Misa hiyo Takatifu imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya.  Askofu Kinyaiya aliwasisitiza waumini kujitokeza katika kupiga kura kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu watakaowatumikia kwa miaka mitano ijayo. Pia ametoa rai ya matumizi sahihi ya akili mnemba (AI) ili kuepusha maovu na udanganyifu katika jamii. Jumla ya Mashemasi watatu wamepata daraja la Upadre katika Misa hiyo ambao ni Padre Joseph Ibrahim, Padre Sajilo Mark pamoja Padre Damian Mtanduzi. Aidha, Misa hiyo imeambatana na uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa jengo la ...

TANESCO SACCOS YAIGUSA SEKTA YA AFYA KWA KUTOA MASHUKA YENYE THAMANI YA MILIONI 23 JIJINI DODOMA

Image
Na. Janeth Raphael, MichuziTv -Dodoma  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema pamoja serikali kufanya kazi kubwa hasa katika Sekta ya Afya ikiwemo ununuzi wa vifaa, Dawa, Majengo na miundombinu na watumishi lakini bado safari ya maendeleo katika sekta hiyo huwa haiishi kutokana na watu kuongezeka na magonjwa kubadilika. RC Senyamule alisema hayo jijini Dodoma katika hafla fupi ya kupokea Mashuka 300 ya kuhudumia wagonjwa waliopo katika hospitali za Mkoa wa Dodoma yaliyotolewa na wana Ushirika wa Tanesco Saccos.  Alisema kuwa kutoka na uhitaji wa kila siku serikali hata kama ingenunua mashuka mengi kiasi gani bado yasingeweza kudumu siku zote kwasababu ingefika muda yangechakaa na kuhitajika mengine. “Tunajua kuwa serikali yetu chini ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia imefanya kazi kubwa sana katika Sekta ya Afya. Zipo sekta nyingine lakini katika sekta ya Afya imefanya makubwa kuanzia Vifaa,Majengo,Miundombinu,Watumishi na vitu vingine vingi, lakini tunafahamu ...

MAWAKILI NCHINI WATAKIWA KWENDA KUZISOMA SHERIA ZA UCHAGUZI MKUU

Image
Na. Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Mawakili nchini Tanzania wametakiwa kwenda kuzisoma sheria za Uchaguzi Mkuu, ili waweze kuwasaidia kujaza fomu wagombea waliojitokeza kutia nia, lakini pia kutatua migogoro itakayowasilishwa kwa kukosa uelewa katika Mahakama mbalimbali hapa nchini. Jaji Mkuu wa Tanzania ,George Masaju aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akiwathibitisha na kuwapokea Mawakili 449 wakiwemo wa Serikali na wa kujitegemea, ikiwemo kuorodheshwa rasmi katika orodha ya mawakili waliothibitishwa hapa nchini. Aidha, aliwataka Mawakili hao kwenda kufanya kazi katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam na Dodoma ambayo ina mawakili wa kutosha, ili kuepuka kuitwa vishoka hasa ukizingatia soko la Kada hiyo ni kubwa kwa sasa. Alisema kuwa kuna sheria nyingi zikiwemo za Polisi, Uchaguzi na nyingine. Na kusema kuwa Mawakili wanapaswa kutumia muda mwingi kuzisoma na kuzielewa ili waweze kutumia fursa ya kuwasaidia wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea na...

RAIS SAMIA ANAPENDA KUFANYA KAZI NA VIONGOZI WA DINI - DKT. BITEKO

Image
  📌 Asisitiza milango ya Rais Samia ipo wazi kwa ajili ya mazungumzo kwa mustakabali wa Taifa 📌 Asema Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Taasisi za dini 📌 Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini kuchochea maendeleo 📌 Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano – Baba Askofu Shoo 📌 CCT yahimiza maadili ya kisiasa, utulivu wa jamii na kampeni za kistaarabu 📌 Taasisi za dini Afrika zatajwa kuchangia maendeleo ya sekta ya afya kwa 30%- 70% Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile. Dkt. Biteko aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akimwakilisha  Rais, Dkt. Samia Su...