DC Shekimweri awataka wazazi kuwa karibu na watoto wao

Na. Arafa Waziri, DODOMA MAKULU Mkuu wa Wilaya wa Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri aliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya kikatili ili wawe katika mazingira salama. Mkuu wa Wilaya wa Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri akiongea na walimu na wazazi Aliyasema hayo wakati alipotembelea Shule ya Msingi Kisasa na kuongea na walimu na wazazi shuleni juu ya masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia na uelimu kwa ujumla. Alhaj Shekimweri alisema kuwa ukatili wa kijinsia hutokea katika familia kutokana na kuaminiana sana baina ya wanafamilia. “Upo ukatili wa kijinsia, tafiti zinaonesha ukatili wa kijinsia kwa watoto asilimia kubwa wanafanyiwa na ndugu wa karibu Dunia imebadilika sana hivyo, nawasisitiza hatuna budi kuchukua tahadhari katika kuwaangalia watoto kwa karibu’’ alisema Shekimweri. Alisema kuwa ni vema wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa kuangalia watu wanaokutana na kuhusiana nao ili kubaini kama wanafaa kumjenga mtoto h...