Posts

Showing posts from 2024

Usafi mwisho wa Mwezi waendelea Kata ya Mnadani

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Wananchi wa Kata ya Mnadani Halmashauri ya Jiji la Dodoma walifanya usafi wa mazingira mita tano kuzunguka maeneo yao ya makazi na biashara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la usafi, Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka ngumu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, alisema kuwa ni wajibu wa viongozi kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kufanya kazi kwa pamoja na wananchi. Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na utupaji wa taka ovyo katika maeneo na kufanya usafi katika mitaro ambayo inapitisha maji machafu kipindi hiki cha mvua nyingi na kujiepusha na mafuriko yatokanayo na uzibaji wa mitaro. “Usafi ni ustaarabu ambao unaanza na mimi na wewe. Lakini katika kipindi hiki cha masika, kumekuwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali ya kuhara na kutapika ambayo tunaweza kujiepusha kwa kufanya usafi kwenye maeneo yetu” alisema Kimaro...

Madiwani wadaiwa uthubutu kufanya maamuzi ya kimaendeleo

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, wametakiwa kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi ya kimaendeleo ili kuwanufaisha wananchi wanaowasimamia. Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alipokuwa akiwakaribisha madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mstahiki Meya, Prof. Davis Mwamfupe akifafanua jambo “Kikubwa katika mtakachokiona, sio utajiri wetu wa pesa ni uthubutu wa kufanya maamuzi, unaweza kuwa na pesa lakini hauna uthubutu wa kuzitumia, ukipewa shilingi milioni moja, utapata wasiwasi kuzitumia kwasababu zitaisha, hutakubali matumizi ya laki mbili au tatu. Lakini sisi hatuogopi, kama tuna mradi wa hoteli iliyopo hapa ambayo imegharimu shilingi Bilioni 12, hatuogopi mradi wa Soko la wazi la Machinga, ingawa serikali ilituchangia shilingi Bilioni tatu, na sisi tukaweka shilingi bilioni sita nyingine. Hatuogopi kwamb...

Wataalam watumike kukuza mapato ya ndani

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetakiwa kuwajengea uwezo wa kimbinu na kuwatumia wataalam wa ndani ili kuongeza mapato ya ndani sambamba na kubuni miradi ya kimkakati yenye tija kwa maendeleo ya nchi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua jambo kwa mfano Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, waliotembelea Dodoma kwa lengo la kujifunza na kuongeza wigo wa namna sahihi ya kuongeza mapato ya ndani kupitia miradi mbalimbali, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Hakuna mapato madogo na hakuna mradi mdogo, ila tunapoandaa miradi, tujiulize tunaandaa miradi yenye mfumo gani?. Kwahiyo, tunavyofikiri miradi, hata yenye mtazamo wa kibiashara lazima tufikirie kwenye kukua kwake. Hivyo, kila kitu kinaweza kikaanza kwenye udogo, kikakua na mapato yaleyale madogo tunaweza tukaanzisha miradi kwa mapato ya ndani. Nilicho...

Wananchi watakiwa kuwa msitari wa mbele kupinga ukatili

Na. Coletha Charles, CHAMWINO Wakazi wa Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma walipewa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na malezi bora ambayo imetolewa katika Ofisi ya Afisa Mtaa wa Mwaja kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua yanayoendelea kwenye jamii.   Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Mratibu wa Jinsia na Watoto, Fatuma Kitojo amewataka wazazi hao kuwa walezi bora kwa watoto wao na kutowatamkia maneno mabaya ambayo yanawakatili kisaikolojia ili wakubalike na jamii inayo wazunguka. Kitojo alisema kuwa ni muhimu kwa wazazi kuelewa kwamba maneno wanayosema yanaweza kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya watoto kihisia, kujitambua, na uhusiano mzuri na Watoto wengine. “Watoto wetu wanatupenda sana na wanapenda kuona sisi tunafanikiwa ni kweli tuna shughuli nyingi tunakimbizana na muda na maisha kwa sababu za hali za kiuchumi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. lakini tunajua kwa asili mwanamke ndiyo mlezi namba moja. Kwahiyo tunatakiwa tutenge mda wa ...

RC Senyamule azipongeza Club za Jogging Dodoma

Image
Na. John Masanja   Vikundi vya 'Jogging C lub s ' Mkoa wa Dodoma vimepongezwa kwa kuendelea kuwa na mshikamano na kuwa vinara wa kuhamasisha watu kufanya mazoezi kwa kuboresha afya zao na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kuelimisha jamii kupitia kampeni mbalimbali.    Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule baada ya kumalizika kwa mazoezi na mbio fupi zilizofanyika kwa kuratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma k wa kushirikiana na “ Friends of Mavunde ” na “ Dodoma City L egends Family” .    “ Katika makundi tuliyonayo kwa mkoa wetu hivi vilabu vya Jogging wamekuwa kinara wa kuimarisha m shikamano wao wenyewe na wafuasi sisi tunaoungana nao kufanya mazoezi, ni makundi ambayo hayana uvivu wa kufuatilia jambo lao wakiamua nawapongeza sana.    " Kupitia mchango wao wa kuhamasisha unatupa sisi fursa ya kufikisha ujumbee mbalimbali . Kwa jamii, jambo kubwa nimefurahi leo k wa sababu mazoezi haya...

Bonanza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali jijini Dodoma 2024 lafana

Image
Na. John Masanja, DODOMA   Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Neema Kilongola ambaye ni Afisa Michezo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ameshiriki katika Bonanza la kufunga m waka la m ashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) Mkoa wa Dodoma.   Aidha , bonanza hilo lenye kaulimbiu isemayo "Mazoezi ni Tiba" limefanyika katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Jamhuri na kuhudhuriwa na wanamichezo na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma. Akizungumza na wanamichezo hao, Kilongola alisema kuwa matokeo yanayotegemewa kutokana na bonanza hil o ni ongezeko la aina ya michezo na ushiriki wa jamii katika michezo, ongezeko la uelewa wa jamii na mabadiliko ya tabia juu ya ufanyaji wa mazoezi pamoja na ushuhuda wa watu juu ya kupungua kwa maumivu ya mwili na uzito. Alitoa rai kwa mashirikia yasiyo ya k iserikali kuanzisha uchangiaji wa jamii na wadau ili kuwapa motisha walimu na wataalamu wa afya na manunuzi ya vifaa vya michezo. "Niwasha...

Bonanza la kufunga Mwaka la Mashirika yasiyo ya kiserikali lafanyika Dodoma

Image
 

Mbunge Mavunde akila chakula pamoja na watoto kwenye Kituo cha Malezi QADIRIA

Image
 

Mbunge Mavunde akifanyiwa Dua

Image
 

Mbunge Mavunde akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa QADIRIA Orphan Centre

Image
 

RC Senyamule azindua Kampeni ya changia Damu jijini Dodoma

Image
 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma kwenye "Rudisha Tabasamu kwao Jogging"

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule mwenye kofia ya kimkakati katikati akiongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma kwenye "Rudisha Tabasamu kwao Jogging"

RC Senyamule akiongea na mamia ya wakazi wa Dodoma walioshiriki Jogging "Rudisha Tabasamu kwao" Chinangali Park

Image
 

Watoto kulindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani Dodoma

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Rachel Balisidya amewataka wazazi kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha wanaweza kutimiza ndoto na malengo yao kwa kuzuia madhara yanayoweza kuwaharibia maisha kisaikolojia. Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma ambae ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Rachel Balisidya akihutubia katika Tamasha la (TASHMEKU) Wito huo aliutoa leo alipomuwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma kwenye Tamasha la Tanzania Shiriki Malezi Endelevu Kupinga Ukatili (TASHMEKU) katika Shule ya Sekondari Dodoma Makulu kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto. Balisidya alisema kuwa Wilaya ya Dodoma bila ukatili inawezekana. Alisema kuwa ipo changamoto ya ukatili kwa watoto na asilimia kubwa ya ukatili inaanzia nyumbani kupitia baba, mama, mjomba, mwalimu na wale wanaowazunguka na kuwaharibu watoto kisaikolojia kwa kuwatesa, kubakwa na kuwanyim...

Wasimamizi miradi Jiji la Dodoma watakiwa kuwa wazalendo

  Na. Faraja Mbise, DODOMA Wasimamizi wa miradi ya ujenzi katika Shule ya Sekondari Matumbulu wametakiwa kuwa wazalendo na kutokwamisha juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.    Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Matumbulu iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Matamanio ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuleta hizi shule ni kwasababu watoto wasitembee umbali mrefu. Bado sisi Mkoa wa Dodoma tuna utoro na baadhi ya changamoto inayochangia utoro ni watoto kutembea mwendo mrefu kwenda shule. Kwahiyo, anaona fahari asiende shuleni. Lakini tuna ukatili wa kijinsia, kati ya maeneo ambayo watoto wanafanyiwa ukatili ni akiwa anaenda shuleni, wanapita maporini kwasababu ya umbali mrefu, yote haya Rais ametaka ayamalize kwa kuwajengea shule karibu na eneo lao” alisema Senyamule. Kwa upande wak...

Viwanja vya Kikombo Vinauzwa rasmi

Image
 

Mamia wajitokeza Kilele Siku 16 za Kupinga Ukatili Jiji la Dodoma

Image
 

RC Senyamule ahitimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili Dodoma

Image
 

Miaka 63 ya Uhuru, watanzania waaswa kutunza na kuthamini Uhuru

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Watanzania wameaswa kutunza na kuthamini uhuru kwa kufanya mambo yanayoleta amani na usalama wa nchi, ili kufurahia matunda ya uhuru yaliyopatikana ndani ya miaka 63 tangu tarehe 09 Desemba, 1961. Hayo, yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya M iaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika makutano ya Barabara ya Mzunguko (Ring Road) katika Kata ya Makutupora, jijini Dodoma. Senyamule alisema “ i li uhuru huu tuendelee kuufurahia na kuuenzi, kwanza tuhimize amani na usalama wa nchi yetu kwasababu ni msingi wa mafanikio. Huu uhuru tunausherekea kwasababu bado tunaulinda, usije ukafikiri ukipata uhuru ndio imeisha, unaweza ukapata uhuru na baadae ukapotea tena kwasababu unaweza ukaingiliwa. Tuendelee kutunza kwa kufanya mambo ya amani na utulivu” Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika Mi aka 63 ya Uhuru, aligusia mafanikio mbalimbali k...