RC Senyamule azipongeza Club za Jogging Dodoma
Na. John Masanja
Vikundi vya 'Jogging Clubs' Mkoa wa Dodoma vimepongezwa kwa kuendelea kuwa na mshikamano na kuwa
vinara wa kuhamasisha watu kufanya mazoezi kwa kuboresha afya zao na kuepukana
na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kuelimisha jamii kupitia kampeni
mbalimbali.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule
baada ya kumalizika kwa mazoezi na mbio fupi zilizofanyika kwa kuratibiwa na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na “Friends
of Mavunde” na “Dodoma City Legends Family”.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Gwamaka Mlagila alisema “michezo ni afya na kutoa damu ni upendo na hakuna michezo bila upendo. Kwahiyo, niwahamasishe mjitokeze kwa wingi kuchangia damu ili ziwasaidie wagonjwa wanaohitaji damu”.
Vikundi vya "Dodoma City Legends Family na kikundi Cha Friends of Mavunde’' wametumia siku hii kufanya uzinduzi rasmi wa vikundi vyao na watashiriki mambo mbalimbali ya kurudisha furaha kwa jamii kwa kuwatembelea watoto yatima na kuchangia damu zitakazookoa maisha ya wengine. “Vikundi hivyo, vinafanya matendo hayo ya huruma kupitia kaulimbiu "Rejesha Tabasamu Kwao".
Akiwasikisha salamu za Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo na kuwataka wananchi waendelee kudumisha mazoezi ya mara kwa mara kwa ustawi wa afya za kula mmoja.
Zoezi la Jogging limeanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hadi katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma likikamilisha idadi ya kilometa 5 Kwa wakiambiaji na washiriki.
Comments
Post a Comment