Posts

Showing posts from November, 2023

JIJI LA DODOMA KINARA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeibuka kinara katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 iliibuka nafasi ya kwanza kimkoa, kikanda na nafasi ya pili kitaifa. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto) akikabidhi cheti cha mshindi wa kwanza wa Mwenge wa Uhuru ngazi ya Mkoa na Kanda Jiji la Dodoma Taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu matokeo ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 katika kikao cha mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya na watendaji katika mkoa na halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Senyamule alisema kuwa mwaka 2023 Mkoa wa Dodoma ulikuwa mkoa wa 30 kabla ya mkoa wa kilele kukimbiza Mwenge wa Uhuru. “Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wanakuwa na vigezo wanavyoangalia hasa wanaangalia fedha zilizoletwa zimetumikaje, ubora wa miradi iliyoletewa fedha na Mheshimiwa Rais imesimamiwaje kwa tija na ufanisi kiasi gani...

KAMATI YA SIASA KATA YA MSALATO YATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI

Image
  Na. Dennis Gondwe, MSALATO KAMATI ya Siasa ya Kata ya Msalato imetakiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ili kujiridhisha ya thamani ya fedha. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba alipoongoza Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma kutembelea na kukagua ujenzi wa mabweni mawili, vyumba saba vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Kata ya Msalato jijini hapa. Mamba alisema kuwa Kamati ya Siasa Kata ya Msalato ina wajibu wa kufuatilia na kusimamia miradi yote ya maendeleo inayotekelzwa katika kata hiyo. “Kamati ya Siasa Kata ya Msalato mradi huu ni wa kwenu, msisubiri Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma kuja kukagua. Lazima muwe mnapanga ratiba zenu kukagua miradi hii. Serikali ya awamu ya sita inaleta fedha nyingi kwenye kata kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, jukumu lenu ni kusimamia utekelezaji wake na thamani ya fedha ionekan...

KAMATI YA SIASA WILAYA YA DODOMA YAPONGEZA UJENZI KITUO CHA AFYA ILAZO

Image
  NA. Dennis Gondwe, ILAZO KAMATI ya Siasa ya Wilaya ya Dodoma imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo unaoendelea na kusema kuwa wilaya inaoga maendeleo. Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma wakikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba alipoongoza Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo kinachojengwa jijini Dodoma. Mamba alisema “nianze kwa kumshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuitendea mema Dodoma hasa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Sisi tunaoga maendeleo. Kata ya Nzuguni, Ipagala na kata za jirani. Mradi huu ni wenu na ni jukumu lenu kuutunza ili uwe endelevu”. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma, Shaban Shaban alisema kuwa wasimamiz wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo wapo makini. “Kwa jinsi tulivyoukagua tu mradi tumeona kuta zimenyooka vizu...

KAMATI YA SIASA MKOA WA DODOMA YAPONGEZA USIMAMIZI UJENZI SHULE YA MIYUJI B

Image
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI KAMATI ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma imepongeza usimamizi mzuri wa shule mpya inayojengwa ya Miyuji B iliyopo Kata ya Miyuji jijini Dodoma na kusema kuwa shule hiyo itawapunguzia hadha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi. Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga akisisitiza jambo Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga alipoongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Miyuji B inayojengwa Kata ya Miyuji. Mbaga alisema “nimpongeze mkuu wa shule jirani ya Miyuji anayesimamia ujenzi wa shule hii kwa kazi nzuru na usimamizi mzuri. Hakika majengo ni mazuri na yanapendeza. Aidha, niwapongeze na wahandisi kwa kusimamia vizuri shule hii. Maeneo mengine wahandisi hawasimamii miradi ya ujenzi jambo linalopelekea miradi mingi kujengwa chini ya kiwango kwa kukosa usimamizi”. Vilevile, kiongozi huyo wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma alielezea kufurahishwa kwake kwa taa...

NYUMBA YA WALIMU YAJENGWA KWA VIWANGO SHULE YA MTEMI CHILOLOMA

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA KAMATI ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na viwango vya ujenzi wa nyumba ya walimu ‘two in one’ katika Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma na kusema kuwa utakuwa imejengwa kwa viwango bora. Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga akiongea na umma baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya walimu (two in one)  Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga alipoongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mbaga alisema kuwa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na ujenzi wa nyumba ya walimu shuleni hapo. “Mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu ni nzuri na umejengwa na kusimamiwa vizuri. Huko zamani wahandisi walikuwa nyuma katika kusimamia miradi ya ujenzi, lakini siku hizi wapo mstari wa mbele na wanafika katika kusimamia miradi ya ujenzi. Jukumu letu ni kuwaambia wananchi kazi nzuri inayofanywa...

UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA MTEMI CHILOLOMA MSAADA KWA WALIMU

  Na. Dennis Gondwe, DODOMA MRADI wa ujenzi wa nyumba ya walimu (mbili kwa moja) katika shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma utawasaidia walimu kukaa mazingira ya shule jambo litakaloongeza ufanisi katika utendaji kazi wao na kutoa matokeo chanya. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma, Mwl. Livinus Tanganyika alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu (two in one) katika Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma iliyopo Kata ya Hombolo Makulu Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mwl. Tanganyika alisema kuwa serikali kupitia mradi wa kuboresha shule za sekondari (SEQUIP) ilitoa jumla ya shilingi 95,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu ambapo lilikuwa ni hitaji kubwa kwa sababu eneo la shule liko mbali na eneo la makazi ya watu. Fedha za ujenzi ziliingizwa katika akaunti ya shule tarehe 20/6/2023 na kuvuka mwaka na kuanza kutumika katika mwaka wa fedha 2023/2024. Akiongelea utekelezaji wa mradi huo alisema kuwa uli...

Waziri Mkuu Majaliwa Avutiwa Na Mchango Wa NBC Kuchochea Kasi Ya Kilimo, Biashara Na Michezo

Image
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameonyesha kuvutiwa na mchango unaoendelea kutolewa na benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kukuza sekta mbalimbali nchini ikiwemo kilimo, biashara na michezo kupitia huduma na ufadhili wa benki hiyo kwenye maeneo hayo. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja wa NBC tawi la Lindi Bw. Iovin Mapunda (Kushoto) na Meneja Mahusiano wa beniki hiyo Bi Brendansia Kileo (Katikati) wakati alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moj...

Mkurugenzi Mkuu Wa VETA Afanya Ziara Ofisi Za VETA Kanda Ya Kati Na Chuo Cha VETA Dodoma

Image
    MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Prosper Mgaya amefanya ziara katika Ofisi za VETA Kanda ya Kati na Chuo cha VETA Dodoma ambapo ametembelea karakana kujionea shughuli za mafunzo na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Kanda na Chuo.   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Prosper Mgaya akiwa katika Chuo cha VETA Dodoma na Ofisi ya   VETA  Kanda ya Kati Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo tarehe 13 Novemba, 2023, Dkt. Mgaya ameainisha mikakati mbalimbali ya kuboresha utoaji mafunzo ya ufundi stadi nchini ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi na kuwawezesha kuendesha shughuli za kiuchumi kwa ufanisi.   Mikakati hiyo ni pamoja na kuongeza ubunifu kwenye kuandaa kozi za muda mfupi zinazojibu mahitaji halisi ya jamii, kuboresha vifaa vya utoaji mafunzo vinavyokidhi ukuaji wa teknolojia na kuhakikisha ubiasharishaji wa vifaa vya kiubunifu vinavyozalishwa kw...

WAZIRI JAFO AWATAKA WAWEKEZAJI WA BIASHARA YA KABONI KUWA WAWAZI

Image
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo amewataka wawekezaji wa Biashara ya Kaboni nchini kuwa wawazi katika biashara hiyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo na viongozi mbalimbali wakionesha mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Bilioni 4.7 aliyoikabidhi kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na Biashara ya Kaboni Ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya sh. bilioni 47 kwa wakazi wa Wilaya za Kiteto na Mbulu ambazo zimenufaika na mradi huo mkoani Manyara leo Novemba 14, 2023. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Jafo amewaelekeza wawekezaji kuwa na vyeti vinavyoonesha mahali walipouza bidhaa zao ili kuwa wawazi kwa mujibu wa kanuni ya 4 ya Sheria ya Mazingira inayowataka kuwa na uwazi katika biashara zao. Kwa muktadha huo amewataka kuwa wawazi zaidi na mchanganuo unaoonesha mwanakijiji na mwekezaji wananufaikaje na Biashara ya...

Kamati Ya Bunge Ya Mambo Ya Nje, Ulinzi Na Usalama Imeridhika Na Uendeshaji Na Uendelezaji Wa Kiwanda Cha Maji Cha Uhuru Peak

Image
  KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeridhika na uendeshaji na uendelezaji wa Kiwanda cha maji cha Uhuru Peak kinachoendeshwa na Suma JKT baada ya kuongeza uzalishaji wa maji. Hivyo, imeyataka mashirika ya umma, Wizara na taasisi za serikali zinunue maji ya Uhuru Peak ili kuendeleza ukuaji wa kiwanda hicho.   Akizungumza leo walipotembelea kiwanda hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Tanzania Vita Kawawa amesema maagizo ya serikali yalielekeza taasisi za serikali wanapoandaa shughuli mbalimbali wanunue maji yanayozalishwa na Suma JKT.   Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Tanzania Vita Kawawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Maji cha Uhuru Peak kilichopo JKT Mgulani jijini Dar es Salaam leo Amesema hapo awali kiwanda hicho kilikuwa kinazalisha lita 250 kwa saa na baada ya kufunga mitambo mipya yenye uwezo mkubwa wanazalisha lita 10...